Mkuu zamani kwenye elimu zinye displine ya uchumi na masuala ya fedha walengwa wakubwa walikuwa ni matajiri wakubwa na wenye mitaji mikubwa, ila taasisi za kifedha zilipokuja kuanza kuwaamini wajasiriamali wadogo wadogo ndipo walileta micro finance ambayo inahudumia wateja wadogo wadogo walio wengi kuliko matajiri wakubwa ambao kimsingi ni wachache...and you kno what! Mjasiriamali ana displine kubwa sana ya fedha kuliko tajiri kwa kuwa hana namna nyingine ya kutoka kimaisha isipokuwa kabiashara kake ambako kamesimama kwa hisani ya mkopo!
Kuna watu wengi sana ambao hawana ujuzi wowote,na ambao nina hakika kama wakipata fursa ya kuelekezwa wazo kama hili na kama ikiwezekana wakaona kwa mfano hai kesho wangekuwa walishaji wa Taifa....
Ikiwa moja ya majukumu ya maafisa mikopo kwenye taasisi za fedha ni kumfundisha mjasiriamali namna ya kutumia vizuri mkopo ili aweze kufaidika na kurudisha mkopo inashindikanaje kuaply hii kitu kwa wakulima kupewa visual darasa na shamba darasa na baadaye somo likiisha waingia mhisani nae akatafuta masoko?