Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
wazo nzuri sana, ila mtawasaidiaje vijana wasiokuwa na ajira kuweza kufanya hiyo shughuli, na ukizingatia mil 5 tayari ni tatizo kwao ili waweze kujikomboa na aza ya kukusanyika kwa nafasi chache za ajira?
nasubiri picha mkuu, ninakauchochoro ka hatua 30x15 nikifanyie kazi, si umesema 5x8 unapata 600,000/= kwa mwezi!
Yaani nikishaona mtu katika biashara zetu za kawaida anaingiza mawazo ya kina Adam Smith, Mara sijui return of investment, accounting rate of return na mengine kama hayo, huyo hata umpe 1,000,000,000 afanye biashara kesho yake tu anafilisika. Na kawaida watu hao wengi unawakuta ana MBA au amesomea "masomo ya biashara", anadhani biashara ni vitabu, kibongobongo wanaotoboa katika biashara hata Adam Smith hamjui wala Hana mpango wa kumjua milele! Muuzlie S.H. Amon kama anamjua Adam Smith!
Ni jambo jema kutambua kuwa mafanikio ya mtu yoyote hayategemei usomi wake, wala ujuzi nk. Mafanikio yanategemea ATTITUDE. Na Attitude ni mitazamo ya watu na inatofautiana. Jambo lolote unaweza ukaliangalia katika mtazamo hasi au chanya. The choce is yours!
Asante sana kwa mchango!
There is a doubting Thomas for everything on earth. Ningependa kukukaribisha kwangu shambani eneo la Nairobi ukaone production ya kila wiki kisha upate imani. 20tons in a year with proper management and with following agronomy instructions is quite conservative.
Ndugu zangu watanzania naomba nitoe tahadhali kuhusu uanzishwaji wa greenhouse hasa haya yanayotangazwa kibiashara kabla ya kufanya uamuzi wa kuyanunua nawaomba mpate ushauri kutoka kwa wataalam wa kilimo. kuna mambo ya msingi sana yanatakiwa yazingatiwe emissivity na transmissivity ya cladding/greenhouse cover ni muhimu sana wafanyabiashara wengi wamekuwa wakidanganya hivyo kupunguza efficiency ya greenhouse yenyewe. pia greenouse inategemea na location uliyopo, hali ya hewa na availability ya resources. mimi ni mtaalam wa kilimo ambaye kwa sasa nasomea greenhouse hort nchini uholanz be careful my people.KWA NINI UWE MASKINI?
JE, UNGEPENDA KUVUNA NYANYA NYINGI KILA WIKI NA KUJIPATA KIPATO KIKUBWA KUPITIA KILIMO CHA GREEN HOUSE?
View attachment 165705
Team ya AMKA NA BADILIKA ya CONSNET GROUP ikishirikiana na wataalamu wa GREEN HOUSE katika maeneo ya joto AFFORDABLE GREENHOUSE kutoka Kenya wanapenda kukujulisha kuwa unaweza kujengewa GREEN HOUSE ya ukubwa wa Mita 8 kwa Mita 15 na kupanda mazao upendayo ya bustani kama Nyanya; Pilipili Hoho; Vitunguu; Bilinganya; Vitunguu; Matango nk ambayo yanaweza kukupatia zaidi ya tani zaidi ya 20 kwa Mwaka na kukuingizia kipato kikubwa.
Kujengewa GREEN HOUSE moja ya 8M X 15 M (Kutumia mirunda na mbao za dawa) ni TZS 5.0 Millions Tu na unajengewa katika kipindi cha wiki 2 pamoja na kupandiwa mazao. Pesa hiyo inahusisha mbegu za kisasa, mbolea, madawa, kupima udongo na maji maabara, tank la lita 1000, drip irrigation system, na mafunzo na kujengewa.
Kwa sasa zipo KITS za kutosha za Green House. Kama utapenda kujengewa Green House na bajeti iko tayari, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba: +255 755 285 023
mkuu hapo ndiyo bussiness as usual, tatizo ni soko na ndiyo maana hawataki kupasua kichwa sana , hichi kilimo kinafaa sana sehemu yenye mahotel ya kitalii , lakini kwa sisi wengi wetu tunatumia kwa matumizi ya nyumbani , bora kulima vitunguu . na ni vema wakasoma masoko ya sehemu husika kuliko kuwajengea tu , yaani ni vema kutoa smina ya biashara na kilimo
Mkuu nipo iringa, labda nijiulize, mimi eneo langu halipo tambarare, lina mteremko kidogo, pia nimejenga fensi ya ukuta eneo la ndani ni mita 9 kwa 18 je litafaa?
