Mafuriko Rufiji | Wananchi wamlilia Rais Magufuli

Mafuriko Rufiji | Wananchi wamlilia Rais Magufuli

March 20, 2020
Kidatu, Morogoro
Tanzania

Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano Mh. Engineer Isack Kamwelwe afika Kidatu kukagua daraja linalovuka mto Ruaha Mkuu mkoani Morogoro lililotishiwa kuharibiwa na maji mengi yenye kasi kubwa.

 
March 20, 2020
Iringa

Kufuatia mvua kubwa zinazoendelea changamoto kubwa ktk miundo mbinu Maeneo ya Pawaga, Kipera, Nyangoro, Ipogoro , Nzii, Msembe na Ruaha mkoani Iringa

 
March 2020
Iringa

Ziara ya Mkuu wa mkoa Iringa Mh. Ally Hapi na msafara wake kutembelea wananchi, ilibidi upite ktk barabara zilizofurika maji kutokana na mvua nyingi zinazonyesha Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania



Source : Habari Kwanza
 
March 22, 2020
Rufiji, Pwani
Tanzania

Barabara iendayo mradi wa umeme Stiegler's Gorge
Mbunge wa Rufiji mkoani Pwani Mh. Mohamed Mchengerwa akielezea hali ya barabara jimboni kwake kama ilivyo katika video inayotoka Kibiti kwena Ikwiriri, Mkongo, Ngororo, Mloka mpaka katika mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere HydroPower Project ilivyo na kukwamisha uwezekano wa ndoto ya nchi mradi kukamilika ktk muda uliopangwa:



Source : Millard ayo
 
March 18, 2020

LIVE: MAFURIKO RUFIJI | WANANCHI WANAVYOMLILIA JPM

Wananchi wa Rufiji mkoani Pwani waamua kujitokeza baada ya kuona hakuna hatua za dhati za viongozi wa maeneo yao kuifahamisha serikali kuu kuchukua majukumu kuwasaidia.




Serikali ya CCM Mpya vilio hivi vya wana Rufiji visifunikwe ili mbali ya serikali kuu, hata waTanzania wenye moyo wa kujitolea wafahamishwe hali hii tete ili kuweza kuwanusuru na kuwahifadhi waTanzania wenzao.

Source: Jamvi online TV

Subiri watukanwe
 
Tokea Awamu ya tano ijisimeke madarakani ilikaribishwa na matetemeko ya ardhi huko kanda ya ziwa
Mikosi baada ya nuksi upigwaji risasi na upotevu wa wanasiasa umekuwa kitu cha kawaida

Huku viongozi mbalimbali wakikanusha kila kitu

Karma karma karma karma karma karma inanyong'onyea
Fikiria nchi ikipewa ma dj na malesbians si tutaangamizwa na gharika Kama la nuhu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonde la nyerere likianza kuzalisha umeme hii kero ya mafuriko itaisha! Haya ndo manufaa ya mradi huu wa umeme japo vibaraka wa mabeberu akina zitto na wenzake wanaupinga!
Siyo kwa mvua zinazonyesha msimu huu,,Hao watu wanaitaji msaada na sio habari za mradi wa umeme, kwa iyo waendelee kutabika wakisubiria mradi ukamilike ndio wawe salama.
 
March 23, 2020
Msolwa Stesheni
Kilombero, Morogoro

Kamati ya maafa yafika kuona athari za mafuriko Msolwa Stesheni, Kilombero

Maafa hayo ni kutokana na mvua zinazonyesha nchini na mto Ruaha, Mto Ruaha Mkuu na Kilombero kuzidi kujaa maji kupita kiasi.

 
March 18, 2020

LIVE: MAFURIKO RUFIJI | WANANCHI WANAVYOMLILIA JPM

Wananchi wa Rufiji mkoani Pwani waamua kujitokeza baada ya kuona hakuna hatua za dhati za viongozi wa maeneo yao kuifahamisha serikali kuu kuchukua majukumu kuwasaidia.




Serikali ya CCM Mpya vilio hivi vya wana Rufiji visifunikwe ili mbali ya serikali kuu, hata waTanzania wenye moyo wa kujitolea wafahamishwe hali hii tete ili kuweza kuwanusuru na kuwahifadhi waTanzania wenzao.

Source: Jamvi online TV


Siju imekuwaje serikali hii imeamua kuwatelekeza hawa watani zangu. Angalao marehemu Mbaraka Mwishehe angekuwa hai angewatungia wimbo wa kuwapa pole kwa mafuriko watani zake wa Rufiji na Ulanga kama alivyofanya miaka ya 70 yalipotokea mafuriko kama haya.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi!
 
Back
Top Bottom