Magari ya Hybrid yanayofanya vizuri Tanzania

Kwanini wasitoe na yale yenye solar panels? Mimi ninachoona ni kwamba Fanya ufanyavyo Dunia nzima kuna watu wachache sana ndio wanufaika wa mwisho haswa kwenye nishati uongozi nk.
Naamini wanaweza kutengeneza magari yenye solar panels na yakawa yanaendeshwa na full umeme. Ila lengo ni kutumikisha watu kuwanyang'anya uhuru mwisho kuendelea kuwatawala.

Ndio hao wanaochichea vita na kupandisha juu bei za nishati. Na vyakula.
 
Wazo zuri sana mkuu, na Makampuni ya magari wameanza kulifanyia kazi mkuu. Ila kuna changamoto kidogo hapo. Nayo ni kwamba, roof ya gari ina eneo dogo sana kutengeneza umeme wa kutosha.

Ni hivi, magari mengi yana roof yenye surface area ya square mita 3 hadi 5 hivi, na kwa technolojia ya sasa, solar panels nyingi zinatengeneza 150 watts kwa square mita moja. Ambayo ni karibia sawa na energy ya kuwasha taa moja ya nyumbani.

kwahiyo economically, wanaona bora waache tu.

Gari kama Prius 3rd generations (2009 hadi leo) zina solar panels ambazo zinaongezea umeme kidogo kwenye battery. Mfano: Prius 2019 zina solar panels ambazo zinaweza kuongeza range ya kilometa 5 hadi 10 ikiwa imewekwa kwenye jua siku nzima. Na iyo option unakuta inauzwa $700

Tatizo una uhakika wa jua kila siku? Je km 10 zinaworth? Wana sacrifise vitu vingi sana ukiweka solar panel kama panoramic roof, sunroof etc.
 
Umewiva sana mkuu. Sina shaka na wewe. Wakati ukiwadia lazima nikutafute unikabidhi chuma yangu.
 
Uzi mzuri kaka vip wanaosema kipind cha mvua gari za hybrid ni hatari kutumia kwa sababu ya umeme mwingi na je vip unapobadili unaweza kupata original kama ilokuja na gari
 
Uzi mzuri kaka vip wanaosema kipind cha mvua gari za hybrid ni hatari kutumia kwa sababu ya umeme mwingi na je vip unapobadili unaweza kupata original kama ilokuja na gari
Kuhusu kipindi cha mvua, nadhani izo ni nadharia tu. Technology za haya magari nadhani kwakua yanatumia battery kubwa lazima walifikiria issue ya maji.

Kubadirisha battery sio issue kama unavyoifikiria. Baadhi ya magari, mfano Toyota, hauna haja y kubadirisha battery zima, unabadirisha cells kadhaa tu.
 
Prius 2010 mkononi. Sijaona shida yoyote zaidi ya kuenjoy wese kiduchu.
 
Mie natumia hybrids tu...nipo na prius mbili...pia kwakua mie ni DIY person....huduma zote nafanya mwenyewe..yaan ninafanya service mwenyewe ya mifumo ya hybrid
 
Mie natumia hybrids tu...nipo na prius mbili...pia kwakua mie ni DIY person....huduma zote nafanya mwenyewe..yaan ninafanya service mwenyewe ya mifumo ya hybrid
Kaka, February najiunga na chama
 
Hond vezel 2016 Hybrid vipi kwa Tanzania
Job kuna mtu anayo ina 6 months. Ni nzuri muonekano na ndani ipo poa.
Sema naona bei yake imesimama ila ningekua fresh ningeichukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…