Mafundi wa Kitanzania badilikeni

Mafundi wa Kitanzania badilikeni

Kingine tabia za mafundi ukipeleka kitu jitahidi uwepo la sivyo atatoa vitu vizuri vizuri ataweka vibovu
Hili ni tatizo sugu sikutaka kuligusia maana najua linajulikana. Hili wanafanya hasa mafundi wa vifaa vya elektroniki kuanzia simu hadi computer, unaenda na tatizo moja unaondoka na matatizo manne. Kuna sehemu yao special sana motoni.

kingine mafundi ujenzi ndio shida sana bila usimamizi utapigwa mifuko ya simenti mpaka unyooshe maelezo kiufupi mafundi wa kibongo ni shida tu
Hao mafundi ujenzi ndiyo wameshindikana kabisa
 
siwezi kupiga deki sehemu smbayo nmefnya kaz kama kuna uchafu mwmgi ntatpa tu sio kusafsha hyo n kaz yako
Hakuna anayesema upige deki. Acha sehemu karibia na ulivyoikuta, siyo unaacha mazagazaga yako yametapakaa kila sehemu. Kama kuna uchafu umetengeneza ukusanye, walau urundike sehemu moja usepe zako. Ukipenda kazi yako hili jambo wala hauhitaji kufundishwa
 
Vyuo vyote vya ufundi somo la kwanza kabisa ni usalama sehemu ya kazi, usalama wako wewe fundi usalama wa vifaa vyako na usalama wa kazi unayo fanya.
Sambamba na hilo ni usafi, kwanza usafi wako wewe na vifaa vyako usafi wa kazi yako na usafi wa eneo la kazi.
Kuanza usafi kabla ya kazi na baada ya kazi ni kanuni namba moja ya fundi.
Nilikuwa nahisi lazima watakuwa wanafundishwa hili suala la usafi na uaminifu ila labda inahitaji msisitizo zaidi au labda ni tatizo la uaminifu lililopo katika jamii nzima
 
Mi pia hiyo tabia siipendi, fundi anakuja kubadili kitambaa cha kochi anabeba alivyotoa kama vile mali yake.

Kuna mmoja alikuja kuweka wall paper gundi yangu, kamaliza kazi akabeba yote iliyobaki kama vile robo tatu li wall paper lenyewe wiki tu likabanduka....aliniudhi sana. Mxyuuuu
Yaani umemlipa kwa kazi aliyofanya, bado anaona anastahili kubeba material iliyobaki. Kazi zenyewe wanafanya kimagumashi, baada ya muda mfupi unarudi pale pale.
 
Fundi yoyote lazima akuibie kimoja kati ya
Pesa
Muda
Material

Sasa nI wewe uchague akuibie kipi, ila ukiwa mzembe anaweza kukuibia vyote
 
Yupo mmoja ni fundi kuchomelea alikuja kufanya kazi akaunganisha nyaya zake kutokea kwenye sakiti breka ya ndani kwangu kumbe wakati anaunganisha alitakiwa waya mmoja kama sio zote azifungie ile tap nyeusi ila akapuuzia akaendelea na kazi kumbe zile zikagusana ghafla ukazuka moshi mweusi mara moto huu hapa bahati nzuri tuliwahi kuudhibiti maana alikuwepo binti ndani anaangalia TV ndiye aliyetoa taarifa. Sasa nikakaa nikamuuliza shida nini ndio kuniambia aseeh nilishikwa hasira.

Alipomaliza kwa siku hiyo nikamwambia aseme anadai kiasi gani nikamlipa akaondoka na vifaa vyake. Nilikasirika sana mpuuzi yule anataka kunichomea nyumba yenyewe ya urithi. Kule alikokua anachomelea(mlango wa banda la kuku) kulikaa karibu wiki 3 ndio nikaja kutafuta mwingine akamaliza kazi. Naamini yule wa kwanza atajifunza akipata kazi nyingine huko. Mafundi kuweni makini msifanye kazi kimazoea
 
Wanatamaa sana.... kuna mmoja alivyokuja hom akakuta nina wadogo zangu wakali akalleta tamaa za kutaka tumuozeshe kaacha kilichomleta
 
Yupo mmoja ni fundi kuchomelea alikuja kufanya kazi akaunganisha nyaya zake kutokea kwenye sakiti breka ya ndani kwangu kumbe wakati anaunganisha alitakiwa waya mmoja kama sio zote azifungie ile tap nyeusi ila akapuuzia akaendelea na kazi kumbe zile zikagusana ghafla ukazuka moshi mweusi mara moto huu hapa bahati nzuri tuliwahi kuudhibiti maana alikuwepo binti ndani anaangalia TV ndiye aliyetoa taarifa. Sasa nikakaa nikamuuliza shida nini ndio kuniambia aseeh nilishikwa hasira.

Alipomaliza kwa siku hiyo nikamwambia aseme anadai kiasi gani nikamlipa akaondoka na vifaa vyake. Nilikasirika sana mpuuzi yule anataka kunichomea nyumba yenyewe ya urithi. Kule alikokua anachomelea(mlango wa banda la kuku) kulikaa karibu wiki 3 ndio nikaja kutafuta mwingine akamaliza kazi. Naamini yule wa kwanza atajifunza akipata kazi nyingine huko. Mafundi kuweni makini msifanye kazi kimazoea
Hatari sana. Kama mdau mmoja alivyoshauri, hii fani inabidi wapewe leseni na kuwe na utaratibu wa kuripoti na kurekodi review za wateja aliowahudumia na review hizo mtu yoyote aweze kuwa na uwezo wa kuziangalia pale anapotaka kuchagua fundi. Itawafanya wawe makini zaidi.
 
Hapa nitaongea kwa ufupi sana na hii mada inawahusu mafundi wa aina zote hasa wale wanaokuja majumbani au maofisini kufanya matengenezo fulani kuanzia mafundi ujenzi, wapakaji rangi, fundi umeme hadi fundi wa maji.

Kuna mambo mawili ambayo yanakera sana ambayo wanafanya mafundi wa Kitanzania.

Kwanza, ni ishu ya kutofanya usafi baada ya kumaliza kazi. Mafundi wetu hawa hawadhani kuwa ni wajibu wao kuacha pasafi mazingira waliyofanyia kazi. Hili nimeliona hata kwa wale ninaodhani watakuwa wamepitia mafunzo. Nashauri vyuo vya ufundi vifundishe na kusisitiza utaratibu sahihi wa fundi kufanya kazi iliwemo kuacha mazingira safi baada ya kazi.

Pili, ni suala la kuondoka na vifaa vya mteja. Anaweza kuja kubadili au kufix kitu fulani, akimaliza kazi wengi wana tabia ya kuchukua kifaa alichobadilisha. Usipokuwa makini, kama siyo kifaa chote basi kuna kitu alichobadili atabeba bila kuomba au kutoa taarifa.

Kwa leo nitagusia hayo tu.

Wengi sio waaminifu wala sio reliable. Ndio maana huwa hawakui katika fani zao. Wanafanya mambo kwa namna ile ile miaka nenda miaka rudi. Na huwezi kuwatumia nje ya Tanzania, maana mnaweza kujikuta mmepigwa na kufungwa bila utaratibu
 
Back
Top Bottom