Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha greenhouse

Horseshoe Arch na Masanja naomba please tutafutane. Muhimu sana. nahisi kuna kitu tunaweza kuwasaidia Watanzania wenzetu.

Mkiwa radhi I would love to host you in my show "AMKA NA BADILIKA"
 
Last edited by a moderator:
Picha mkuu, weka picha za_kutosha.
Wapi shamba darasa?
 

Salaam Sana

Aliyoandika Mkuu huyu yana ukweli wa kiasi fulani hasa kwa sehemu za baridi. Little Search (Google) ya Green House in a Hot Climate utagundua kuwa challenges hizo are the talks of the past unless kama mtu hajaweza kujua juu ya improved Technology.

I am challenging aliyepost hii anione nimpeleke Mombasa; malindi, Kilifi in Kenya etc akashuhudie Green House in a Hot Climate kama ilivyo coast ya Tanzania. Wenzetu matatizo waliyoyapata toka miaka ya 90 yaliwafanya wabuni mambo ya ziada.

Isitoshe hapa DSM kuna watu wana green houses and can be visited.

Green House katika Hot Climate inakuwa regulated as follows:

1. Building facing wind directions for air circulation
2. Net covering 70% to allow ventilation
3. Black or Green Net to absorb the heat na
4. Sprinklers to cool the temperature

Yeyote aliye na shaka anayo nafasi ya kutembelea na kuona.
 
Mbona kama ka desa kwa JF member mamaNA?thread kamahi tayari ipo..
 

Ni lazima kuwe na maji.
Umeme hauusiki

Maelezo ya kina yametolewa juu
 
Waganga wa kienyeji bana? unaenda kwake akufanye uwe tajiri wakati yy hana kitu? y mstajirike wenywe kwanza tukaona?

mnaingiza watu chaka na biashara zenu

"Wakati Yeye Hana Kitu?" - Karibu sana.
"Msitajirike kwanza siye tukaona" - karibu sana. Njuguna unahusika hapa na utajiri wako.
"Mnaingiza watu chaka" - Tembea ujionee. Naahidi kukutembeza Green House za DSM na Kenya at my coast. Sometimes si wazo baya kuingia gharama ili asiyeamini aamini. Just contact me.
 

Sina uhakika kama Njuguna kalijibu hili.

Masoko ya nje ni makubwa sana kiasi kwamba unahitaji kuwa na reliable supplies at a fixed quantity kubwa.
Soko la nyumbani bado lipo: Graden Produces ni consumables katika maisha kila siku na kuna high na low kutegemea msimu. With Green House hakuna high na low.
 
Tatizo letu siasa imetuathiri, ingia kwenye youtube search kilimo biashara utaniambia ni uongo au ni nafasi yako kuachana na umaskini wa kujitakia

Thanks kwa kuonyesha njia. Pia Wanaalikwa kuangalia AMKA na BADILIKA PROGRAM.

NIkiandika hapa TZ kuna Ng'ombe wanatoa LITA 60 za Maziwa kwa siku sijui watabisha pia?
 
Kiukwel kuchange mind set ya wabongo kuhusu kilimo biashara Au kilimo in general t will take a century......
People are so reserved hawatak kuthink beyond.... Wao kuwa employed Ndo ndoto zao kuuubwaaa.... Ni Shida sna Kwa kweli...

Asante kwa observation yako!
 
Ahsante Mkuu. Na mie nimetoa onyo hapo juu. Naona hii fani imeanza kuingiliwa na watu wanaotaka kuwa tapeli watu bila kuwapa ukweli wote. Very sad. Watu watafanya lolote ili kupata pesa, hata kama inamaanisha kukufilisi ka akiba kako ulikoweka bank.

Mkuu hilo limejibiwa bila shaka umesoma posts iliyojibu!

Cha ajabu utashangaa kuona hata watalaam wetu uwa Kilimo toka vyuo vyetu bado wanaamini vitabu kuliko practicals. No Wonder kuna maandiko mengi kwenye makabrasha lakini utendaji kidogo.