Ukiweka kivuli mimea itastawi vp wakati yenyewe inahitaji mwanga ili iweze kutengeneza chakula chake (This does not sound proffesional)Kaka, kwa greenhouse ambayo imejengwa kwa small scale farming hauhitajiki kuwa na umeme ili kucontrol hali ya joto. Kulingana na mahali unapotaka kulima, tunajenga greenhouse ambazo kwa sides ziko na ventilation 70%. Hii inahakikisha kwamba kuna flow ya hewa from one side to the other, na kiwango cha joto kinakuwa chini. Kama sehemu yako ina baridi, tunajenga nymbaa ikiwa na curtain ili wakati wa baridi unafunga curtain ili nyumba isipoteze joto.
Kwa sehemu za joto kali kama vile pwani, tunaweza kutumia curtain-net nyeusi ambayo inakupa kivuli ndani ya greenhouse yako na hivyo mimea yako itastawi.
Ndugu zangu watanzania naomba nitoe tahadhali kuhusu uanzishwaji wa greenhouse hasa haya yanayotangazwa kibiashara kabla ya kufanya uamuzi wa kuyanunua nawaomba mpate ushauri kutoka kwa wataalam wa kilimo. kuna mambo ya msingi sana yanatakiwa yazingatiwe emissivity na transmissivity ya cladding/greenhouse cover ni muhimu sana wafanyabiashara wengi wamekuwa wakidanganya hivyo kupunguza efficiency ya greenhouse yenyewe. pia greenouse inategemea na location uliyopo, hali ya hewa na availability ya resources. mimi ni mtaalam wa kilimo ambaye kwa sasa nasomea greenhouse hort nchini uholanz be careful my people.
Agric pays Do it.
Mkuu vipi kuhusu janga la upepo? Hii makitu siyo kwamba inaweza kuvulumishwa na upepo halafu 5m ndo inateketea hivyo? Au mna utaratibu wa bima? Na hiyo picha uliyotuwekea hapo ni greenhouse za Tz au za Ulaya mkuu umeiweka tu ili kutuvuta?
Wazo ni zuri nimelipenda, usije nishawishi ka-plot kangu ka 20m x 40m nikakageuza mradi kwa kujenga greenhouses za kutosha! Ila sijui kama mipango miji wanaweza kuruhusu hii kitu ifanyike katikati ya mji?
Kwamba kuna green house wala halina ubishi.... nazijua sana pengine kuliko wewe. Mimi niko kwenye namna ''ulivyopaisha'' mapato yake vs bei unayouza. Utafikiria rocket ya kwenda mwezini!
hyo inawafaa nyie wa mjini mnaotaka kulima kwenye lami,kw cc wakulima haitufai kabisa.embu fikiri eneo 5*8m utazalisha nn?nahapo lazima uwe na systm ya croprotation ukilima nyanya then kitungu.embu niambie kwenye kitungu kwa eneo hlo utapata gunia2 ukiuza 50alfu utapata laki kw miez4,kwenye nyanya ukipanda mbegu eden utapata debe30 na c zaidi ukiuza kwa alfu20 kwadebe utapata laki6 hapo umekula miezi 4 hadi 5 ukijumlisha nahyo yakitungu unamiezi 9 mwaka umeisha umepata laki8.ukipanda mbegu ana utapata cyo zaididebe 50 ukiuza kwa ishrni alfu utapata milion ukijumlisha nakitunguu una milion laki2.hyo ndyo hesabu zako za greenhause otherwise niambie unatumia mbegu gani ili nipate kipato kikubwa kwa eneo ndogo kiac hicho.sbb 5milion nikiamua kulima nyany nawezakulima eka3 yanyanya nakm nikitungu nikijibana nalima eka3 nakapata return kubwa tu.
Kwa Mwanza mnapatikana wapi?
Nakuombea uzima mkuu, natamani kuona hii kitu ikiwa applicable .... nitakuwa member, kwa sasa settlement yangu haijatulia... nakusupport ila tukumbuke kuwasaidia na wanaotaka ila wasio na uwezo!
hi ki2 kwavile mzungu analima gorofani na sisi pia tunaka kulima gorofani bila sbb yakujua kwnn analima gorofani.wenzetu ulaya wanatumia greenhause sbb ya ufinyo wamaeneo je na sisi wenye maeneo namapori yanalala tu tuanze kujinyima kwenye ka green hause.poa lakini nisijenamharibia mshkaji dili yake
Hivi jamani, hao watanzania wa kawaida ndo wapi?
