DOKEZO Mafundi wengi huikimbia miradi ya serikali ya ujenzi kutokana na mlolongo mrefu wa malipo!

DOKEZO Mafundi wengi huikimbia miradi ya serikali ya ujenzi kutokana na mlolongo mrefu wa malipo!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,280
Reaction score
2,522
Wakuu

Katika kipindi HIKI cha ujenzi wa madarasa nchini unaoendelea, nimefanya mazungumzo na mafundi wakuu na wakuu wa shule mbalimbali na kukutana na malalamiko kuhusu mlolongo mrefu sana wa upatikanaji wa fedha za malipo kwa mafundi wakuu na vibarua wao!

"Unajuta day worker anaomba hela yake ya siku, wakati maafisa wanataka hadi jengo lisimame lionekane ndio wawe tayari kusaini cheque za malipo, basi ni tabu tupu hadi baadhi ya mafundi wanasusa kazi au kuondoka kabisa kwa kukosa uvumilivu! Haya ni malalamiko ya fundi mkuu ndugu kazimili Zengo.

"Kwa nini mambo yote yasisimamiwe na mkuu wa Taasisi husika kuanzia kusaini cheque na malipo kufanyika kutokana na KAZI inavyoendelea!? Awepo tu mkaguzi mkuu wa kuangalia matumizi ya Fedha yanaendana na hali husika ya jengo linavoendelea, kuliko kuhangaika kusaka saini za maafisa pale wilayani na WAKATI mwingine wanaringa sana kusumbua kutia sahihi zao na kukwamisha malipo KWA WAKATI kwa mafundi na vibarua wa miradi ya serikali!

"Wakati Mwingine tunalazimika kukopa Fedha au kutumia akiba yetu Ili KUWALIPA na kusubiria KWA muda mrefu hadi fedha zitapoidhinishwa na maafisa wilayani!

Mi naona ipo haja ya Serikali kuwaamini wakuu wa Taasisi Ili washulikie malipo kirahisi kuliko ilivyo sasa, yaani mkuu wa Taasisi ndio aunde kamati ya malipo na ujenzi na cheque zote zisainiwe na malipo ya fanywe na yeye huku akikaguliwa na engineer wa halmashauri KWA kadri mradi inavoendelea kuliko Sasa ambapo mafundi na wasimamizi wanafanya KAZI nkwa mikopo Hadi mradi unapokomaa ndio wanalipwa hii husababisha mafundi Hao kususia miradi ya serikali na wakuu kuwa katika heka heka za mradi kutokamilika KWA wakati na kukoromewa kama watoto na maafisa Hao Hao walio hujumu mradi KWA kutokusaini documents KWA wakati Ili kuwezesha malipo!

Serikali itazame hilo,pale halmashauri wabaki ma engineer kama wakaguzi wakuu wa miradi na thamani ya Fedha na wakuu wa Taasisi wawe ndio wasimamiaji na waidhinishaji wa malipo na kusaini cheque zao za malipo yaani wawe ndio wawe watoaji Fedha na walipaji KWA kutumia bodi za taasisi na kamati za Fedha!

Naamini wahusika watapitia na kulifanya kazi hili!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu
 
Back
Top Bottom