Mafunzo ya Jeshi, Ufundi Magari na Sabato

Mafunzo ya Jeshi, Ufundi Magari na Sabato

Sosoma Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
312
Reaction score
281
Kijana mwenye umri wa miaka kumi aliketi ametulia akisikiliza kwa makini hotuba yake ya kwanza katika Kanisa la Waadventista wa Sabato. Mhubiri alieleza kuhusu mfanyakazi wa Posta ambaye alipokea barua inayoenda kwa Santa Claus (Babu Krismasi).

Kijana mdogo alikuwa ameandika barua kwa Babu Krismasi, naye alikuwa anatamani sana kupata zawadi ya gari moshi la kitoto la kuchezea. Mfanyakazi huyo wa Posta hakuwa na mtoto, hivyo akaamua kumnunulia mtoto huyo gari moshi hilo la kuchezea. Mvulana huyo mdogo alishàngilia kupokea zawadi hiyo!

Kadri Rosen Nakov alivyosikiliza kisa hicho, yeye pia kama mtoto alisisimka kwa furaha. Naye pia alikuwa na shauku ya kupata gari moshi la kitoto la kuchezea hapo nyumbani mwao Sofia, Bulgaria.

Kisa hicho kilimgusa moyo wake, naye akarudi kuhudhuria kanisani hapo Sabato iliyofuata. Na pia Sabato iliyofuata. Muda si mrefu alifanya urafiki na watu hapo kànisani na kufanya urafiki na Yesu.

Baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari, Rosen alihitajika kujiunga na elimu ya jeshi kwa mujibu wa sheria, kulingana na nchi hiyo ya Kikomunisti nyakati hizo. Ila alikuwa na chaguzi mbili: Kujisajili kuwa askari kwa miaka miwili, au kujisajili kufanya kazi kiwandani kwa miaka mitano. Rosen Nakov alichagua kufanya kazi kiwandani ili awe huru kuishika Sabato. (soma Kutoka 20:8-11).

Yumkini Waadventista kumi walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda kikubwa cha magari huko jijini Sofia. Kijana Rosen Nakov alichagua kufanya kazi hapo,(soma Isaya 58:13, 14) badala ya kwenda jeshini kwa mujibu wa sheria. Alipofika kiwandani hapo, Rosen Nakov alikutana na Mwadventista ambaye alimwalika apate kujiunga katika idara ya kuweka injini kwenye magari.

Kijana Rosen Nakov alienda katika ofisi ya kiwanda hicho ili kuomba apewe nafasi hiyo ya kazi. Hata hivyo meneja wa kiwanda hicho aliziangalia karatasi za maombi za Rosen na kugundua kuwa ana uzoefu wa ufundi magari. "Kwa nini unaomba kazi ya kuweka injini kwenye magari?" Meneja alimhoji. "Yakupasa ukakarabati injini za magari kule kwenye karakana."

Mara moja Rosen Nakov aliuliza endapo kazi hiyo inatoa ruhusa kwenda kanisani siku za Sabato. (soma Ezekieli 20:20, 12) "Ndiyo," alijibu Meneja. "Kazi hiyo hufanyika Jumatatu hadi Ijumaa."

Meneja akamuelekeza kijana Rosen kwa meneja uajiri akakamilishe karatasi zake za maombi. Rosen Nakov alipowasili karatasi zake kwa Meneja Raslimali Watu ghafla akaulizwa, "Kwa nini uombe kazi ya umakanika kwenye karakàna ya injini za magari? Wewe unafaa kwenda karakana ya kuunda injini ndogo za magari."

Siku ya kwanza ya Rosen kwenye kiwanda, alitambua kwamba watu wengine sita walifanya kazi kwenye duka la injini ndogo. Wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana, mfanyakazi mmoja alimwuliza Rosen Nakov, "Unafahamiana na nani wa cheo cha juu hapo kiwandani?"

"Je unamaanisha nini?" alihoji Rosen.

"Lazima uwe na rafiki wa ngazi ya juu" mtendakazi mmoja alimweleza.

Rosen aligundua kuwa karakana hiyo ya injini ndogo za magari ilikuwa ni moja ya sehemu zilizopendwa sana kwa kazi kiwandani humo.

Wengi wa wafanyakazi kiwandani hapo walifanya kazi ngumu zenye kuchafua. Ila kazi katika karakana ya injini ndogo ilikuwa rahisi kidogo na iliyo safi. Marafiki wote wa Rosen walipata kazi kwa vile walikuwa na marafiki wenye vyeo ngazi za juu.

Rosen alitambua kuwa kwa kumheshimu Mungu kwa kuishika Sabato (Luka 4:16), Mungu amemheshimu kwa kumpatia kazi iliyotamaniwa sana na wengi.

Wakiendelea kula, mtu mmoja kutokea upande mwingine wa meza alimsisitiza Rosen atoe jibu, "Ni nani aliye rafiki yako?" Rosen alijibu kwa kuelekeza kidole chake mbinguni na kusema, "Rafiki yangu yupo juu mbinguni."

Tangu siku hiyo, kila mmoja katika karakana hiyo ya injini ndogo, na pia katika karakana kuu walitambua kuwa Rosen Nakov alikuwa Mwadventista wa Sabato. Wengi walitafuta ushauri kwake wa kiufundi walipojua kuwa ni Makanika mashuhuri. Rosen Nakov alikuwa ndiye Mwadventista pekee katika kitengo cha ufundi magari.

Wakati wa mahojiano Robin alisema, "Waadventista wengi walifanya kazi katika kiwandani, ila hakuna aliyefanya kazi katika karakana, yumkini Mungu alinihitaji mahali hapo."

Rosen, kwa sasa akiwa na umri wa miaka 48, hajui endapo yupo mtendakazi amempokea Yesu kupitia mvuto wake,ila anajua kuwa Mungu alikuwa na mpango maalumu kumweka hapo.

"Kama vile Mungu alivyotumia kisa cha gari moshi la kitoto la kuchezea kuweza kuugusa moyo wangu nikiwa mdogo, pengine alinitaka niwe katika karakana hii ili niguse moyo wa mtu fulani," alisema Rosen. "Bwana mwema anajua namna ya kugusa moyo wa kila mtu."
Barikiweni nyote na Mungu Muumba Mbingu na nchi.

Amani ya BWANA iwe pamoja nanyi katika majukumu yenu ya kila siku.

Asanteni!!!
 
Hivi huko kwenye usabato hakuna hadithi zinazohusu vijana au watu ambao ni Waafrika?

Kila hadithi wazungu tu. Sabato hakuna Waafrika?
 
Imani nisiyoielewa hata kidogo hii. Nikiwa shule ya sekondari nilisoma vipeperushi vingi vya imani hii pamoja na kuwasikiliza katika makongamano yao lakini kamwe sikuwaelewa wanachosimamia kwa ajili ya wafuasi wao zaidi ya kupambana na ukatoliki!
 
Hakuna dhehebu la kipumbavu na lililojaa wajinga kama hili la wasabato. Ni bora watu na wachungaji wenu wawe wanapewa elimu ya dunia kwanza!! , Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuwa msabato maana hata muanzilishi wa kanisa hili William Mirror alilikimbia na kuuomba msamaha ulimwengu kwa uongo aloutabir wa ujio wa Yesu mara ya pili mwanzoni mwaka 1843. Ellen White na mme wake ndo baadae waliliendeleza na awamu hii wakajikita kwenye utabir mpya et yesu atakuja mara ya pili 2050 ,na bwana william mirror alikosea kupiga maesabu yaliyoandikwa katika kitabu cha Daniel sura ya 8
 
Back
Top Bottom