- a. hakikisha unanunua spark plugs original kwa ajili ya aina ya gari lako, kila gari ina spark plugs zake zimetofautiana joto, urefu, n.k. kama unatumia Toyota nenda kwa dealers wao wakupe aina ya pluga inayofaa kwa gari yako, plug moja inaweza kuwa ni elf 60 ila zinapiga kazi kwa kilometa laki 1 (miaka zaidi ya 7 kwa mizunguko ya mjini), ni bora kuzidi kununua plugs za elf kumi au 15 halafu unabadili kila baada ya miezi 6 au mwaka na huwa zinakula zaidi mafuta kuzidi original.
- b. Weka mazoea ya kujaza kuanzia lita kumi kabla taa nyekundu haijawaka, pampu ya mafuta huwa inafanya kazi vizuri kwa ufanisi mafuta yakiwa yameenea vizuri, Mafuta yanapokuwa kidogo sana (chini ya lita 10–15), matuta, mashimo na barabara zetu korofi husababisha pampu wakati mwingine kunyonya hewa, Pampu ya mafuta hutegemea mafuta kwa ulainishaji (lubrication) na kupoeza (cooling).
- c. kama gari yako ni used na hujawahi kabisa kusafisha fuel filter ya kwenye pampu nakushauri kaisafishe. kuwa mwangalifu wasikubadilishie motor, inapendeza zaidi wasafishe hapo hapo ukiwa unaona wasiende mbali, huwa ni process ya kutoa vitu viliyonasa kwenye chujio kama vumbi, mafuta machafu, n.k. . hii pia inaweza kuwa suluhisho la matatizo kama gari kujizima, kupata ugumu kuwaka, kukosa nguvu, n.k.
- d. Jaribu kujaza mafuta kampuni moja tu, usipende kuchanganya changanya. kama ni total iwe total, kama ni puma iwe puma, kama ni oryx iwe hivyo, n.k. pendelea kujaza kampuni kubwa na vituo vinavyoaminika, kama umechanganya sana nenda gereji hasa zile za kwenye vituo vya mafuta vikubwa waambie watoe tenki wamwage mafuta yote uanze upya, makadirio ya huduma hii ni elf 20 hadi 40 (pamoja na kusafisha filter ya pampu).
- Kama unapanga kutumia petrol treatment, ni bora uchague ile inayotoka kwa kampuni unayonunua mafuta yao. Kwa mfano, ukijaza mafuta ya Total, tumia petrol treatment yao rasmi utayoweza kuipata kwenye vituo vyao vya mafuta.