GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kama yote yaliyofundishwa mashuleni, hasa Shule ya Msingi, huenda haya yasingetokea:
1. Matumizi ya leso
Ni kawaida kwa baadhi ya watu, wanapopenga "kamasi", kutokkutumia leso. Bdala yake, hutumia mikono yao kuziba pua kidogo na kupuliza pia, " pwiii", kupuliza pembeni. Halafu maji maji yanayobakia mikononi, anayakausha kwa kufikicha mikono, kisha kazi zinaendelea kama kawaida. Hakuna kuna kunawa mikono.
Lakini enzi tukiwa shule ya Msingi, tulifundishwa kutumia leso, na kama huwezi kupata ya kununua, ujutengenezee kwa kukata kutoka katika nguo zisizotumika.
Je! Wengine hawakufundishwa hayo au wameamua kupuuzia?
2. Ulaji mlo kamili
Kwa wengine, chakula kizuri ni kama wali kuku, nyama rosti, na rosti rosti zinginezo.
Lakini tulipokuwa shule ya Msingi, tulindishwa umuhimu wa kula mlo kamili. Mboga za majani na matunda ni kati ya vyakula tulivyosisitiziwa kula kwa wingi.
Ni wangapi wanaozingatia hilo?
3. Usafi wa vyoo
Labda wengi walisomea kwenye shule zenye vyoo vya shimo kama ilivyokuwa kipindi chetu.
Kwa niliyoyaona kwenye baadhi ya vyoo vya umma, kama stendi ya mabasi, masoko, na vivuko (ferry), inaonekana kuna kitu kinapelea katika usafi na utumiaji wa vyoo.
(A). Masinki machafu, japo yanasafishwa kila siku.
(B). Tiles zilizochakaa kabla ya wakati was kuchakaa.
(C). Kuwa na mfumo wa maji usiofanya kazi.
(D). Harufu mbaya.
Hata hivyo, kwa suala la vyoo, ninasita kulaumu. Nilishaambiwa na mtu mmoja kuwa vyoo ni kati ya vitu vilivyokujaa kwa ndege.
Je! Kuhusu ulaji wa mboga za majani na matunda, pamoja na matumizi ya leso, waliopata Elimu ya shule ya Msingi wameamua kupuuzia au hawakuelewa?