Mafundi wetu wanakwama wapi?

Mafundi wetu wanakwama wapi?

Mnyiramba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2022
Posts
1,141
Reaction score
3,119
Mimi ni kati ya watu wenye ndoto za kujenga ghorofa, lakini mada nyingi zimekuwa zinaibuka humu kwamba gharama ya ghorofa ni kubwa sana hasa gharama kubwa inakuwa ni msingi na nguzo zile zinazosimamisha ghorofa!

Lakini nimejatibu kufanya utafiti mbali mbali wenzetu wanajenga vipi huko kwenye mabara mengine!

Nilichogundua wenzetu kuna ghorofa zinajengwa bila zile nguzo kabisa yaani ghorofa inasimama na kuta tu pekee, na inakuwa imara kabisa!

Je, wafundi wetu wanakwama wapi? ama ndio wamekariri kuwa bila nguzo huwezi kujenga ghorofa?
 
Mkuu kwenye research yako umegundua wenzetu kwenye ujenzi wao wanatumia material gani kusimamisha ukuta .

Je, ni masonry block au concrete
 
Aisee...Fundi Maiko acha kabisa...
Nenda kasome Beams and Deflections...(Structural Mechanics)
Hakuna ghorofa inayojengwa bila kuwa na beams( nguzo)..1
Nadhani huwa anaona maghorofa ambayo nguzo zake huwa zinafichwa vizuri kwa matofari.Basi,yeye hudhani hakuna nguzo.Ghorofa bila nguzo lafaa nini basi kama si ghorofa lililojengwa hewani?
 
Aisee...Fundi Maiko acha kabisa...
Nenda kasome Beams and Deflections...(Structural Mechanics)
Hakuna ghorofa inayojengwa bila kuwa na beams( nguzo)..1
Acha uongo,
Ni ulaya hapa(Ukraine)
Nionyeshe nguzo ziko wapi hapa[emoji848]
IMG_20220814_101441.jpg
 
Picha zinadanganya sana...fuata ushauri wa fundi
 
Mimi ni kati ya watu wenye ndoto za kujenga ghorofa, lakini mada nyingi zimekuwa zinaibuka humu kwamba gharama ya ghorofa ni kubwa sana hasa gharama kubwa inakuwa ni msingi na nguzo zile zinazosimamisha ghorofa!

Lakini nimejatibu kufanya utafiti mbali mbali wenzetu wanajenga vipi huko kwenye mabara mengine!

Nilichogundua wenzetu kuna ghorofa zinajengwa bila zile nguzo kabisa yaani ghorofa inasimama na kuta tu pekee, na inakuwa imara kabisa!

Je, wafundi wetu wanakwama wapi? ama ndio wamekariri kuwa bila nguzo huwezi kujenga ghorofa?
Gharama kubwa hailetwi na nguzo.
1. Msingi lazima uwe imara, hii nikwasababu utabeba mzigo mkubwa.
Beam na slab pia hula mpunga wa maana haswa. Kwahiyo nguzo umezionea tu
 
Gharama kubwa hailetwi na nguzo.
1. Msingi lazima uwe imara, hii nikwasababu utabeba mzigo mkubwa.
Beam na slab pia hula mpunga wa maana haswa. Kwahiyo nguzo umezionea tu

Hoja ni kwamba tunaweza kujenga ghorofa bila nguzo!,tujikite kwenye hoja husika
 
Kazi kuu ya column ni kubeba mzigo (loads) wa slab, column iliyopo juu yake (kwa jengo la ghrofa zaidi ya moja) na truss then kusafirisha kwenda kwenye msingi!

Sasa! ni kweli kbsa unaweza kujenga ghorofa bila nguzo hata moja na badala yake ukatumia ukuta lakini kuna conditions zake.

1. Ukuta wako lazima uwe (load bearing wall) ukuta ambao unaweza kubeba mzigo na kuusafirisha kwenda kwenye msingi!
Hapa kuna calculations za kufanya ili kujua unene wa ukuta hitajika kutoka na jengo lako! Siri ya majengo hayo lazima ukuta wake uwe mnene kidgo (thickness) ili kuruhusu loads iapply vizuri. (Sasa ww kasimamishe tofal zako za inch 5 zenye thickness ya 150mm[emoji1787] natania tu[emoji1787][emoji1787])

2.Majengo haya ayafai kujenga kwenye maeneo yanayopata tetemeko la ardhi au kukumbwa na land sliding na land subsidence kwa sababu load bearing wall ni very very weak kuresist lateral forces (force inayopiga au kwenda perpendicular na ukuta)

3. Inashauriwa kutumia ujenzi huu pia kwa majengo ya ghorofa chache may be 2 or 3

Nimejitahidi kuhighlight kidgo juu juu naamini mtapata cha kujifunza!
 
Kazi kuu ya column ni kubeba mzigo (loads) wa slab, column iliyopo juu yake (kwa jengo la ghrofa zaidi ya moja) na truss then kusafirisha kwenda kwenye msingi!

Nimejitahidi kuhighlight kidgo juu juu naamini mtapata cha kujifunza!

Nadhani picha inajieleza bila hata kupika data za hapa na pale [emoji851]
 
Back
Top Bottom