Mafuriko ya dunia nzima kwa mujibu wa biblia

Mafuriko ya dunia nzima kwa mujibu wa biblia

Kama kulikuwa na mafuriko dunia nzima basi samaki chuchungi wa bahari ya nchunvi angepatikana ziwa victoria.
 
Biblia imesema ukosefu wa imani na mamalalamiko kibao ndio sabu ya Mungu kuwaadhibu wana israel adhabu ya "kuzurula jangwani miaka 40"
Jamaa walimlalamikia MUNGU Ati Bora wangebaki Misri... kwamba hata Mana imewakinaisha .... MUNGU akawatandika na nyoka wafilie huko...
 
Changamoto ni chanzo ya maji ya ziada na yalienda wapi baada ya mafuriko.
Kabla hatujafuatilia maji yaliyopo chini ya ardhi, embu fuatilia maji yaliyoganda kama barafu iwapo yatayeyuka kiasi gani cha ardhi duniani kitabaki kikavu.
 
Hizo ni fiction za uongo na kweli ngoja nikupe kisa...

Kanisa Katoliki la Roma lilimpa adhabu Galileo Galilei, na sababu kuu ilikuwa ni mafundisho yake kuhusu mfumo wa jua.. heliocentric theory...

Galileo alithibitisha ushahidi wa kisayansi kwamba sayari, pamoja na dunia, huzunguka jua. Hii ilikuwa kinyume na imani ya wakati huo...

Kanisa Katoliki lilikuwa na ushawishi mkubwa katika masuala ya kisayansi, kifalsafa, na kijamii. Mafundisho ya Biblia yalionekana kuunga mkono wazo kwamba dunia ndiyo inazungukwa na jua... soma mhibiri 1:5 na Zaburi 104:5 ...

1633 Galileo alishutumiwa kwa kushikilia na kufundisha imani potofu kwamba jua halisogei na dunia ndiyo inayozunguka. Alilazimishwa kujiondoa kwenye imani hiyo hadharani, na inasemekana alijitetea kwa sauti ya chini akisema 'na bado inazunguka'....

Galileo alihukumiwa kifungo cha maisha cha nyumbani ,house arrest, na vitabu vyake vilipigwa marufuku. Aliishi chini ya uangalizi hadi kifo chake mwaka 1642.



Miaka mingi baadaye, Kanisa Katoliki lilianza kukiri makosa. Mnamo mwaka 1992, Papa Yohane Paulo II alikiri rasmi kwamba Galileo alihukumiwa kimakosa na kwamba Kanisa lilihitaji kujifunza kutokana na tukio hilo.

Yaani miaka yote hio kanisa kwa aibu limekija kukiri kumkosea Galileo mwaka 1992...

Always naamini katika sayansi ....

Science is the best!
 
Kiwango jumla cha maji duniani hakipunguwi wala hakiongezeki.Maji yapo kwenye mzunguko isiwo na kikomo Maji baharini,kwenye maziwa , mito,ardhi iliyo na unyevu kutokana joto la jua yanabadilika kuwa mvuke ambao hatimaye unakuwa mawingu. Mawingu ambayo ni mvuke ulioganda ndio chanzo cha mvua. Mvua inarutubisha,mito,maziwa,bahari na maji ya ardhini.Mzunguko unaendelea,kwa jina la kiaalamu hydrologic cycle.
 
Dunia nzima haiwezi kujaa maji?
Haiwezi wakati hapo mwanzo ilijaa maji?
Mwanzo 1
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
 
Kiwango jumla cha maji duniani hakipunguwi wala hakiongezeki.Maji yapo kwenye mzunguko isiwo na kikomo Maji baharini,kwenye maziwa , mito,ardhi iliyo na unyevu kutokana joto la jua yanabadilika kuwa mvuke ambao hatimaye unakuwa mawingu. Mawingu ambayo ni mvuke ulioganda ndio chanzo cha mvua. Mvua inarutubisha,mito,maziwa,bahari na maji ya ardhini.Mzunguko unaendelea,kwa jina la kiaalamu hydrologic cycle.
Basi umejiona msooooomiiiiii mwenyewe kwa kuandika "Hydrologic cycle" badala ya "Hydrological Cycle" 😁😁😁

Unaijua sayansi ya uumbaji mkuu? Unajua maji yalikuwa yameijaza dunia nzima na yakagawanywa sehemu mbili?
 
Biblia inasema:Maji yalizidi juu ya mlima mrefu(Mt Everest?) kwa dhiraa 15(mita 7) (Mwanzo 7:20)
Ilikufunika hadi kilele cha Everest dunia ingehitaji maji ya ziada kiasi cha takribani kilomita za ujazo bilioni 4.5 mara tatu ya maji yote yaliyopo kwenye bahari sasa.

Changamoto iliyopo hakuna chanzo kinachojulikana cha maji haya yote, wala sehemu ambapo maji hayo yangeenda baada ya mafuriko kumalizika.

Naomba mwongozo wa wana elimu.
Ushaambiwa aliefanya ni mungu so kila kitu ni miujiza. ni km musa kupasua bahari
 
Back
Top Bottom