Mafunzo ya Student Investor yazidi kuvutia wanafunzi wengi UDOM

Mafunzo ya Student Investor yazidi kuvutia wanafunzi wengi UDOM

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
WhatsApp Image 2026-05-24 at 10.12.17.jpeg


Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana (UDOM) na TISEZA pamoja na Shirika lisilo la Kiserikali la Save Youth Dream Foundation (SYDF), leo tarehe 23/05/2026 katika Ukumbi wa Auditorium – CIVE, wameendelea na programu ya mafunzo ya Student Investor yenye lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kiuchumi, ujasiriamali na uwekezaji.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo alikuwa ni Bw. Sudi Mtengela, Meneja wa TANTRADE – Dodoma, ambaye aliwapa vijana mwanga mpya kuhusu nafasi na fursa zinazotolewa na TANTRADE katika kutangaza bidhaa na huduma zao kupitia masoko ya kitaifa na kimataifa.

WhatsApp Image 2026-05-24 at 10.12.17 (1).jpeg


Aidha, Bw. Mtengela aliwasisitiza vijana kutumia vyema ubunifu na maarifa waliyonayo ili kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani sokoni. Pia aliwahimiza kuendelea kuipa thamani chapa ya Made in Tanzania, akieleza kuwa ni fahari ya taifa na nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia bidhaa zinazozalishwa na vijana wenyewe.

Kwa upande wake, Meneja wa Miradi kutoka Save Youth Dream Foundation, Bi. Winnie Kaaya, amesema programu hiyo itaendelea tena wiki ijayo ambapo wawezeshaji kutoka sekta mbalimbali wataendelea kutoa elimu na uzoefu kwa wanafunzi. Aidha, aliwataka vijana kutumia vizuri fursa hiyo kwa kuwa mafunzo hayo yanatolewa bure kabisa kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwafungua kiuchumi.

WhatsApp Image 2026-05-24 at 10.12.18 (2).jpeg


Mafunzo hayo yameendelea kuwa kichocheo kikubwa kwa wanafunzi wa UDOM, ambapo idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kila wiki. Hali hiyo inaonesha mwamko mkubwa wa wanafunzi katika kuchangamkia fursa za elimu ya uwekezaji, ujasiriamali na maendeleo binafsi.

WhatsApp Image 2026-05-24 at 10.12.18 (1).jpeg
 
Back
Top Bottom