Mafuriko yalitaka kunitoa roho, ila Mungu hakutaka kabisa itokee

Mafuriko yalitaka kunitoa roho, ila Mungu hakutaka kabisa itokee

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Kwema Wananchi

Leo nimekumbuka tukio baya zaidi la ajali ambalo lililotokea mwaka 2014 nikiwa natoka kazini kupitia njia ya Jangwani ofisi ya mwendo kasi, zamani mlango/geti likiwa limekelezea upande kama unaenda kariakoo hivyo na kufanya maji ya mvua yanayotawanyika kutoka kwenye ofisi zao yapite moja kwa moja kuelekea mto mdogo ambao upo upande ule wa kuendea Kariakoo.

Basi, mkononi nilishika simu 2 pamoja na kiasi cha elfu 90 ilikuwa full shangwe naelekea kuvuka pale getini niliona maji madogo na kweli ilikuwa ni madogo tatizo kasi na pressure ya maji iilikuwa ni kubwa kupitiliza, nikiwa nmharakati ya kuvuka kuelekea home nimejikuta naingiza mguu kwenye shimo dogo tu!

Ghafla maji yakanichukua mguu mwengine yakawa yananipeleka kwenye mto mdogo uliokariana na stendi ya jangwani ya mwendokasi aiseeee! Mungu si athumani wala juma mti mdogo ndiyo uliokoa maisha yangu kwa kuegemea na kutoka mzima, salama kabisa.

Na ikumbukwe kabla ya mimi dk 3 nyuma kumbe kuna mmoja alichukuliwa na maji.

Kheri yangu mpk sasa ni mzima wa afya.
 
Mimi nilikoswa koswa sehem moja inaitwa kambi ya mchanga ni mtoni tunaenda na malori kupakia mchanga. Siku hiyo mvua imenyesha huko juu sisi tunapakia mchanga tu. Akaja jamaa akasema ondokeni haraka sana hapa, nikawaambia jamaa fanyeni chap tumalize tukitoe.sijamaliza kauli yng naskia sauti km tren inakuja. Nikawa napambana niichomoe gari inazimika.asee nilipata kihoro ikabidi niruke nipande juu ya kilima.gari ilisombwa ile km kiberiti.
 
Mimi nilikoswa koswa sehem moja inaitwa kambi ya mchanga.ni mtoni tunaenda na malori kupakia mchanga.siku hiyo mvua imenyesha huko juu sisi tunapakia mchanga tuu.akaja jamaa akasema ondokeni haraka sana hapa.nikawaambia jamaa fanyeni chap tumalize tukitoe.sijamaliza kauli yng naskia sauti km tren inakuja.....nikawa napambana niichomoe gari inazimika.asee nilipata kihoro ikabidi niruke nipande juu ya kilima.gari ilisombwa ile km kiberiti
Duuuuuh pole mzeeewengine walipona?
 
Back
Top Bottom