SoC04 Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Mujibu wa Sheria kwa wahitimu wa kidato cha nne wasio na vigezo vya kujiunga kidato cha tano na vyuo shirikishi

Tanzania Tuitakayo competition threads

BintiRamadhani

New Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
2
Reaction score
3
UTANGULIZI
Vigezo vya watahiniwa wa kidato cha nne kuchaguliwa kujiunga kidato cha tano ama vyuo shirikishi ni ufaulu wa kuanzia daraja I hadi III hivyo ni wazi kuwa idadi kubwa ya watahiniwa waliofanya mtihani wanakosa vigezo vya kujiunga na elimu ya kidato cha tano pamoja na vyuo shirikishi. Kwa mujibu wa Takwimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia tovuti ya Wizara hiyo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | Mwaka wa masomo 2023/2024 ni asilimia 37.42 tu ya watahiniwa wote waliofanya mtihani ndiyo walipata ufaulu wa kuanzia Daraja I hadi III sambamba na mwaka wa masomo 2022/2023 ambapo asilimia 36.49 pekee ya watahiniwa wote waliofanya mtihani walipata daraja I hadi III, kwa mwaka wa masomo 2023/2024 jumla ya watahiniwa 332,170 walipata daraja IV hadi 0 sawa na asilimia 63 ya watahiniwa wote 529,596 waliofanya mtihani sambamba na mwaka wa masomo 2022/2023 ambapo jumla ya watahiniwa 264,376 walipata daraja la IV hadi 0 sawa na asilimia 64 kati ya watahiniwa wote waliofanya mtihani 456,975.

TAFITI
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu chini ya Utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi 2020/2021 kupitia tovuti National Bureau of Statistics - Home ilibainishwa kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana wenye umri wa miaka 15-35 kimeongezeka kutoka asilimia 12.1 mwaka 2014 kufikia asilimia 12.6 mwaka 2020/2021 ikiwa idadi kubwa ya vijana wenye elimu ya sekondari wana viwango vikubwa zaidi vya ukosefu ajira

ATHARI
Maelfu ya wahitimu wasio na vigezo vya kujiunga na elimu ya kidato cha tano pamoja na vyuo shirikishi wamekuwa wakiachwa mtaani bila dira au muelekeo madhubuti kwa namna watajikita katika shughuli gani za kiuchumi zitakazo waingizia kipato cha kukidhi mahitaji yao binafsi hali inayopelekea kukithiri kwa Ukosefu wa Ajira, Utegemezi, Umasikini, Uraibu wa pombe, Uraibu wa madawa ya kulevya, Uasherati, Kuibuka kwa makundi ya wizi na Kudhorota kwa ugunduzi na ubunifu nchini

PENDEKEZO
Napendekeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ishirikiane na wadau mbalimbali wa Elimu na Maendeleo kuanda na kuratibu programu mahsusi ya MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA MUJIBU WA SHERIA BURE ili kuwawezesha wahitimu wote wa kidato cha nne wasio na vigezo vya kujiunga na elimu ya kidato cha tano na vyuo shirikishi kujiunga na vyuo vya ufundi stadi vitakavyowapatia ujuzi katika fani mbalimbali zenye tija kwenye ukuaji wa Uchumi kama vile Ufundi wa teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT),Ushonaji, Utengenezaji wa bidhaa za ngozi, Utengenezaji vipodozi, Ufundi viyoyozi, Ufundi magari, Uchakataji vyakula, Ufundi mwashi na Ufundi kompyuta kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi nchini ( VETA) na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Tanzania (SIDO) chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.Tumeona Serikali imefanikiwa kuandaa programu inayolingana na hii niliyoipendekeza chini ya Wizara ya kilimo nchini inayofahamika kama Building a Better Tomorrow. Wahitimu wengi wa kidato cha nne wana umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24 hivyo ni wazi kuwa ni watu wenye mchango muhimu kwenye Nguvu kazi ya taifa letu. Kuliacha kundi hili kubwa la vijana mtaani kwa kuwa hawana vigezo vya kujiunga na elimu ya kidato cha tano pamoja na vyuo shirikishi ni hatari kwa Maendeleo ya nchi na usalama wa raia na mali zao.

