Mafuta au Manukato ya Bint Sudan

Mafuta au Manukato ya Bint Sudan

Kwetu sisi binadamu na hata wanyama kuna kuwa na nguvu fulani za mvutano ambazo ni Hasi na Chanya ambazo zinamsaidia sana kwenye mahusiano na mwingiliano na watu wengine.
Ndio, pale unakuta watu wanasema fulani ana bahati sana au fulani ana mikosi sana..hii inatokana na nguvu alizonazo mtu na kuna wakati nguvu hizo zinafifia au kukosa nguvu.
Hivyo, ili kuzihuisha nguvu hizo haiwi vibaya kutumia njia mbali mbali ili kungarisha mvuto wako na ndio maana wapo humu JF walioelezea manufaa ya kuongea Chumvi ya Mawe nk.
Kwa minajili ile ile matumizi ya hayo mafuta pia yanasaidia kwenye kuongeza mvuto Hasi kwa anae yatumia na wala hakuna uhusiano wowote na Majini.
Ikumbukwe pia manukato yote tunayoyatumia yanawekwa na kutengenezwa na vitu ambavyo vinaleta mvuto kwa mtumiaji na wale walioko jirani yake..vitu hivyo ni kama vile Ambari inayotokana na samaki, Musk inayotokana na Mnyama(Deere/Ghazal),Udi inayotokana na Mti nk.
 
Wadau Habari zenu,

Naomba kufahamu zaidi kuhusu haya manukato (mafuta) yanayoitwa Bint Sudan ambayo watu tofauti huyatumia kama manukato tu ya kawaida na wengine tiba ya mambo tofauti kama kunuka KIKWAPA, lakini pia wengine hutumia kitaalamu zaidi kwa ajili ya kuondoa Nuksi na Mikosi.

Sasa mimi ninachohitaji kujua, ni kweli kwamba ukiyatumia kwa kujipaka yanaweza kuleta majini kwako au kwa mtu wa karibu yako?

Maana wengine wanayasifia na mengine wanayaponda na kudai yana uhusiano wa karibu sana na majini (mapepo).

Attachments​

  • 1712999629417.jpg
Mafuta ya Binti sudan hayo uliyo onyesha ni feki yenyewe orignal yana kifuniko chekundu.
image-1.png




View:
 
Back
Top Bottom