Mafuriko:Vodacom waanza kampeni ya simu; kuchangia Vod. Foundation

Mafuriko:Vodacom waanza kampeni ya simu; kuchangia Vod. Foundation

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kwa wale wanaokumbuka tulianza sisi (watu wa TPN, JF, n.k) kuanzisha harambee ya kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu kufuatia mafuriko ya Kilosa na sehemu nyingine nchini tukiamini kuwa serikali peke yake haiwezi kubeba jukumu la kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika. Ikumbukwe tulibuni hili la kusaidia Chama chetu cha Msalaba Mwekundu kabla ya tetemeko la Haiti na kabla US wao hawajaamua kutumia mtindo huu huu kusaidia chama chao cha msalaba mwekundu.

Ndipo tukaanza kutumia mtandao wa simu kwa kuwahamasisha watu kujitokeza kuchangia shilingi 150 kwa siku (baada ya kulipa shs 250 kujiandikisha) kwa kutuma neno "TPN" kwenda namba "15522". Hadi hivi sasa karibu watu 1800 wamejitokeza kujiandikisha huku walio nje ya nchi wameweza kuchangia kwa namna wanayoweza japo ni wachache mno (hadi sasa hawajazidi watu 10!!!)

Leo hii Vodacom ambao pia tunatumia mtandao wao nao wameanzisha kampeni ya kuchangia Vodacom Foundation kwa mtindo huu huu ili waweze kusaidia katika maafa. Kampeni yao inazinduliwa leo.

red%2Balert.bmp



Pamoja na juhudi hizi za Vodacom.. ninawasihi Watanzania tuendelee kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania kwa wingi zaidi kwani hawa ndio mstari wetu wa kwanza wa kinga linapotokea janga lolote lile. Tuendelee kujiandikisha kwa kutuma hilo neno la "TPN" kwenda "15522" ili hatimaye mwisho wa wiki ijayo tena tuweze kuwasilisha misaada yetu moja kwa moja kwa Red Cross.

NB: Kama tulivyosema utakatwa sh 250 kujiandikisha mara moja, na kwa siku 30 utakatwa shilingi 150 kwa siku kwa jumla ya Tsh 4500 kwa mwezi.

Pamoja tunaweza!!
 
Mwanakijiji;

Binafsi natamani kama kampeni hizi zote zingekuwa ni initiative moja kuonyesha umoja wa kitaifa hasa katika majanga kama vile Marekani wanavyofanya.

Kuna usemi wa kiswahili unaosema " Mnajenga nyumba moja, fito mnagombea za nini?"

Hata hivyo kwa kuwa nia yetu wote ni moja, huenda haijalishi ni nani kaanza na ni nani kafuata. Kikubwa ni kuwasaidia wahanga wa mafuriko.

Upande wa initiative za TPN; JF na wadau wake, tumeshakabidhi misaada awamu ya kwanza Red Cross na awamu ya pili tutakabidhi this week. Tunatumaini kuwa wadau mbali mbali bado wataendelea kuitikia wito wa kuwachangia ndugu zetu.
 
Sanctus.. you are very diplomatic; I'm not. Vodacom Foundation wanachangia Vodacom Foundation! Sijui tangu lini Vodacom Foundation imewahi kuomba msaada kutoka kwa public. Kama wangetaka kusaidia Red Cross ya Tanzania wangefanya hivyo kwa kushirikiana na watu wengine.

Kama juhudi zetu zilikuwa na shortfall ya aina fulani au zinahitaji kuboreshwa wangeweza kukaa chini na kusema wapi to improve.

Bado nataka kusaidia Red Cross ya Tanzania kwa sababu ninaamini siku janga litakapofika hakuna mtu atakayeuliza wako wapi Vodacom Foundation.. watu watalia na kuuliza where is the "Red Cross" not "Red Alert".. ( I hate playing with words!).

I hope when they initiate the company watasema kuwa wana lengo la Kusaidia Chama cha Msalaba Mwekundu na asilimia 100 ya fedha yote inayokusanywa itapelekwa kwenye Red Cross au kugawanywa kwenye other Relief Charities! Hii ya kujichangia wenyewe.. inatisha.
 
