Mafuriko yanatutoa jasho, yakitokea yaliyotokea Haiti jee?

Waberoya,

Nashukuru kwa mchango wako, lakini kuna kitu kinanitatiza kuhusiana na majibu yako.

Sisi tuna barabara, reli, nyumba, mitaro, mabwawa, mifereji na miuondo mbinu mingine ambayo bila hata ya kupatwa na misukosuko kama kimbunga, mafuriko, tetemeko au Tsunami, tunashindwa kuona ubora wake na uweo wa kustahimili!

Mfano tuchukulie barabara zetu, ni vipi mpaka leo hii, tunashindwa kuwa na barabara nzuri na imara?

Hivyo kwa hilo la Wahandisi, niauliza kwa kutumia kigezo kidogo kama barabara na hata nyumba.

Au ni uroho na mazoea ambayo yamekuwa kawaida ya Watanzania kutofanya mambo kwa tathmini na kwa thamani kamili na kukimbilia kufisadisha kila kitu?

Ikiwa tunaambiwa mfuko mmoja wa Twiga, Simba au Tembo kwa wastani unaweza kutoa matofali bora 35-39, lakini mhandisi anatumia mfuko huo huo mmoja na kufyatua matofali 60, pamoja na kuwa pesa zipo, unajiuliza, kwa nini mhandisi afanye upuuzi kama huo?

Je Nyani Ngabu maarufu kama Julius yupo sahihi kusema ndivyo tulivyo?
 
Hivi, moto ulipotokea kule Tabora kwenye Disko siku ya Iddi El Fitri, mafuriko yalipozoa watu Same, Meli ilipozama pale Lake Vctoria, Jengo la Nasaco, BOT na mengine yalipooungua, ilituchukua muda gani kuweza kudhibiti maafa na kuokoa maisha ya watu na mali?
 
Rev Kishoka
Nakwambia nivyosikia ya Haiti, akili ilinijia yakitokea Tanzania ni balaa. Fikiria ya Kilosa tu sasa hivi, tabu bin tabu.
Dar ukiangalia mifereji ya kupitisha maji tumegeuza dampo, tunataka nini sisi lakini?
Tanzania hatuhitaji ya Haiti, barabara tu zinamaliza watu ila watawala bado wanadhani 'ajali haina kinga'

Miafrika Ndivyo Tulivyo NN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…