Mafuriko ya Nepal yanahusiana vipi na kufukuzwa kwa Waislam

Mafuriko ya Nepal yanahusiana vipi na kufukuzwa kwa Waislam

Hazchem plate

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
11,059
Reaction score
15,534
Licha ya migogoro ya kijamii iliyotokea hapo awali, mashirika makubwa ya misaada ya Kiislamu kama vile Islamic Relief, Muslim Aid, na Muslim Response USA yamekuwa mstari wa mbele kuchangisha fedha na kupeleka misaada ya kibinadamu (chakula, malazi, na maji safi) kwa waathirika wote wa mafuriko nchini Nepal bila ubaguzi wa kidini.

lakini watu wengi wanadhani chanzo cha mafuriko hayo ni ghadhabu ya KiMungu baada ya waislam kugukuzwa, kuchomwa kwa nyumba na vitabu vya dini.

hii ina ukweli gani?
 
Attachments

  • IMG_2768.jpeg
    IMG_2768.jpeg
    62.3 KB · Views: 13
Hao watu wengi ni kina nani?
Maana vilaza wa kiimani hawakosi. Nchi za Waislamu wenyewe kama Turkey na Iran hukumbwa na matetemeko, Indonesia nchi yenye Waislamu wengi kwa namba duniani iko kwenye ukanda wa majanga ya asili kama mafuriko, tetemeko, milipuko ya volcano na tsunami.

Pakistan ya pili kwa idadi ya Waislamu duniani na ambayo inapigana na India dini ikiwa sababu mojawapo, nayo mwaka huu 2026 imepata mafuriko yaliua watu 900+ na kuhamisha makazi watu milioni 2. Mwaka jana 2025 ilipata mafuriko yakaua watu 1,000+ na kuhamisha mamilioni makazi. 2022 watu 1,700+ walikufa kwa mafuriko na nchi ilipata hasara ya zaidi ya trilioni 100 TZS.

Mafuriko yameanza kutokea kabla Mtume hajazaliwa. Zote hizo nchi tatu ziko location mbaya duniani, Nepal iko na steep slopes za Himalayas, Pakistan ina monsoon rains, Indonesia iko ukanda wa mvua nyingi, active volcanoes na tectonic plates zinazosuguana na kuleta tsunami.

Hakuna Mtume wala Yesu kwenye majanga hayo.
 
Quran 34:15-17

"Hakika ilikuwapo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. (Wakaambiwa) Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu.Lakini wakaacha. Tukawapelekea mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyengine zenye matunda makali machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi.Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyo kufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipo kuwa anaye kufuru?"
 
Quran 74:31

"....Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu."
 
Hakuna jambo la hatari kama kuishi karibu na Watu wasiomuamini Mungu au wale wenye kumshirikisha Mungu kwa kuabudia masanamu.

Aisee ukiona upo kwenye jamii hiyo basi kimbia maana ni watu ambao hawako mbali sana na adhabu ya Mungu. Chini yao ardhi inatamani kupasuka iwameze wakiwa hai na juu yao mbingu inatamani ichanikechanike na kuwafunika wakiwa hai.
 
Licha ya migogoro ya kijamii iliyotokea hapo awali, mashirika makubwa ya misaada ya Kiislamu kama vile Islamic Relief, Muslim Aid, na Muslim Response USA yamekuwa mstari wa mbele kuchangisha fedha na kupeleka misaada ya kibinadamu (chakula, malazi, na maji safi) kwa waathirika wote wa mafuriko nchini Nepal bila ubaguzi wa kidini.

lakini watu wengi wanadhani chanzo cha mafuriko hayo ni ghadhabu ya KiMungu baada ya waislam kugukuzwa, kuchomwa kwa nyumba na vitabu vya dini.

hii ina ukweli gani?
Acha ubwege, uzembe, ujinga, uzwazwa.
 
Nepal haijawah kufukuza waislam Achen akili ndogo. Ilikuwa ni Mynamar. kabila lake Rohingya ambao Wana dai ni wabangladesh
 
kama huyo mungu wenu kaamua kuua watu kwa stahili hiyo baada ya kupandwa na ghadhabu basi atakuwa hamnazo!
 
kama huyo mungu wenu kaamua kuua watu kwa stahili hiyo baada ya kupandwa na ghadhabu basi atakuwa hamnazo!
Sasa unashangaa haya ulishawahi kusikia kuhusu mafuriko yaliyowaangamiza watu wa Nuh?

Ulishawahi kusikia jinsi walivyozamishwa watu wa Firauni?

Hujawahi kusikia habari za watu wa miji ya Sodoma na Gomora jinsi walivyonyeshewa mvua ya mawe yenye moto na kisha walivyofudikizwa ndani ya ardhi?

Ulishawahi kusikia kuhusu Tsunami 2004? .... Ni kawaida kwa Mungu kuangamiza watu waovu mara baada ya kuwa kashawaonya sana ila hawakutaka kusikia.

Mungu sio tu anawaangamiza bali anafuta kabisa kumbukumbu au ishara kama kulikuwa na jamii ilikuwa ikiishi mahala hapo
 
Fatilia kinachofanywa na hao watu wa dini ya mabudha dhidi ya waislam
sio wanepal sasa na jamaa kwanza hawapigi waislam kama dini ila hiyo jamii ya warohingya. na sababu ni kuwa wanadai ni wageni kutoka Bangladesh walikuja wakakaa then wamezaliana so wanahis jamaa wanachukua utamaduni wao. mzee ukipata muda muwe pia mnasafir sio kulishwa stor tu. na hayo maeneo japokuwa mabudha ni wengi kuna dini nyingi. shida ni kabila mzee sio dini maana ukienda kila mahali ndan ya hizo nchi wapo waislam kwanini hapo tu. kuua sio jambo zur lakin kuunasibisha mauaji na dini ni ungese kama mwingine.
 
Licha ya migogoro ya kijamii iliyotokea hapo awali, mashirika makubwa ya misaada ya Kiislamu kama vile Islamic Relief, Muslim Aid, na Muslim Response USA yamekuwa mstari wa mbele kuchangisha fedha na kupeleka misaada ya kibinadamu (chakula, malazi, na maji safi) kwa waathirika wote wa mafuriko nchini Nepal bila ubaguzi wa kidini.

lakini watu wengi wanadhani chanzo cha mafuriko hayo ni ghadhabu ya KiMungu baada ya waislam kugukuzwa, kuchomwa kwa nyumba na vitabu vya dini.

hii ina ukweli gani?
kwa asilimia kubwa ninaweza kuwa ivyo coz yale mafuriko si ya kawaida hata kidogo,yanatisha hata kuyatazama kwenye cm au tv sipati picha waliokuwa wanayaona live
 
Back
Top Bottom