Nimetuma neno MAAFA kwenda 15599 nikajibiwa na SMS kutoka VODACOM yenye maneno yafuatayo:

Asante kwa mchango wako. Tuma MAAFA kwenda 15599 kuchangia Tsh 250 tena. Thanks for donating to Vodafone Red Alert. SMS REDALERT to 15599 to donate Tsh 250 again.
 
Nimetuma neno MAAFA kwenda 15599 nikajibiwa na SMS kutoka VODACOM yenye maneno yafuatayo:

Asante kwa mchango wako. Tuma MAAFA kwenda 15599 kuchangia Tsh 250 tena. Thanks for donating to Vodafone Red Alert. SMS REDALERT to 15599 to donate Tsh 250 again.

Mi nawaambieni nyie akina Mtsimbe,..kama mlikuwa hamjui VODACOM wameamua kuiba reputation yenu baada ya kuona kwamba mmewapiga bao kwa kurespond mapema kwenye ishu hii ya mafuriko...

Na mbaya zaidi mlitumia mtandao wao, kwahiyo wamekaa na kuamua kuweka mambo upside-down, inside-out!

Halafu, hata kama watapata michango, basi watapiga PASU-PASU, kwa maana kwamba kitakachopelekwa sehemu -lengwa ni nusu ya kitakachopatikana.

VODA ni wezi mbona? kwanini mlipitishia kwao?
 
this is whats up!! wametuma message za promotion naamini kwa subscribers wao.. na kama nusu tu wakiamua kujiandikisha..
 
PakaJimmy;

TPN na Wadau wake haina mkataba na Vodacom. Ina mkataba na Push Mobile (http://push.co.tz/). Push Mobile wametuunganisha katika mitandao ya Zain; Tigo na Vodacom.

Yeyote aliyeoko katika mitandao hiyo anaweza akachangia katika harambee yetu kwa pesa au vitu. Michango yote inapelekwa Red Cross in publi na update inatolewa. Vitabu vyote viko wazi kwa uhakiki wa mtu yeyote kujenga uwazi, ukweli na uaminifu.
 
Mimi nawapa changamoto Vodacom Foundation kuwa michango yao yote wanayokusanya kusaidia wahanga waipeleke Red Cross ya Tanzania!! as a matter of fact I dare them to!
 
this is whats up!! wametuma message za promotion naamini kwa subscribers wao.. na kama nusu tu wakiamua kujiandikisha..

Mwanakijiji sina uhakika kama wametuma SMS kwa subscribers wao. Niliarifiwa na Mmari wakati anaongeza salio la simu yake inayotumia mtandao wa Vodacom, aliona SMS ikimjulisha juu ya Promotion ya Maafa. Nilijaribu kutuma SMS ndiyo nikapata response SMS hiyo hapo juu.
 
Mi nawaambieni nyie akina Mtsimbe,..kama mlikuwa hamjui VODACOM wameamua kuiba reputation yenu baada ya kuona kwamba mmewapiga bao kwa kurespond mapema kwenye ishu hii ya mafuriko...

Na mbaya zaidi mlitumia mtandao wao, kwahiyo wamekaa na kuamua kuweka mambo upside-down, inside-out!

Halafu, hata kama watapata michango, basi watapiga PASU-PASU, kwa maana kwamba kitakachopelekwa sehemu -lengwa ni nusu ya kitakachopatikana.

VODA ni wezi mbona? kwanini mlipitishia kwao?

Si jambo la kutisha sana kwa mtu yeyote yule kuchangia matatizo ya nchini lakini ingekuwa ni jambo la busara sana kwa Vodacom Foundation kuja na kampeni ambayo hela inakwenda moja kwa moja Red Cross badala ya Red Alert. Hizi marketing terminologies kama watu wasipokuwa wahangalifu watakuwa wanaliwa sana.

this is whats up!! wametuma message za promotion naamini kwa subscribers wao.. na kama nusu tu wakiamua kujiandikisha..

Kila mtu anajua ni dili sana kuingia katika promosheni za namna hii. Ni marketing idea tu ambayo watu au makampuni utumia kama njia ya kuingiza kipato mbali na kupitia kwa wateja wao ambao ununua kadi za simu ama kuweka kwa mwezi.
 
