Waberoya,
Nashukuru kwa mchango wako, lakini kuna kitu kinanitatiza kuhusiana na majibu yako.
Sisi tuna barabara, reli, nyumba, mitaro, mabwawa, mifereji na miuondo mbinu mingine ambayo bila hata ya kupatwa na misukosuko kama kimbunga, mafuriko, tetemeko au Tsunami, tunashindwa kuona ubora wake na uweo wa kustahimili!
Mfano tuchukulie barabara zetu, ni vipi mpaka leo hii, tunashindwa kuwa na barabara nzuri na imara?
Hivyo kwa hilo la Wahandisi, niauliza kwa kutumia kigezo kidogo kama barabara na hata nyumba.
Au ni uroho na mazoea ambayo yamekuwa kawaida ya Watanzania kutofanya mambo kwa tathmini na kwa thamani kamili na kukimbilia kufisadisha kila kitu?
Ikiwa tunaambiwa mfuko mmoja wa Twiga, Simba au Tembo kwa wastani unaweza kutoa matofali bora 35-39, lakini mhandisi anatumia mfuko huo huo mmoja na kufyatua matofali 60, pamoja na kuwa pesa zipo, unajiuliza, kwa nini mhandisi afanye upuuzi kama huo?
Je Nyani Ngabu maarufu kama Julius yupo sahihi kusema ndivyo tulivyo?