Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM imetoa tamko leo Disemba 5, 2025 jijini Arusha, ikiwataka Watanzania kuacha vitendo vya vurugu na uharibifu wa mali za umma na binafsi, ikisisitiza kuwa njia hiyo siyo suluhisho la changamoto za Taifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa, Fadhili Maganya, amesema maisha hayakosi changamoto na uongozi wowote una mapungufu yake, lakini kutatua matatizo kwa kuchoma magari, Vituo vya Mafuta, kuharibu biashara na miundombinu ni sawa na kuongeza maumivu mapya kwa Wananchi.
Soma pia: Maganya: Mtu hawezi kwenda kumshika mama mkwe sehemu za siri, na sisi hatutakubali mtu ambeze Rais Samia
Maganya ameifananisha nchi na boti kubwa lililobeba Watanzania zaidi ya Milioni 61, akieleza kuwa kulitoboa boti kwa madai ya kumtafuta “mchawi” ni uamuzi wa kujiangamiza kwa pamoja, kwani tukizama hatazama mtu mmoja bali Taifa lote.
Akirejea matukio ya Oktoba 29, Maganya amesema yamesababisha vifo, hofu kwa Wananchi, kufungwa kwa shughuli za kijamii na kiuchumi, pamoja na hasara kubwa ya mali na fedha zilizolazimika kutumika kurekebisha uharibifu wa miundombinu.
Amehitimisha kwa kutoa wito kwa Watanzania kutanguliza amani, busara na uzalendo, akisema wazi kuwa Taifa tukilivuruga na nchi ikawa haitawaliki, hakuna Mtanzania atakayekuwa salama wala kuwa na mahali pa kwenda.