Mimi huku nilipo nimeona maeneo mengi ya wafanyabiashara wa mananasi wanauza na kutoa maganda ya mananasi kuwapa wateja kwa wanaoomba.
Ila nimeona wateja wengi ni wakike wanasema maganda ya mananasi yanatibu U.T.I kama ukichemsha na kunywa maji yake.
Je, kuna ukweli wowote U.T.I inaondolewa kwa tiba asili kama hiyo?
Ila nimeona wateja wengi ni wakike wanasema maganda ya mananasi yanatibu U.T.I kama ukichemsha na kunywa maji yake.
Je, kuna ukweli wowote U.T.I inaondolewa kwa tiba asili kama hiyo?
- Tunachokijua
- Ufafanuzi wa Dkt Bernard Kivuma wa Ifakara Mkoani Morogoro.
Majani ya nanasi yana kemikali iitwayo acetic acid, ambayo imeoneshwa kwenye majaribio ya kimaabara kuwa na uwezo wa kuzuia ukuaji wa bakteria kama Enterococcus faecalis anayesababisha UTI (The antimicrobial effect of acetic acid--an alternative to common local antiseptics? - PubMed).
Hata hivyo, hali hii haijaoneshwa kutokea ndani ya mwili wa mwanadamu anayekula maganda au majani ya nanasi.
Hii ni kwa sababu ili dawa au kemikali iweze kufanya kazi kwenye eneo husika la mwili, inahitaji kufikia kiwango fulani cha wingi (concentration) kinachohitajika kufanya kazi hiyo.
Kwa upande wa UTI, mtu akila maganda au majani ya nanasi, kemikali hizo zitapitia kwanza kwenye mfumo wa chakula na umeng’enyaji, kisha zichukuliwe na mwili na kusafirishwa kwenye damu, ziende kwenye figo, na hatimaye kufika kwenye mfumo wa mkojo.
Hili ni vigumu kutokea kwa kiwango kinachoweza kutibu UTI, kwa sababu mfumo wa umeng’enyaji utakuwa tayari umevunjavunja kemikali hiyo kabla haijafika kwenye njia ya mkojo kwa kiwango kinachohitajika kuweza kudhibiti maambukizi ya UTI.
Kemikali nyingine inayopatikana kwenye nanasi, iitwayo bromelain, imeoneshwa ikitengenezwa kama tiba mbadala kwa njia ya vidonge maalum husaidia kupunguza uvimbe mwilini (inflammation).
Hii ni kwa sababu vidonge hivyo hutengenezwa kwa mfumo unaosaidia bromelain isipotezwe haraka kwenye mazingira yenye tindikali (acid) tumboni kabla haijafyonzwa vizuri mwilini.
Hata hivyo, bromelain yenyewe sio tiba ya UTI. Tafiti zinaonesha kuwa inaweza kusaidia kuongeza upenyaji wa dawa za UTI kwenye tishu za mfumo wa mkojo zilizoathirika, hivyo hutumika kama njia saidizi pamoja na dawa za antibiotic, na sio kama tiba pekeyake.
Tafiti zimethibitisha kuwa tiba sahihi ya UTI ni matumizi ya dawa za antibiotic pamoja na kunywa maji ya kutosha kusaidia kusafisha njia ya mkojo (Uncomplicated Urinary Tract Infections - StatPearls - NCBI Bookshelf).