Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Mafunzo kwa Wathamini na Warasimu Ramani kwa ajili ya zoezi la Uandaaji Vitalu vya Thamani ya Ardhi (Valuation Block) yanaendelea mkoani Kagera
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi nchini (LTIP) ndiyo inayoendesha mafunzo hayo kwa wataalamu wake wa mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ili kuwajengea uwezo.
Mafunzo hayo yanahusisha wataalamu wa fani ya Uthamini na Urasimu Ramani kutoka ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kagera pamoja na halmashauri zote za mkoa huo.
Mthamini Mkuu wa Serikali Bi. Evelyne Mugasha aliwatembelea wataalamu wanaopata mafunzo hayo na kuwaasa kwa kuwataka kuhakikisha wanazingatia mafunzo waayopatiwa ili kutoa huduma kwa weledi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.
Mratibu wa Mafunzo hayo ambaye ni Mthamini kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali Bw. Baraka Mollel amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha na kuwafundisha wathamini na warasimu ramani ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa kipindi hiki ambacho Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaboresha mifumo yake na kuwa ya kidigitali.
Mafunzo hayo yanawafundisha wathamini na warasimu ramani namna ya kuandaa Vitalu vya Thamani ya Ardhi (Valution Block) ili kusaidia utekelezaji wa shughuli za uthamini kama vile Rehani, Uhamishaji Milki na Uthamani kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya serikali.