Mafuta kwenye ini

Mafuta kwenye ini

nsalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
1,189
Reaction score
1,240
Nilikwenda kufanya kipimo cha ultrasound kwa ajili ya tatizo la uzazi dokta akanipima ini na figo akaniambia kuwa ini lina mafuta. Naomba wenye utaalamu mnieleweshe mwenzenu ini kuwa mafuta kunasababishwa na nini.

Nitumie nini kuondoa hayo mafuta. Huwa sipendelei kula vyakula vyenye mafuta mengi nashangaa hayo mafuta yametoka wapi jamani.
 
Kwanini usingemuuliza huyo daktari aliyekupa taarifa hizo? Unatuamini zaidi sisi madaktari vishoka kuliko daktari halisi!
 
Hiyo hali ilimtokea dogo mmoja, alivimba tumbo likawa linamuuma mpk kukaa anashindwa, kula napo tabu. ..tukampeleka aar wakampima na kugundua ini lina mafuta. ...wakampa dawa baada ya kipindi akawa fresh kabisa ..We ni mnywaji wa pombe?
 
hiyo ni hatua ya mwanzo kabisa ya kuelekea ugonjwa mbaya kabisa unaoua wa HEPATITS,
inabidi ufanye sana mazoezi na kuwahi tiba mapema kabla ya kufikia stage ya mwisho.
 
Asante ndugu yangu kwa ushauri mzuri. Naenda hospitali mara moja.
 
Hiyo hali ilimtokea dogo mmoja, alivimba tumbo likawa linamuuma mpk kukaa anashindwa, kula napo tabu. ..tukampeleka aar wakampima na kugundua ini lina mafuta. ...wakampa dawa baada ya kipindi akawa fresh kabisa ..We ni mnywaji wa pombe?
Hapana sinywi pombe ndugu yangu. DUUU Sikujua kama ni tatizo kubwa namna hiyo. ngoja niwahi hospitali.
 
Kwanini usingemuuliza huyo daktari aliyekupa taarifa hizo? Unatuamini zaidi sisi madaktari vishoka kuliko daktari halisi!

Nashukuru. Ila kama huna jibu ungenyamaza tu ingekuwa vizuri zaidi. Wanaojua wameshanijibu na nimeshachukua hatua.
 
Si mnywaji wa pombe ila nina kisukari.

Back
Top Bottom