Again, asiyeamini anaalikwa at my cost kutembezwa katika Green House katika maeneo ya joto akashuhudia.
 

Interesting . . . . Kama kawaida ni facts za kwenye vitabu ambazo hazina ubishi. Ukweli ni kuwa kuna GREEN HOUSES Mombasa na DSM and can be visited na zinafanya vema tu. Modified local experience matters!

Kwa waleo walokwisha kushuhudia na kuona my TV Program najua wanaamini yaliyoandikwa. Wakati kuna watu wanao-doubt kama kawaida kuna wengine actually they are doing it!
 
Masanja umedadavua vizuri sana!

Hapo kweye red mkuu ndipo kuna utata. Kwa vile vichwa vyetu vina ukakasi inakuwa ngumu sana kuamini katika teknolojia hizi zinazotujia ili kutukwamua kwenye umaskini. Nafikri umeona baadhi ya michango ya akina Jasho la Damu, Synthesizer (anavyojaribu kufanya synthesis ili kuonesha kuwa teknolojia hii ni majanga), hii yote ni kutokana na sisi wa-TZ kukosa ile hali ya uthubutu. Kila unapoona idea mpya kinachotangulia ni kuliwa bila kutafakari kwa mapana na marefu yake. Kizazi chetu hiki kina shida sana na taabu kubwa sana kwenye vichwa vyetu. Kufikia mabadiliko unayoyasema nafikri mpaka kwanza hiki kizazi chetu kipite, ingawa napo napata shida sana kuamini kama kweli kizazi kijacho nacho kitakuwa bora kuliko sisi kutokana na maandalizi ya elimu yetu tunayoendelea nayo leo hii!

Bado tuna safari ndefu sana kufikia mabadiliko ya kweli katika nyanja zote, ifike mahali tufanye maamuzi magumu ya overhauling the whole system bila kuangaliana usoni labda hapo ndo tutatoka. Teknolojia kama hizi zingekuwa zimeingizwa hata kwenye mitaala yetu (hili sina uhakika kama pale SUA watu wa Horticulture wanafundishwa) ingesaidia sana hata kuibua ajira kwa vijana wetu badala ya kupanga misururu na kujazana watu 10,500 kwenye nafasi 70.

Ushauri kwa bwana Sanctus na wenzake, kama inawezekana kukawa na green houses za mfano kwenye baadhi ya maeneo ili watu wakapata mahali pa kutoa tongotongo itasaidia sana kuonesha kwamba these things are doable na hivyo kupunguza mapingamizi ya akina Synthesizer na Jasho la Damu. Maana ukisoma mabandiko yao hakika unakata tamaa kabisa!!

Mwisho mkuu umenichekesha na hiyo habari ya dogo anayeomba apelekwe JW au Polisi, hii kitu hata mimi napambana nayo sasa hivi kuna mpwa alikuwa anasomea kwangu lakini sijui bahati haikuwa kwake au niseme uwezo wake ulikuwa mdogo akalamba division 5, nikamtafutia shule nyingine ili ajipange upya nikiamini kwamba labda alianguka kutokana na utoto, sasa nashangaa mtu amerudi home anataka atafutiwe Polisi au JW! Kweli??? Taifa hili linaangamia (hawa si ndo wanaelekezea na kuwafyatulia watu mabomu ya machozi na kuwamwaga matumbo?) - Shen.zy type kabisa!!
 


Job K you are right! Mafanikio yote unayoyaona na hata hayo wanayosoma kwenye vitabu, kabla hawajaandika kuna watu walipioneer wakatenda. Akina Gallileo walitaka kunyongwa waliposema dunia ni mviringo (duara) kwa sababu wakati huo dunia nzima iliaminishwa kuwa dunia ni flat.

Mbaya zaidi hata mtu anapoambiwa kuna watu wamefanya na it is working lakini bado hataki kujua. Nini cha kufanya zaidi?
 
Unaweza kuniambia emissivity na transimitivity ya cover materials mnazotumia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…