figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Tanzania imefungua vizuizi vya utafutaji wa mafuta ndani ya Ziwa Tanganyika, mojawapo ya maziwa makubwa zaidi ya maji safi duniani yaliyyo kati ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia.
Ziwa hilo linamiliki 17% ya maji safi duniani, lina zaidi ya spishi 1,500, na linasaidia maisha ya zaidi ya watu milioni 10.
Tanzania imefungua Vitalu vya Utafiti wa mafuta na gesi, ikiwa ni pamoja na maeneo ndani ya ziwa tanganyika, na kuruhusu makampuni Makubwa ya nishati kutafuta mafuta chini ya ziwa Tanganyika.
MY TAKE
Nadhani Samia angetuambia Mafuta ya Mtwara tunapata bei gani.
Alitakiwa ahakikishe Nchi inapata faida na kuziba mianya ya rushwa kwenye miradi ya Gesi, Mafuta na Madini.
Samia ameshauza Urithi wa Watanzania kuanzia bandari zote.
Anataka aondoke madarakani akiwa ameuza na ziwa Tanganyika?
Malengo ya Nchi kwa kipindi hiki ni kusamabza maji ya Zaiwa Tanganyika katika maeneo ambayo hayana maji jirani na Ziwa hilo.
Wakianza kuchimba mafuta, wananchi Wasahau kuhusu kutumia maji hayo.