Mafundi wetu wanakwama wapi?

Mafundi wetu wanakwama wapi?

Kwani humu hakuna maengineers? Au nao hawajui hii. Nyie mliosomea civil eng. Pale mlimani mkuje huku
 
Mimi ni kati ya watu wenye ndoto za kujenga ghorofa, lakini mada nyingi zimekuwa zinaibuka humu kwamba gharama ya ghorofa ni kubwa sana hasa gharama kubwa inakuwa ni msingi na nguzo zile zinazosimamisha ghorofa!

Lakini nimejatibu kufanya utafiti mbali mbali wenzetu wanajenga vipi huko kwenye mabara mengine!

Nilichogundua wenzetu kuna ghorofa zinajengwa bila zile nguzo kabisa yaani ghorofa inasimama na kuta tu pekee, na inakuwa imara kabisa!

Je, wafundi wetu wanakwama wapi? ama ndio wamekariri kuwa bila nguzo huwezi kujenga ghorofa?
Habari,
Ujenzi wa ghorofa bila nguzo inawezekana lakini tu unashauriwa kutumia ukuta wenye upana wa inch 9 au 230mm kwa floor ya chini yaan kuta za chini zijengwe kwa kulaza tofali. Kwenye msingi, nguzo ziishie level ya msingi ilikupa msingi stability nzuri.

Lakini pia aina hii ya ujenzi sio imara. Endapo litatokea tetemeko tegemea nyufa za kutosha au jengo kufail kabisa.

Ghorofa bila nguzo inawezekana lakini sio Salama. [emoji120]
 
Back
Top Bottom