Mi nawaambieni nyie akina Mtsimbe,..kama mlikuwa hamjui VODACOM wameamua kuiba reputation yenu baada ya kuona kwamba mmewapiga bao kwa kurespond mapema kwenye ishu hii ya mafuriko...

Pakajimmy;

Kama kuna moja kati yetu ambaye alikuwa anafanya kampeni hii kwa ajili ya reputation, basi inawezekana kuwa alikuwa na maono tofauti.

Sisi kama viongozi tunalo jukumu ya kusimamia yale yote ambayo yana manufaa kwa walengwa na taifa kwa ujumla bila kuangalia reputation. Kwa hili la maafa sisi tunafanya sehemu yetu.

Kama kuna wanaofanya kwa ajili ya reputation au malengo fulani binafsi . . basi binafsi nitakuwa siafikiani nao.
 
Wamefanya hivyo baada ya kuona michango yako na malengo na mengi uliyofanya kwa ajili ya Tanzania mzee wangu lakini pia tazama hata huko kama kweli wanaweza kusimamia vizuri pesa hizi MM babu
 
Pakajimmy;

Kama kuna moja kati yetu ambaye alikuwa anafanya kampeni hii kwa ajili ya reputation, basi inawezekana kuwa alikuwa na maono tofauti.

Sisi kama viongozi tunalo jukumu ya kusimamia yale yote ambayo yana manufaa kwa walengwa na taifa kwa ujumla bila kuangalia reputation. Kwa hili la maafa sisi tunafanya sehemu yetu.

Kama kuna wanaofanya kwa ajili ya reputation au malengo fulani binafsi . . basi binafsi nitakuwa siafikiani nao.
By the way,
Dont call it reputation on the forrum here, but our hearts do call it in that way!
Aksante Mkuu!
 
Vodacom yazindua kampeni ya kuchangia waathirika wa maafa leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare(katikati) akizungumza na Waandishi wa habari leo asubuhi kabla ya uzinduzi wa kampeni ijulikanayo kama Vodafone Red Alert,inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.Kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja wa Vodacom kuwachangia Watanzania waliopatwa na maafa kwa kutuma neno MAAFA kwenda namba 15599,kila ujumbe mmoja utatozwa shilingi 250.alieyakaa kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali mstaafu Bakari Shabani na kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shabani(katikati)akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa wa kampeni ijulikanayo kama Vodafone Red Alert,inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo inalenga kuwahamasisha wateja wa Vodacom kuwachangia Watanzania wenzao waliopatwa na maafa kwa kutuma neno MAAFA kwenda namba 15599,kila ujumbe mmoja utatozwa shilingi 250 pamoja na VAT (kushoto)ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Dietlof Mare.

.Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba(kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ijulikanayo kama Vodafone Red Alert,inayoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania.Kampeni hiyo ina lenga kuwahamasisha wateja wa Vodacom kuwachangia Watanzania waliopatwa na maafa kwa kutuma neno MAAFA kwenda namba 15599,kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaban na Mkurugenzi Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraim Mafuru.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akibadilishana mawazo na Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shabani kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali mstaafu Bakari Shaban, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wanaohusika waliojitolea kusaidia jamii wakati wa maafa, Voda Heroes wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya kusaidia wahanga wa maafa mbalimbali hapa nchini.

Vodacom Tanzania leo imezindua rasmi kampeni ya kusaidia waliofikwa na maafa, na kupitia kampeni hiyo, wateja wa Vodacom sasa wanaweza kutoa michango yao kwa wahanga wa majanga hayo.

Akizindua kampeni hiyo asubuhi hii, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw Dietlof Mare alisema kampeni hiyo ni muhimu katika kuyarejesha katika hali ya kawaida maisha ya Watanzania walioathiriwa na maafa katika sehemu mbalimbali za nchi.

Aliwataka wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika kampeni hiyo ili waweze kuwasaidia waathirika wa majanga hayo.

Ili kuwachangia wahanga, wateja wa Vodacom wanapaswa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA au REDALERT kwenda namba 15599, na ujumbe huo wa mchango unagharimu Sh. 250 pamoja na VAT, mteja anaweza kutuma mara nyingi kadri awezavyo.

