Habari wakuu,
Kuna hawa waagiza magari wanaitwa HEDGARS MOTORS niliwapatia pesa ya kuniagizia gari tangu Mwezi wa sita, Ilipofika mwezi wa saba mmiliki wa hiyo ofisi (HEDGAR MSUYA) alipotea hewani na kutokupatikana tena na ofisi wakafunga mpaka hivi sasa bila ya kutoa taarifa zozote kuhusu hela zetu alizochukua kutuagizia magari. Naomba msaada kama kuna yeyote aliye na updates zozote za hii ofisi, au mwenye changamoto kama yangu na hii ofisi. Napokea ushauri kuhusu namna ya kufanya kuhusu hii case.