Magari ya Hybrid yanayofanya vizuri Tanzania

Magari ya Hybrid yanayofanya vizuri Tanzania

Job kuna mtu anayo ina 6 months. Ni nzuri muonekano na ndani ipo poa.
Sema naona bei yake imesimama ila ningekua fresh ningeichukua.
Mkuu hiyo prius 2010 mbona cc 1,700 zake nyingi sana au haina shida ukilinganisha na Aqua ambayo cc1500 ni ipi bora.Alafu nimecheki mtandaoni naona gari zipo mpaka za million 9,10,13,15 ni kwamba magari yameshuka bei au watu bado wana hangover ya kiberiti IST😄
🤝

Ila Aqua nyingi KM zimesonga embu tupo shule maana wabongo tushakariri mambo ya Km sio mchezo.
 
Screenshot_20250120-143958_1.jpg

👆👆👆👆Naona ofa za mwisho wa mwaka ndo hizi bado zipo sana😄😄😄

Wazee acheni kununua viberiti used(IST ) za wabongo namba D ila unaambiwa imetembea 90KM🙌🙌🙌🙌
 
Sikia wenyewe wanakwambiaje kuhusu kumiliki USED HYBRID,,,,"UKITAKA KULA KUBALI KULIWA"
Screenshot_20250120-151937.jpg
 
Magari mengi ya HYBRID betri inakuwa na survival time ya 10yrs au approximate 150,000KM.Mnadani huko magari mengi yanasoma 100,000Km and above hapa kuna kazi ya kubet😄😄😄 Mad Max
Screenshot_20250120-152533.jpg
 
Hao TRA ndio adui wa watanzania kuingiza vitu current kutokana na kodi zao zisizo na tija.

Ni ajabu watu kuwa proud kutumia mitumba iliyokuwa backdated miaka 20+.
Ni sera za chama tawala !

Sa100 mi5 tena!
 
Mkuu hiyo prius 2010 mbona cc 1,700 zake nyingi sana au haina shida ukilinganisha na Aqua ambayo cc1500 ni ipi bora.Alafu nimecheki mtandaoni naona gari zipo mpaka za million 9,10,13,15 ni kwamba magari yameshuka bei au watu bado wana hangover ya kiberiti IST😄
🤝

Ila Aqua nyingi KM zimesonga embu tupo shule maana wabongo tushakariri mambo ya Km sio mchezo.
1. Kuhusu Aqua na Prius, kwanza kumbuka zote ni Prius kasoro Aqua inaitwa Prius C (City). Imenyimwa power kidogo, zote zinatumia hybrid system moja. Hapo chagua muonekano Aqua ni ndogo wakati Prius kubwa. Ila Aqua kwa misele ya mjini itakua more efficient.

Kama unanunua Aqua yenye ushuru mzuri ni 2015 ina Mil 7.5 so ukipata ya Mil 10 SBT/BF unapata cheaper.

2. Magari yameshuka huku kodi zimepanda.

3. Kuhusu kilometa za Hybrid tushawahi ongaelea hii kitu:

Hybrid ya zamani yenye kilometa chache ni ya kuiogopa kuliko hybrid yenye km nyingi. Kwasababu ya vitu viwili:

Moja: Possible wamerudisha nyuma km. Imagine unakuta gari la 2010 hafu km chini ya 100k inamaanisha nn?

Pili: Kama halijarudishwa, hybrid haipendi kukaa inapenda kuendeshwa. Namaanisha kinachoua battery ya hybrid moja wapo ni kukaa muda mrefu bila kurecharge na kudischarge.

Kwahiyo:
Chagua hybrid ya miaka ya karibuni kadri uwezavyo.

Kilometa zisiwe issue sana kwa mfano mimi gari la hybrid lenye 150k ningeagiza bila wasiwasi.

Umri wa kuogopa ni kuanzia miaka 15+ labda maana miaka hii ndio hybrid battery zinakua zimemaliza warranty na life span nyingi zimo humo
 
Magari mengi ya HYBRID betri inakuwa na survival time ya 10yrs au approximate 150,000KM.Mnadani huko magari mengi yanasoma 100,000Km and above hapa kuna kazi ya kubet😄😄😄 Mad Max View attachment 3207388
Sasa mkuu miaka 10 ndio magari yetu aya. Tutaweza kweli aya 2016 kuja juu?

Dah itabidi tukomae na Prius za 2010 kibishi.
 
