Mafuta mazuri ya kuifanya ngozi iwe soft

Mafuta mazuri ya kuifanya ngozi iwe soft

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Waheshimiwa wakuu naomba ushauri wenu. Mara nyingi ngozi yangu inatatizo la kutoka vipele vilivyo mfano wa chunusi pale ninapojipaka mafuta hususan baada ya kuoga. Vipele hivyo hutokea baada ya siku tatu na huendelea kutoka kadri ninavyoendelea kujipaka. Nikiacha kupakaa mafuta vipele navyo hukoma kujitokeza. Nimejaribu kukaa bila kupaka mafuta kwa kipindi fulani, na ngozi yangu katika wakati huo hubadilika kuwa kavu isiyopendeza. Wataalam naombeni ushauri nitumie mafuta aina gani ili ngozi yangu ipendeze na iwe soft? Lotion nyingi nimejaribu hizo ndo hatari kabisa! Nawasilisha.
 
Nenda S.H amon mtafute mdada yeyote apo akushauri ila angalia usiangukue kwa jamaa m1 hapo nasikia ameumia
 
chukua mafuta ya korie (refined palm oil), kama mils 250 pamoja na mchaichai (lemon grass) handful 2 au 3 zilizokatwa katwa; chemsha hayo mafuta na mchaichai. Baadaye yaache yapoe; hayo ndio mafuta yako!
 
Ushauri wako mkuu nitaufanyia kazi na baada ya wiki mbili nitakuPM nikupe results.
 
Mmmmh................?! Mkuu niende wapi kutatua tatizo linalonisibu au nifanyeje?

Nenda maryrose cosmetics watakupa ushauri mzuri sana.S H amons sikushauri,watakupa mengi ambayo utatumia gharama kubwa na wala usifanikiwe
 
Usiende S.h amon watakuharibu.

Bora uwaambie.S.H. Amon toka lini wakawa dermatologists?
Nimeona siku hizi hata yule mlinda mlango amepewa promotion ni beauty consultant lol.
Muuliza swali kuna vitu vya kuzingatia:
1. Umezungumzia kupaka "mafuta" hujasema ni mafuta gani.Kama ni mikorogo ujue tatizo linaanzia hapo.
2. Unatakiwa ujue aina ya ngozi yako - kuna oily, dry na combination skin types.Hii itakusaidia kujua ununue mafuta gani kwa ngozi yak😵ily na combination japo ni nzuri kwa maana ya kutokupata mikunjo ya uzee mapema, tatizo lake ni kulipuka matatizo ya ngozi hasa chunusi/acne.
3. Jichunguze ratiba yako na utaratibu wa kutunza ngozi yako. Kwanza kabisa osha uso wako mara mbili kwa siku minimum. Oshea sabuni maalum ya ngozi na nikisema sabuni haimaanishi sabuni za kujichubua.Nenda duka la dawa au supermarkets utapata hizi sabuni/cleansers.Tumia toner baada ya kuosha ili kuiweka ngozi katika usafi kamili. Malizia na lotion ya aina ya ngozi yako.EPUKA MIKOROGO! Hata siku moja usilale na make-up.
 
Nkushaurivo nikwamba heri uende kwenye duka la karibu la mambo hayo ya urembe coz wataalamu ni wengi siku hizi so watakushauri vizuri kutokana na aina ya ngozi yako watakavo kuona, so sikila ushauri humu utakufaa nivema ngozi yako ikaonwe kwanza na wataalamu wangozi ndivo tunavofanya ndugu.
 
mm mwenyewe najua S.H hamon is one of greatest cosmetics retailers in dar na wanao watalaam wao wa mambo ya ngozi....not sure of maryrose..
 
Jaribu na kupima UKIMWI, inawezakuwa ni sababu mojawapo. Maji unakunywa? unapaka mafuta gani? wewe ni mwanaume?
Waheshimiwa wakuu naomba ushauri wenu. Mara nyingi ngozi yangu inatatizo la kutoka vipele vilivyo mfano wa chunusi pale ninapojipaka mafuta hususan baada ya kuoga. Vipele hivyo hutokea baada ya siku tatu na huendelea kutoka kadri ninavyoendelea kujipaka. Nikiacha kupakaa mafuta vipele navyo hukoma kujitokeza. Nimejaribu kukaa bila kupaka mafuta kwa kipindi fulani, na ngozi yangu katika wakati huo hubadilika kuwa kavu isiyopendeza. Wataalam naombeni ushauri nitumie mafuta aina gani ili ngozi yangu ipendeze na iwe soft? Lotion nyingi nimejaribu hizo ndo hatari kabisa! Nawasilisha.
 
je nilazima upake mafuta usoni?
Amesema ameshajaribu kuacha kupaka lkn ndani ya kipindi kifupi tu ngozi yake imekuwa mbaya zaidi,itakuwa ilikuwa ngumu km ya kenge ktk kipindi ameacha kupaka kabisa
 
Back
Top Bottom