Magari 24,521 yanaswa kwa malimbikizo ya faini barabarani Tanzania

Magari 24,521 yanaswa kwa malimbikizo ya faini barabarani Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
magari.jpg

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Tanzania, Wilbroad Mutafungwa amesema katika kipindi cha siku tano zilizopita, idadi ya magari 24,521 yamekamatwa kupitia oparesheni ya ukamataji wa magari yenye malimbikizo ya faini zinazotokana na makosa ya barabarani.

Akizungumza na wanahabari leo Januari 25, 2021 Jijini Dar es Salaam, Kamanda Mutafungwa amesema oparesheni hiyo iliyoanza Januari 20, 2021 itaendelea katka mikoa yote hadi Februari 20, mwaka huu chini ya utekelezaji wa Kanuni za faini ya makosa barabarani za mwaka 2011.

“Makosa yanayosababisha zaidi uvunjifu huo wa sheria za barabarani ni pamoja na madereva kutumia mwendokasi maeneo ya makazi, kutosimama katika mistari ya zebra na ku-overtake(kulipita gari kwa mbele wakati wa mwendokasi), “alisema Mutafungwa.

Katika oparesheni hiyo, maofisa wa jeshi hilo wakiongozana na baadhi ya maofisa wa Mawasiliano Mamlaka ya Mapato Tanzania wameendelea na ukaguzi wa magari mitaani, maeneo ya kupaki magari, maeneo ya kutengeneza magari(gereji) au maeneo mahali penye mzunguko wa magari.

“Sasa kutokana mazingira hayo tumeamua kuanzisha msako mkali ili kuhakikisha madeni yaliyotokana na tozo za usalama barabarani yanalipika kwa maana ya kuwapata wahusika na magari husika ili walipe madeni, kwa kufanya hivyo adhabu ndio itakuwa imekamilika tuliyoitoa,”amesema.

Mutafungwa amesema miongoni mwa sababu za malimbikizo ya madeni hayo ni pamoja na wamiliki wa magari kukosa utamaduni wa kukagua magari baada ya kuyaazimisha kwa madereva wenzao na wamiliki kutofanya ukaguzi wa magari baada ya kuwaachisha kazi madereva.

Kwa mujibu wa Mutafungwa, tayari kiasi cha Sh1.4bilioni kati ya Sh11bilioni zimeshakusanywa ndani ya siku hizo tano ikiwa ni siku 25 zimebakia kabla ya kufunga oparesheni hiyo inayoendana na usimamizi wa sheria pamoja na utoaji wa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri nchini.
 
Hayo magari wakiyashika wanayapeleka wapi? Wanayatunza kuyaangalia kwa cost za nani? Au ndio hao wakosaji huenda wakajikuta badala ya kumili gari wanamiliki scrapper lilishaibiwa kila kitu.

Pia kama gari lipo garage huoni kwamba ni sababu tosha ya mtu kutokulipa. Hizi sheria zisiwe kukomoana bali kuendelezana na kusaidiana.
 
Hayo magari wakiyashika wanayapeleka wapi ?, wanayatunza kuyaangalia kwa cost za nani ? Au ndio hao wakosaji huenda wakajikuta badala ya kumili gari wanamiliki scrapper lilishaibiwa kila kitu.

Pia kama gari lipo garage huoni kwamba ni sababu tosha ya mtu kutokulipa. Hizi sheria zisiwe kukomoana bali kuendelezana na kusaidiana
Wamekusaidia kistaarabu kabisa kwa kukuwekea sheria za barabarani, umezikiuka halafu umetimua na kujificha kusikojulikana. Wakusaidieje sasa, kimfano!
 
