Brightman Jr
JF-Expert Member
- Mar 22, 2009
- 1,224
- 234
Waheshimiwa wakuu naomba ushauri wenu. Mara nyingi ngozi yangu inatatizo la kutoka vipele vilivyo mfano wa chunusi pale ninapojipaka mafuta hususan baada ya kuoga. Vipele hivyo hutokea baada ya siku tatu na huendelea kutoka kadri ninavyoendelea kujipaka. Nikiacha kupakaa mafuta vipele navyo hukoma kujitokeza. Nimejaribu kukaa bila kupaka mafuta kwa kipindi fulani, na ngozi yangu katika wakati huo hubadilika kuwa kavu isiyopendeza. Wataalam naombeni ushauri nitumie mafuta aina gani ili ngozi yangu ipendeze na iwe soft? Lotion nyingi nimejaribu hizo ndo hatari kabisa! Nawasilisha.