Wakati nilipokuwa nafikiria kujishughulisha na hii biashara baada ya kupata wazo hili, niliamua kufanya research kujua ukubwa wa hii biashara hapa nchini na competition yake. Nikaja kugundua kuwa soko lake ni kubwa mno. Na nilifurahi sana nilipokuja kuiona hii post ya huyu mdau humu na hiki kitabu chake kilichonisaidia sana kuanzisha biashara yangu.
Kumbe hapa nchini kuna makampuni makubwa yanayotengeneza huu mkaa wa kisasa nilikuwa sijui kabisa. Inaonekana makundi na wafanyabiashara wengi kukicha wanaingia katika hii business. Kwa mujibu wa report iliyotolewa Feb 2013 na shirika la EEP (Energy and Enviroment Partnership) kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, UKAid, serikali ya Finland na Development Bank of Southern Africa iitwayo ANALYSING BRIQUETTE MARKETS - TANZANIA, KENYA AND UGANDA unaonyesha kuwa Tanzania ina makampuni makubwa 4 yanayotambulika kimataifa yanayotengeneza mkaa huu ambayo ni East Africa Briquette company Ltd ya Tanga (inazalisha tani 2 kwa siku), ARTI Tanzania Ltd, Kilimanjaro Industrial Development Trust (KIDT) na Bagamoyo Brikwiti Company (inayozalisha tani 9.6 kwa mwezi). Biashara hii inakuwa kwa kasi ya ajabu nchini.
Nimeamua kuandika haya ili kuwaonyesha kuwa interest ya kutengeneza mkaa huu kwa watu wengi nchini imeongezeka kwa asilimia 68% kwa kipindi cha 2011 2012 pekee.