Nauliza kwa sababu siku hizi chochote kile utasikia ..watanzania wa kawaida....anayekula rushwa..anayeiba kodi..who ever is doing anything or nothing..anajificha kwenye mgongo wa 'watanzania wa kawaida'. TANESCO, DAWASCO..nk wakisema lipa kiasi fulani cha gharama upewe umeme..utasikia watanzania wa kawaida hawawezi hizo bei..sasa jamani..unataka hizo huduma upewe bure? Hata kama serikali ingetoa ruzuku..bado..hayo mashirika kusudi ya survive..lazima yatoe huduma bora..na huduma bora lazima zilipiwe. Jamani tufike sehemu tukubali..maendeleo ni mtu mwenyewe. Sasa ulitaka hiyo green house ujengewe bure? au ulitaka wacharge bei gani? Everything has a cost. Ukiangalia huo mchanganuo..its fair kabisa..in a sense kwamba hata anayefanya hiyo kazi anataka apate faida japo kidogo na yeye aweze kuendesha maisha yake.
Utasikia..bei zimepanda..itaathiri watanzania wa kawaida...Anything done....hata iwe na good intention kivipi..we simply become negative..je hao watanzania wa kawaida wataacha kuwa wa kawaida lini? All in all..watanzania tuache kiswahili kirefu na kukata tamaa. We should be ready to take responsbilities kwa maisha yetu. Kipimo cha utu ni vile vile..kushiriki kufanya maamuzi makini...mfano unapopewa fursa ya kupiga kura..unaichukuliaje? unachagua viongozi kwa vigezo vipi?...Tafadhali fahamu kwamba maisha hayana dezo. Popote pale. Kwa hiyo..wewe ukiona kila siku ni mtanzania wa kawaida..tafakari..chukua hatua.
The biggest challenge of WE Tanzanians ni kufikiria kwamba..somebody else (whether serikali au raia wengine) will think and act on our behalf...ufanye ujinga....take poor choices or decisions...utegemee wengine watakuonea huruma... That will never happen until Jesus (for those who believe in this man) comes back. Ndo maana utakuta hata mtaani barabara mbovu.....watu wanakaa wanasubiri serikali..yaani hata kujimobilize..wafukie mashimo..wapi...ukiangalia mtaa umejaa maghorofa..nje ya geti..ni uchafu na mashimo..lakini kuona raia wanachukua hatua madhubuti kuweka sawa mambo..ni ngumu. Mimi sijui hii tabia ya kuwa tegemezi na kutaka kuonewa huruma tutaiacha lini. ..ndo maana jamii zetu zimejaa rushwa, uzembe....na mkato mkato...kwa sababu VERY FEW BELIEVE that hard work and honesty pays. Mpaka watoto wetu siku hizi tunawafundisha ujinga tuu..baaba anaiba...anajenga majengo kibao..maviwanja kibao...kisa..unajua nina watoto....To me thats wrong..simply because..hatuwafundishi watoto kutafuta maisha kwa nguvu zao.....we have become a society of greedy..we want to own everything.....maisha na future zetu havina security...ndo maana tunaiba na kumiliki hata vile tusivovihitaji...mzee una mashamba ya kufa mtu huko sijui wapi..leo umestaafu..una ghorofa kubwa masaki..hardly you can use one room wewe na mkeo..hayo mashamba huwezi hata kwenda kuyaangalia tena...Its very sad..jamii tunaijenga kwa kizazi cha leo na kesho sijui itafanikiwa vipi..... We cherish mediocrity. Simply put........ We know the price of everything. We know the value of nothing!
Its a bad culture. We ought to stop it.
Masanja.
Mkuu sana Masanja mfumo wetu umetuandaa hivyo, kuna kasoftware kadogo kanatakiwa kuwa installed kwenye mind zetu kufuta hii mentality, na nina hofu kama hii litawezekana kwa sasa maana ukweli ni kwamba mlinganyo wa maisha kati ya aliye nacho asiye nacho na mwenye kidogo ni mkubwa mno ambapo kwa mwanahisababti utakuwa una unknown tatu za kutafuta wakati dta ulizonazo zinasuit kutafuta unknown mbili...
Kuna mambo ambayo wananchi hatutaepuka lawama kwa kuyaacha yajiendee ovyo tu,mfano kutupa taka hovyo na kufanya shughuli ambazo zinablock miundombinu mathalan ambapo baadaye ikitokea dharura yoyote rescue dudes wanashindwa kumwokoa victim..
