TUKUMBUSHANE
USINUNUE PLATE NUMBER NUNUA GARI
Nina kigari changu MAZDA DEMIO ambako kana namba CYZ ..hakana kazi Sana ni ka mara moja moja kama nikikosa mafuta kwenye mnyamaa (F) nikaona nikapush jamaa mmoja alikuwa anakapenda haka kagari kutokana na condition yake.binafsi nlikanunua sababu ya mamsap baadaye akaja kuzingua ..!!
Kiukweli gari ipo vizuri imetembea kms 60000 plus.jamaa akaja nikamwonesha gari akakagua na kumuita fundi wake mtalaam..maana siku zote nabii hakubaliki nyumbani mwake .... Fundi akanishtua chamber ENGENEER changamka kuwa yeye ntampa tsh ngap.nikamuuliza kwa kazi gani?yeye hakagui kwa niaba yangu.so why nimlipe?halafu mm narushwa mbalimbali nikamwambia maandiko yanasema uwe mwaminifu mpk kufa ,akadai ili jamaa anunue anahitaji maoni yake.nlimkatalia....huo upuzi staki mm hataki asepe
Wakaondoka jamaa hakusikika tena kuzungumzia gari.bahati nzuri work mate wangu tupo vitengo tofauti after a week namwona ana IST namba DPU.sikumuuliza kitu.
But nlishangaa mlio wa ile gari na inatoa moshi kama gari moshi.unaweza sema ina smoke.week mbili anakuja job kwa daladala.akawa hasemi kitu ila maji yakazidi unga akaamua vunja ukimya. Kuwa fundi wake alimwambia ile gari yangu haifa namba C akampeleka kwa jamaa mwingine. Ile gari alinunua baada ya siku mbili ikawa haiwaki.akampigia muuzaji.muuzaji akamtumia namba ya simu ya umeme wa magari,gear box na fundi wa engine.
Yaani alimuuzia gari na kumkabidhi namba za mafundi.kigari kinapiga kelele.,kinavibrate...kama kina majini sometime kinajiongeza speed chenyewe.hapo kama kimefurahi
Kikiudhika kinajishusha speed unakanyaga mafuta mpaka mwisho kinakuwa hakitaki kwenda...hapo kimeamua kususa.mimi gari yangu nafanya service tu sijawahi gusa engine wala gearbox.
Jamaa kaenda nunua plate number kigari kinamtesa balaaa...kauziwa gari na kupewa namba za mafundi kakikata umeme anaitwa fundi wa umeme.kakigoma kuingia gear anaitwa wa gearbox n.k
Narudia jamani hela ngumu hebu kuweni makini uzuri wa gari haupimwi kwa plate number kwa taarifa yako kuna mbinu moja baadhi ya wenye tamaa wanaifanya wanatafuta card ya gari lilopata ajali number D ,..mengi huwa yanachinjwa kama screpa ananunua kadi kama ni ya IST na anabadua ile plate number Anaenda kuweka kwenye Gari iliyochoka number A analenga kwa bei ndogo anabadili plate number ....na kupigwa ki rangi cha laki 3 halafu anatagaza kuuiuza kinachofata watu wakiona number D hawalinganishi document na serios number za injini na chasisi number tayari keshalizwa
Watu wanadhani kuwa eti gari ikiwa number D ndio inakuwa iko poa huko ni kujidanganya unako lala wewe mwenzako ndiko wanakoamkia utalizwa sana wajuaji huwa wanaulizwa na wajuaji kuliko wao
Kuna gari zimekaza lakini ni number A,NUMBER B ,NAMBA C NA NO D ,ZIPO USIKIMBILIE KUNUNUA GARI KWA KUANGALIA PLATE NUMBER UTAANGUKIA PUA SHAULI YAKO
Wadau mnapununua magari zingatieni ubora wa gari siyo plate namba.pateni mafundi wastaarabu na wa kweli siyo fundi dalali..... Halafu waje wawalizie kagua injini endesha uone gerbox inavyopokea maelekezo kutoka kwako .. haya yote nishafundisha lakini watu wanalizwa na mafundi dalali,njoo kwetu jerry empire sehemu pekee utapouziwa gar na kuambiwa kila aina ya chngamoto ya gari na gari zetu tunazouza tunazkagua na kuuza gari mbovu kwetu mwiko
Sent from my SM-G935F using
JamiiForums mobile app