Yuko vizuri huyo, muhimu kwenye gari yoyote ni maintaincance lakini kuna common issues na hasa 745 za 2002, kesi nyingi water leak, idrive, na gearbox kugoma kubadili gear, na hii yote ni kwa sababu haya magari kutwa yapo under electronic input, sensor moja tu ikigoma mara gari inachanganyikiwa, na gari zao ukiidharau taa ya check engine utakuja kujuta. Mana utasema izi gari makusudi wamezipanga ziharibike na kusumbua zikifika km fulani. Ukiingia beforward 7 series unazikuta cheap mpaka unashangaa kweli hii BMW? Lakini value yake imeshuka kwa sababu repair costs doesnt make sense at all. Mi nshapanga ipo siku nitanunua japo hio ya 2002-3-4 engine ikisumbua, unashusha unaweka V8 ya toyota tu lakini unabakisha control box ya bimmer kwa ajili ya features za bmw na control box ya toyota kushughulikia engine tu.