MATOKEO
Kupunguza wimbi la vijana wasio na Ajira; Tukiwawezesha vijana kupata Mafunzo ya Ufundi stadi kutawajengea ujuzi katika fani mbalimbali utakaowasaidia kupata ajira katika sekta tofauti tofauti nchini aidha kuajiriwa kwenye kampuni binafsi ama kujiajiri iwapo watapatiwa ruzuku zitakazotolewa zitazotumika kama mtaji wa kununua rasilimali hitajika kama vile vifaa vya uzalishaji na Kulipia kodi ya eneo la kiwanda

Kuongezeka kwa vijana wenye ujuzi kutachochea ugunduzi pamoja na ubunifu; Iwapo wahitimu wa kidato cha nne wasio na vigezo vya kujiunga na elimu ya kidato cha tano pamoja na vyuo shirikishi watapatiwa Mafunzo ya Ufundi stadi itaongeza idadi ya vijana wenye ujuzi nchini ambao ni muhimu kuchochea ubunifu na ugunduzi utakaoendena na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani kote kukuza uchumi wa Taifa vilevile tunaweza kupeleka mamia ya nguvu kazi hitajika kwenye nchi zenye upungufu wa wajuzi wa fani tofauti tofauti baada ya kuzazalisha wajuzi wanaotosheleza uzalishaji na ubunifu wa bidhaa pamoja na huduma nyinginezo ndani ya nchi.

Ukuaji viwanda vidogovidogo nchini ; Baada ya vijana kupatiwa Mafunzo ya Ufundi stadi kwa Mujibu wa sheria serikali inapaswa kuishirikiana na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Tanzania (SIDO) chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuwawezesha vijana hao kuwekeza kwenye uanzishwaji na wa viwanda vidogovidogo kwa kuwapatia ruzuku zitakazotumika kununua vifaa kama vile mashine, kompyuta na cherehani
Kupunguza Utegemezi na Umasikini; Kundi kubwa la vijana wasio na vigezo vya kujiunga na elimu ya kidato cha tano pamoja na vyuo shirikishi wamekuwa mzigo kwa familia zao kwa kukosa muelekeo wa shughuli za kiuchumi hivyo kuongeza wimbi la umaskini nchini. Iwapo watawezeshwa kupata Mafunzo ya Ufundi stadi itapunguza kwa kiasi kikubwa hali ya utegemezi iliyopo kwa kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kujiajiri au kuajiriwa moja kwa moja watajiingizia kipato cha kutimiza mahitaji yao ya kila siku wao wenyewe

Kupunguza Vitendo vya Uhalifu ; Tumeshuhudia kwa namna gani kundi hili la vijana likijihusisha katika matendo mbalimbali ya kihalifu kama vile wizi, uporaji na uesherati ili kutimiza mahitaji yao ya msingi sambamba na uraibu wa pombe pamoja na madawa ya kulevya ili kuepuka uhalisia wa hali za maisha mtaani hivyo kuwawezesha vijana hawa kupata Mafunzo ya Ufundi stadi kutawezesha kujikita kwenye shughuli mbadala za kiuchumi hivyo kwa namna moja au nyingine tutafanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa matendo ya kihalifu na Kuboresha Usalama wa raia na mali zao.

HITIMISHO
Hali za kiuchumi za watanzania walio wengi ni lazima zizingatiwe hivyo ni vyema Serikali ikaratibu shughuli zote za Mafunzo ya ufundi stadi kwa mujibu wa sheria pamoja na kutoa ruzuku kwa wanufaika wa miradi huo, Mwisho wanufaika wapangiwe vyuo vya ufundi stadi vilivyo karibu na makazi yao. Programu hii italeta mabadiliko chanya kwenye sekta ya Elimu, Sayansi, Teknolojia, Viwanda, Ajira na Biashara nchini ndani ya miaka mitano au zaidi.
 
Upvote 0

Wazo zuri Sana ila ili tuweze kuwa saidia hao vijana aweze fikia hat a njema ktk ujuzi, lazima kwanza tu kubali kuwa elimu ya ufundi stadi inanyanyapaliwa na jamii kubwa hasa zilizo soma, hivyo hamna budi kwanza serikali kudeal na unyanyapaa huo ili mtoto anapopelekwa huko aone yuko Sawa na yalienda form five au chuo, maana bila hivyo huko veta tutazidi kujaza vilaza tu na mwisho tusione ubunifu wala nini maana watoto watakuwa wanasoma kwa kusukumwa... Hawana furaha yakupa pale!
 
Asante sana umesema jambo la maana mno kuzingatiwa,Shukrani.
 
Back
Top Bottom