Kampeni itakuwa ni ya wiki moja kuanzia tarehe 24 Januari mpaka tarehe 1 Februari mwaka huu.

Alisisitiza kuwa bila ya ushirikiano wa wateja wapatao milioni saba wa Vodacom Tanzania zoezi hili halitafanikiwa na hivyo kuwaomba wateja wachangie kwa wingi mfuko huo kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi.

Bw Mare alivishukuru vyombo vya habari nchini kwa kutoa ushirikiano wao kwenye kampeni hii na kuomba ushirikiano wa namna hiyo udumu kwa manufaa ya Watanzania.

Nae Mkurugenzi wa Kitengo cha Mfuko wa Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shabani, alipongeza Vodacom kwa kuanzisha kampeni hii na kuwataka watanzania kwa ujumla kuchangia mfuko huo.

Alisema kwamba siku zote panapotokea majanga mtu wa kwanza anayepaswa kujisaidia ni mwathirika mwenyewe kabla ya kungoja msaada kutoka nje.

Alitoa wito kwa makampuni mbalimbali hata kama siyo ya simu kuwasawaidia waathirika wa majanga hapa nchini.

“Nawapongeza Vodacom Tanzania kwa kuanzisha mpango huu wa kusaidia Watanzania wenzao, nayaomba makampuni mengine nayo yajitokeze,”

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom alisema mpango huo wa Vodafone Red Alert uko katika nchi 27 ambazo kampuni ya Vidafone ipo.

“Hivyo wajibu wetu ni kuwawezesha kwa teknolojia Watanzania wenyewe waweze kuchangia,” alisema.

Alisema kila mara yatakapotokea majanga, basi Vodafone Red Alert itakuwa ya kwanza kuanzisha kampeni ya Watanzania kuchangi,”


 
Yatatimia tu, hata yale yaliyonenwa na wanadamu! Time will tell
 
Hivi Vodacom Foundation ni mali ya akina nani? Tukiwajua wamiliki wa Vodacom tunaweza kupata picha ya kwa nini wameamua kuanzisha kampeni hii badala ya kuungana na kampeni ya akina Mtsimbe.

Mkuu Mtsimbe hongera kwa maelezo mazuri uliyokuwa unayatoa kwenye majadiliano katika kipindi cha kipimajoto cha ITV siku ya Ijumaa. Kilichonistua ni figure ya wale waliokwishaitikia wito wa kuchangia. Ulisema ni 1,600 tu na huende sasa imefikia 2,000. Tanzania ina watu wazima takriban milioni 30 ama zaidi. Labda tusema asilimia 20 ya watu wazima hao wanao uwezo wa kuchangia kiasi cha Sh. 500 kila mmoja. Kwa nini wengi wameshindwa kuitikia wito huu muhimu, ndilo suala la kujiuliza na kuangalia namna ya kufanyia kazi majibu tutakayopata.
 
Hivi Vodacom Foundation ni mali ya akina nani? Tukiwajua wamiliki wa Vodacom tunaweza kupata picha ya kwa nini wameamua kuanzisha kampeni hii badala ya kuungana na kampeni ya akina Mtsimbe.

Mzalendo Mtsimbe hongera kwa maelezo mazuri uliyokuwa unayatoa kwenye majadiliano katika kipindi cha kipimajoto cha ITV siku ya Ijumaa. Kilichonistua ni figure ya wale waliokwishaitikia wito wa kuchangia. Ulisema ni 1,600 tu na huende sasa imefikia 2,000. Tanzania ina watu wazima takriban milioni 30 ama zaidi. Labda tusema asilimia 20 ya watu wazima hao wanao uwezo wa kuchangia kiasi cha Sh. 500 kila mmoja. Kwa nini wengi wameshindwa kuitikia wito huu muhimu, ndilo suala la kujiuliza na kuangalia namna ya kufanyia kazi majibu tutakayopata.

Source: http://en.wikipedia.org/wiki/Vodacom_Tanzania#Vodacom_Tanzania_Partnership

Vodacom Tanzania Partnership

It has been claimed that Vodacom Group has a habit of choosing politicians and their friends as business partners to extends its operations on the continent[6]. It was reported by The Mail & Guardian that Mozambican President Armando Guebuza had become a shareholder in Vodacom Mozambique.