Wengi wetu tumejikuta tumezaliwa na kwamba tumesoma elementary school kwa sababu ilikuwa desturi tu ya watoto wenye umri wa kwenda shule waende, na tukajiendea tu....Tulipohitimu darasa la saba tukajikuta tupo sekondari, kwa kuwa tulichaguliwa ili tusiwe chokoraa mitaani ila baada ya kupata ka exposure kadogo ikabidi kujituma kidogo ili wadogo zetu mtaani wasituone mbumbumbu kwa kushindwa kuingia kidato cha tano...tukaenda na tukajikuta vyuoni kwa namna ile ile ya msaragambo....
Tokea siku ya kwanza ya elimu ya chuo kikuu hadi siku ya mwisho ya elimu ya shahada ya kwanza, ni tambo tu za wakufunzi na historia za nchi walizosoma na ama maisha waliyoishi wakiwa masomoni, wataende mbele zaidi kwa kukuambia kwamba wanakuandaa ili ukajiajiri mwenyewe huku wakisahau wapo chuoni kimkataba baada ya muda wao wa kufanya kazi (kuajiriwa) umepita na kwamba pamoja na nadharia yao ya kukuandaa kujitegemea ila yeye si muumini wa nadharia husika. Unamaliza unaingia mtaani ukiwa na kakiburi cha usomi, na maisha ya kisomi somi...Guess what!
Ndiyo mwanzo wa kuanza kuona serikali haijafanya hili na lile,ndo mwanzo wa kuvishwa chuki za kisiasa, ndo mwanzo wa kuanzisha vijikundi vya kugombana na serikali, ndo mwanzo wa umasikini na kuvunja sheria, ndiyo mwanzo wa kuwa mwenyeji wa mahakani. Na kwa kuwa maisha hayagandi bado uzazi utaendelea, unategemea kizazi kinachozaliwa kwenye vurumai hili kuwaje...nikisema Mtanzania wa kawaida siilaumu serikali ya bwana mkubwa, ni mfumo umetufikisha tulipo..and offcourse we enjoyed ride!
Maridadi kabisa. And thats my point.
Tumekuwa taifa la walalamishi, ujanja ujanja, mkato mkato....wizi pety pety.....yaani hatujitambui..kuanzia kwa viongozi mpaka kwetu wananchi. Lakini kikubwa zaidi..ni kipi kifanyike kuaddress hili tatizo? Mi naamini lazima tuanze kwa kubadilika kifikra. Angalia hata humu JF..kuna watu wakisikia unacomment against their belief in CCM or Chadema or whetevver party..unaonekana msaliti..huna shukrani kwa serikali sikivu! Jana nilibahatika kuangalia bunge na michango ya wabunge! Specifically nilimwangalia msomi Omar Nundu (I didnt know the dude had been a minister)..Yaani I felt very sorry for myself and my country. Yaani jamaa anaongea pumba ni hakuna mfano! Yaani nilikubali ule msome kwamba..some people appear smart until you hear them speak.
I mean wengi wetu tumeshajikatia tamaa kabisa....Lakini is it true kwamba hatuwezi kubadilika? tujadili hili.
Tujue kabisa kwa kila maamuzi tuyafanyayo...lazima kuna consequences. The only way the poor can engage in deliberative dialogue in society such as ours..is to be responsble kwenye maamuzi muhimu kama ya kuchagua viongozi na kuwawajibisha. These viongozi are damn tired na wameshiba mpaka wamejisahau. Unajua wenzetu wanasema stupidity..is doing something over and over again..expecting different results. TuNAFANYA UJINGA ULE ULE tukitegemea mambo yatabadilika.
Naamini ni muhimu hata mitaala yetu ya kishule tuibadilishe kwa namna fulani kuendana na hali halisi. Imagine mtu ana div. four ndo anachaguliwa ualimu. Juzi jamaa ananiambia..bro..nimefeli form four hebu nifanyie mpango wa upolisi au Jeshi!!! Means hizo fani ni za failures! Mkuu kama tumefikia huko na bado hatulioni huoni hatari?
Ndo maana mkuu..leo ukiendesha gari zuri au ukajenga nyumba nzuri..watu wanajua umeiba.....maana hata viongozi wetu..wametuonyesha kwamba kufanikiwa lazima uibe kodi za raia. Sad indeed.
Lakini ideas kama hizi za akina Msimbe..can change one's life positively kabisa..sema wengi wetu tumekata tamaa na I really hope tutabadilika.
Masanja
Some thing is wrong.
Bado nipo kwenye mchakato Mkuu, ndio maana nikashauri kama una affordable altenative basi unifanzie hapa ili nicheki kama kwangu iko poa zaidi!!Nimeupata ushauri wako, ni mzuri. Umefikia wapi na greenhouse yako baada ya kumtembelea huyo jamaa?