Mrejesho mkuu ni kwamba gari iko poa tu, tangu nmenunua sijawahi kugusa kwenye engine zaidi ya kubadilisha engine oil, shock up pia zilizingua nikabadilisha japo nlienda kwa mafundi nnaowaamini maana nlikuwa nackia sauti inagonga kwa mbalii sasa nikapeleka garage moja hapo sinza wakaangalia wakasema ni tairod end nikabadilisha tatzo likaendelea nikarud tena wakasema inabidi kushusha kifua nikashusha lakn tatzo likaendelea, ilibid niwamind sana maana nikama hawana uhakika na tatzo sasa wanakufanya unaingia gharama kwa vtu ambavyo havikuwa na ulazima, na wakishafungua kitu hata kama hakijaharibika wanalazimisha tu kuwa ni kibovu tubadilishe sasa baadaye fundi yule yule aliyesema ni kifua akasema tena itakuwa shock up daah nlichoka ila mwisho wa siku nliweka shock up mpya tatizo likaisha, ila kiu ukweli hawa mafundi wetu wanabuni matatzo hawana uelewa mzuri, so tatzo kubwa ni hilo gari haijawahi kuwa na shida nyingne