Mafunzo ya Usalama wa Wanahabari na Watu wenye Ushawishi
Waandishi wa Habari wa kike na Watu Wenye Ushawishi wameshiriki warsha ya Siku moja iliyohusu kujengewa Uelewa wa Usalama wao katika masuala ya Mtandao, ilifanyika Mei 7, 2024 ikiandaliwa na Taasisi zisizo za Kiserikali, JamiiForums kwa kushirikiana na CIPESA.
Warsha hiyo ililenga kuangalia usumbufu na manyanyaso wanayoyapata, athari na mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za aina hiyo, pia walipewa mafunzo ya masuala ya Ulinzi wa Kidigitali ikiwemo ulinzi wa Taarifa Binafsi.