Mafundo ya Maisha ni Nini?

hisown

Member
Joined
Jul 30, 2017
Posts
20
Reaction score
33
Ni matuaini kuwa wote humu jukwaani.

Awali ya yote namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kwa mara ya kwanza kushiriki katika jukwaa hili; natumaini nitapokelewa.

Nimekuja katika jukwaa hili, kama ambavyo kichwa cha habari kinajieleza kufahamu kutoka kwa wajuzi wa mambo kuhusiana na mafundo ya maisha ni nini? Kwanini yanaitwa mafundo ya maisha? Je, yanatokana na nini? Athari zake ni zipi?

Je, haya mafundo ya maisha yanawapata nani hasa? Je, unayatambuaje? Na je, yana tiba?

Kuhusu familia kama kilele cha jamii na jamii yenyewe, wanao ufahamu juu ya mafundo ya maisha? Nini athari zake katika maendeleo ya binadamu?

Nafahamu jukwaa limesheheni watu mbalimbali na wenye ujuzi mkubwa katika nyanja mbalimbali za maisha, mathalani dini, uchumi, teknolojia, utamaduni n.k.

Lengo ni kujifunza na kuelewa zaidi kuelekea kuyajua maisha kwa jinsi yake na yaliyomo ndani yake binadamu.

Natanguliza shukurani, karibuni!
 
Na ufahamu wangu wotee hapa nimetoka kapa hata concept tu ya mafundo sijaijua...
 
Kwa ufupi sana MAFUNDO Hutokana na Neno FUNDO ambalo linaweza kuwa la kitambaa eitha cha Nguo, kamba, minyororo,ngozi ya mnyama, au kitu chochote watakacho tumia kwa maana ya kutaka Kufunga FUNDO..........

Mafundo hutumika kwa ajili ya Uchawi Kumfunga Mtu asifanikiwe jambo fulani.............
Mafundo yakisha fanya huwekwa sehemu mfano Aridhini, Baharini, Chini ya Bahari au Angani...........Ni shida kwa kweli.................!!!!!

Vitu vinavyofungwa Mafundo ni vile vinavyokuhusu kama vile; alama ya nyayo ya mtu au kiatu katika ardhi, kiatu, soksi, picha, C V, Document/karatasi yenye uhusiano na wewe au details zako, nguo za aina yoyote, Hereni, Pete, Cheni, Mkufu, Kivuli cha Mtu, Vitu vyote ulivyowahi kuvishika, vitu vyote ulivyowahi kuibiwa, vitu ulivyoacha kuvitumia, Waste za PAD za akina mama, Vitu vilivyoibiwa au kupoteza na huvikumbuki, Vyombo vya ndani kama vijike, visu, kikombe, vibao vya vyapati, kitabu, kitu chochote chenye link na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…