Magari ya FORD

Magari ya FORD

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,957
Reaction score
3,245
naomba kujua uzuri wa magari ya FORD

nafahamu ford everest, ford ranger, ford expedition, ford escape, ford explorer.

Je yapo magari used?

Je ni 4WD au 2WD?

kampuni gani iliyopo Dar inauza?
 
Mimi niko USA.

1. Sijui kama kuna kampuni Dar lakini kunaweza kukawa na dealers.
2. Ni vyema kama ungenunua gari USA kwasababu USA unaweza kupata gari kwa bei nafuu. Tofauti ni kwamba gari litakuwa left hand! lakini marafiki zangu wana Toyota pick up left hand bongo wanasema haina shida sana kama watu wanavyofikiria.
3. Ushafirishaji: Usikimbilie kulipia container nzima kwasababu ya gari hivyo tafuta mtu anayetuma container halafu mpe kama $1000 akuwekee gari yako huko. Kama hutaki kufanya hivyo ongea na kampuni za ushafirishaji (uanaweza kuzipata kwenye internet) na waeleze washafirishe gari pekee.
 
CMC Tanzania ndio dealer na agent wa Ford hapa TZ..... also nimeona Kuna ford showroom along Moshi arusha road in Arusha...kama sio USA river basi ni kikatiti... CMC wapo kwenye kona kabisa Azikiwe na Bibi titi
 
naomba kujua uzuri wa magari ya FORD

nafahamu ford everest, ford ranger, ford expedition, ford escape, ford explorer.

Je yapo magari used?

Je ni 4WD au 2WD?

kampuni gani iliyopo Dar inauza?

Rafiki nakushauri usithubutu kununua FORD ukiwa TZ, spare zake hazipatikani kirahisi. Kuna watu huwa wanaziweka gari zao juu ya mawe wakisubiri spare kutoka Nairobi au Marekani.
 
Rafiki nakushauri usithubutu kununua FORD ukiwa TZ, spare zake hazipatikani kirahisi. Kuna watu huwa wanaziweka gari zao juu ya mawe wakisubiri spare kutoka Nairobi au Marekani.

...Inategemea gari lako umelinunua wapi na ni model gani. Everest na ranger zinapatikana kwa wingi Tanzania na vipuri vyake viko vingi pale CMC Automobiles ambao ni wakala wa magari hayo, wapo Azikiwe/Bibi Titi, na jamaa wanatoa huduma nzuri kwa gari lako. Lakini pia wanaweza kukuagizia vipuri iwapo model ya Ford yako ni tofauti na wanazoziuza.
 
Rafiki nakushauri usithubutu kununua FORD ukiwa TZ, spare zake hazipatikani kirahisi. Kuna watu huwa wanaziweka gari zao juu ya mawe wakisubiri spare kutoka Nairobi au Marekani.

Inategemea na yeye mwenyewe tu!..tatizo wabongo tunpenda kwenda kwa "wagonganyundo". Gereji zote za maana huwezi kukosa spea ya gari yoyote! dunia sku hizi ni KIJIJI!
 
Back
Top Bottom