Wamekusaidia kistaarabu kabisa kwa kukuwekea sheria za barabarani, umezikiuka halafu umetimua na kujificha kusikojulikana. Wakusaidieje sasa, kimfano!???
Ukilipa / kutoa pesa ndio kujua sheria ?, Ningeelewa kwa wale watenda makosa ya kiundeshaji kunyanganywa leseni au kupunguziwa points kwenye leseni (wasilete maafa).., sasa kuwatoza watu faini ndio lile gari linapona ? (Msaada ni magari yenye mapungufu yasiingie barabarani) watenda makosa mfululizo warudishwe VETA hapo ni kumlinda mpaka mtembea kwa miguu
 
Hizi tozo zina-involve a range of different traffic offences, sawa! Psychological physicists wanasema ziko dimensions zaidi ya 16 za reasoning, and you don't seem to have approached even a third of the first dimension.
 
Endapo Raisi atakabidhi taasisi nyingine zitoze fine barabarani basi hiyo idadi ya itakuwa ni Lukuki kwa muda mfupi kisha Makosa yatapungua kila siku zinavyokuja kwani Raia watakuwa waangalifu mno...

Kwenye neno la Kuwakabidhi magari Madereva hilo ni tatizo kubwa tulionalo wananchi kwani Unakuta Taa zimeungua Dereva habadilishi Taa zimepasuka anadundisha gari barabarani...

Kuna Makosa mengi ya kuonya lakini Polisi wanakaza mno ili wapewe kidogodogo...

Kuna Askari aliyepo Maeneo ya Barabara mtaa wa Bibi Titi karibu na Mahakama ya Kisutu DSM, zamani alikuwa na uniform za Traffics but sasa kavalishwa khaki sijamuelewa ni kwamba alizoea Rushwa hadi sasa na hizo nguo za khaki na kipande cha karatasi akijaza namba za leseni za waendesha Magari as if yeye bado ni Traffic Polisi bora hata anekuwa na ile Mashine ya Notification tungejua katumwa ila mla Rushwa naomba Takukuru wamumulike , Naomba RTO amuondoshe kwani alizoea kupewa chochote sasa baada ya kuvuliwa utraffic kazi mpya ya kukamata waharifu hataki au kuna watu wanamlinda haswa Traffic wenzake?
 
Hizi tozo zina-involve a range of different traffic offences, sawa! Psychological physicists wanasema ziko dimensions zaidi ya 16 za reasoning, and you don't seem to have approached even a third of the first dimension.
Hauitaji kuwa rocket scientist kuona kwamba kubadilisha offences kama chanzo cha mapato kutapelekea ufanisi wa policing upimwe kwa wangapi wameshikwa na sio education usimamizi umepelekea wangapi kutoshikwa hence kwamba uhalifu umepungua...

Sio sifa kutangaza kwamba tumekusanya kiasi fulani toka kwa traffic offences kwa jicho lingine ni kwamba uhalifu umeoongezeka
 
Hayo magari wakiyashika wanayapeleka wapi? Wanayatunza kuyaangalia kwa cost za nani? Au ndio hao wakosaji huenda wakajikuta badala ya kumili gari wanamiliki scrapper lilishaibiwa kila kitu.

Pia kama gari lipo garage huoni kwamba ni sababu tosha ya mtu kutokulipa. Hizi sheria zisiwe kukomoana bali kuendelezana na kusaidiana.
Hawana haja ya kukamata gari na kulipeleka yard, wanaingiza kosa la kila gari kwenye mtandao, hivyo usipoenda kulipa wana vimashine vyao gari ikipita vinapiga picha na ya gari na kuingiza kwenye system, hivyo wanakudaka.
 
Hizo wanazozifuata mpaka parking na kwenye ma-garage (wakimaanisha kwamba hawa hawajalipa zile fines) kwa msako mkali wanazipeleka wapi ? wanaongeza fine juu ya fine ?
 
Na chanzo cha usalama na nidhamu barabarani. Don't forget that. Imagine kama wangeendesha kistaarabu kwa kufuata sheria za barabarani kama wengine, yangetoka wapi magombano, basi!???
Take it from me, hicho kiasi alichosema huyo kamanda nusu yake imeliwa as rushwa. Imagine juzi nimesimamushwa wakakagua leseni, sijui bima, fire extinguisher, triangle [emoji668] za parking... Yaani huchomoki, usipowapa elfu 5 huchomoki..
 
Back
Top Bottom