Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Takribani watu 14 wamefariki na wengine 11 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini Nepal.
Mamlaka zimeonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mafuriko ya ghafla katika wilaya 49 kati ya wilaya 77 za nchi hiyo, huku mito na vijito ikiendelea kujaa. Chitwan ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi.
Mvua hizo pia zimesababisha kukatika kwa umeme na kuvuruga huduma za mawasiliano katika baadhi ya wilaya, huku vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwatafuta watu waliopotea na kuwasaidia wananchi walioathirika na mafuriko.
Soma Pia: Takribani Watu 95 Wafariki, Mamia Wapotea baada ya mafuriko na maporomoko ya matope kutokea katika eneo la mpaka wa Nepal na Tibet
Maafa hayo yametokea wiki kadhaa baada ya mafuriko makubwa nchini Nepal kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,450, huku maelfu ya wengine wakiachwa bila makazi na wengine kutoweka.