Vodacom Tanzania was licensed in Tanzania with its local partners Planetel Communications holding 36% and Caspian Construction holding 16%. Later Planetel decreased its stake to 16%, while Caspian's increased to 19%[6].
A representative of Caspian on the Vodacom Tanzania board is businessman-politician Rostam Aziz, a close supporter of President Jakaya Kikwete. At the time Vodacom was licensed in Tanzania, neither man was quite as powerful as now.Kikwete was Foreign Minister and Aziz had yet to occupy any formal position in Tanzanian politics.

While spreading its political bets, the CCM's and the former Speaker of ParliamentPius Msekwa was granted Vodacom Tanzania's non-executive chair between 2003 and 2005. When Vodacom Tanzania hosted a "VIP gala night" to bid farewell to outgoing president Mkapa in December 2005, Msekwa attended, presumably in both capacities.

Source: http://www.vodacom.co.tz/docs/docredir.asp?docid=3393

About Vodacom Foundation


VODACOM FOUNDATION

Vodacom is Tanzania's leading cellular network and with our success comes the responsibility of giving back to our society in a meaningful and sustainable fashion.

The Vodacom Foundation was created in July, 2006, for this purpose. the Foundation focuses Vodacom's corporate social investment efforts with the aim of improving the lives of Tanzanians through poverty alleviation and promoting economic development.

The Foundation looks at 4 key areas, namely, Education, Health, Economic empowerment and social welfare which are in line with Tanzania's National development prioroties.

To date the Foundation has carried out over 70 projects in 17 regions of the entire country. these projectshave reached and directly impacted the lives of over thousands of Tanzanian's from an array of backgrounds.


MISSION

The Vodacoom oundation's key mission is to enrich the lives of communities in Tanzania through caring partnerships.The foundation supports Tanzanians especially the disadvantaged and marginalized groups with the aim of helping them to build better lives for themselves through poverty alleviation schemes and programs.

OBJECTIVES
  1. To improve access to education for children especially those in the poorest communities.
  2. To contribute to health challenges faced in Tanzania by providing relevant infrustructure where we can.
  3. To facilitate economic empowerment of Tanzanians.


Mkuu mpaka asubuhi hii wanaochangia sasa wamefikia 1805. Kwa nini wengi hawachangii kwa kweli ni swali gumu. Ingawa wengi kwa nyakati tofauti wana maoni kuwa hili ni Jukumu la Serikali, lakini pia kuna ambao hawana imani kuwa michango wanayotoa itawafikia walengwa kwa kudhania kuwa itaishia katika mikono ya wajanja wachache.
 
Makampuni haya makubwa (corporate) hapa nchini kiwango cha uzalendo kiko chini kulinganisha na profit maximazation na govt lobbying to get more relief in their operations.

TPN tuna jukumu la kuwaelimisha umma umuhimu wa uzalendo katika maeneo mbali mbali kama vile kiuchumi, kisiasa na kijamiiii...
 
Na mkifanya mchezo watawapiga bao la kisigino.Something has to be done to prevent hili bao.
 
Source: http://en.wikipedia.org/wiki/Vodacom_Tanzania#Vodacom_Tanzania_Partnership



Source: http://www.vodacom.co.tz/docs/docredir.asp?docid=3393




Mkuu mpaka asubuhi hii wanaochangia sasa wamefikia 1805. Kwa nini wengi hawachangii kwa kweli ni swali gumu. Ingawa wengi kwa nyakati tofauti wana maoni kuwa hili ni Jukumu la Serikali, lakini pia kuna ambao hawana imani kuwa michango wanayotoa itawafikia walengwa kwa kudhania kuwa itaishia katika mikono ya wajanja wachache.

Asante Mkuu.

Nakubaliana nawe kwamba baadhi ya wananchi hawachangii kwa sababu hawamini kwamba michango yao itawafikia walengwa. Pia, siku hizi umeingia 'ugonjwa' wa wananchi kudai Serikali ifanye kila kitu, hata yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wa wananchi wenyewe kuyafanya kwa kujitolea kama ilivyokuwa huko nyuma. Twaamini TPN mtaweza kuja na mikakati ya kufufua moyo wa kujitolea miongoni mwa wananchi.
 
Back
Top Bottom