Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kwa wale wanaokumbuka tulianza sisi (watu wa TPN, JF, n.k) kuanzisha harambee ya kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu kufuatia mafuriko ya Kilosa na sehemu nyingine nchini tukiamini kuwa serikali peke yake haiwezi kubeba jukumu la kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika. Ikumbukwe tulibuni hili la kusaidia Chama chetu cha Msalaba Mwekundu kabla ya tetemeko la Haiti na kabla US wao hawajaamua kutumia mtindo huu huu kusaidia chama chao cha msalaba mwekundu.
Ndipo tukaanza kutumia mtandao wa simu kwa kuwahamasisha watu kujitokeza kuchangia shilingi 150 kwa siku (baada ya kulipa shs 250 kujiandikisha) kwa kutuma neno "TPN" kwenda namba "15522". Hadi hivi sasa karibu watu 1800 wamejitokeza kujiandikisha huku walio nje ya nchi wameweza kuchangia kwa namna wanayoweza japo ni wachache mno (hadi sasa hawajazidi watu 10!!!)
Leo hii Vodacom ambao pia tunatumia mtandao wao nao wameanzisha kampeni ya kuchangia Vodacom Foundation kwa mtindo huu huu ili waweze kusaidia katika maafa. Kampeni yao inazinduliwa leo.
Pamoja na juhudi hizi za Vodacom.. ninawasihi Watanzania tuendelee kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania kwa wingi zaidi kwani hawa ndio mstari wetu wa kwanza wa kinga linapotokea janga lolote lile. Tuendelee kujiandikisha kwa kutuma hilo neno la "TPN" kwenda "15522" ili hatimaye mwisho wa wiki ijayo tena tuweze kuwasilisha misaada yetu moja kwa moja kwa Red Cross.
NB: Kama tulivyosema utakatwa sh 250 kujiandikisha mara moja, na kwa siku 30 utakatwa shilingi 150 kwa siku kwa jumla ya Tsh 4500 kwa mwezi.
Pamoja tunaweza!!