Mkuu Mad Max kwenye hii Honda Fit na Toyota Aqua ipi unaipa marks nyingi kwenye fuel consumption na gharama ya spare parts na interior size
Bila kujiuliza mara mbili, nitachagua Fit ila Aqua ndio rafiki zaidi kwenye mafuta.

Aqua kwenda 35+ km/L kawaida wakati Fit mostly 28+ km/L

Ila mbali na mafuta, muonekano una matter na vingine mapendeleo binafsi.
 
Sasa mkuu miaka 10 ndio magari yetu aya. Tutaweza kweli aya 2016 kuja juu?

Dah itabidi tukomae na Prius za 2010 kibishi.
PRIUS nimeisearch naona inang'aa kidunia ila ndo hivyo nimezurura kwenye mnada wa BE FORWARD siku ya juzi ila sijaona zenye 60,000Km angalau mengi ya magari ya hybrid ni 100,000km plus.Hii inaonyesha haya magari wenzetu wakiyanunua huwa wanakaa nayo sana🙌🙌🙌🙌.Na hii ni ishara nzuri kuwa ni magari mazuri.

Shida bongo watu wengi WANASOMEA vitu huko vyuoni kwa kufata mkumbo ila ingekuwa watu wanajua hela ilivyo huku kwenye ufundi UMEME WA MAGARI kwa nchi yetu huku ndo utajiri ulipo.Watu wanogopa kuagiza ya magari ya umeme BONGO hakuna MAFUNDI COMPETENT.

Ningekuwa na uwezo ningejisomesha hii fani maana siku za usoni 2030 huko EV ndo habari ya mjini.
 
Bila kujiuliza mara mbili, nitachagua Fit ila Aqua ndio rafiki zaidi kwenye mafuta.

Aqua kwenda 35+ km/L kawaida wakati Fit mostly 28+ km/L

Ila mbali na mafuta, muonekano una matter na vingine mapendeleo binafsi.
Ni kweli, kwa muonekano Aqua ina sura/shape mbaya kishenzi...

Sijui kwa nini gari nzuri vile inakua na bad moulding... Wangeimodoa ikawa shape kama Mazda Verisa (au kama Suzuki Swift) watu wangenunua kishenzi.

Kila napoiona kwa road sitamani hata kuitazama twice.
 
Ni kweli, kwa muonekano Aqua ina sura/shape mbaya kishenzi...

Sijui kwa nini gari nzuri vile inakua na bad moulding... Wangeimodoa ikawa shape kama Mazda Verisa (au kama Suzuki Swift) watu wangenunua kishenzi.

Kila napoiona kwa road sitamani hata kuitazama twice.
Hahaha yaani sijawahi ipeda ule muonekano ila ni moja ya hybrid imara sana kuwahi kutokea.
 
PRIUS nimeisearch naona inang'aa kidunia ila ndo hivyo nimezurura kwenye mnada wa BE FORWARD siku ya juzi ila sijaona zenye 60,000Km angalau mengi ya magari ya hybrid ni 100,000km plus.Hii inaonyesha haya magari wenzetu wakiyanunua huwa wanakaa nayo sana🙌🙌🙌🙌.Na hii ni ishara nzuri kuwa ni magari mazuri.

Shida bongo watu wengi WANASOMEA vitu huko vyuoni kwa kufata mkumbo ila ingekuwa watu wanajua hela ilivyo huku kwenye ufundi UMEME WA MAGARI kwa nchi yetu huku ndo utajiri ulipo.Watu wanogopa kuagiza ya magari ya umeme BONGO hakuna MAFUNDI COMPETENT.

Ningekuwa na uwezo ningejisomesha hii fani maana siku za usoni 2030 huko EV ndo habari ya mjini.
Vyuoni mfano NIT na VETA, DIT ndio wangeanza kuboresha mtaala wa hivi vitu.
 
Vyuoni mfano NIT na VETA, DIT ndio wangeanza kuboresha mtaala wa hivi vitu.
Nchi hii WASOMI WA MCHONGO hawana kitu zaidi ya kunyemelea TEUZI😬😬😬

Shangaa BY 2035 NI SERA YA KIDUNIA HAMNA KUBEMBELEZANA BY THAT TIME.KILA NCHI INATAKIWA IWE IMEHAMIA KWENYE MAGARI YA EV ILA LEO 2025 NCHI ZA AFRICA BADO ZIMELALA USINGIZI MZITO😁😁😁.

IKIFIKA 2032 NDO WANAKURUPUKA WANAANZA KUTOA CERTIFICATE IN EV MECHANICS AND TECHNOLOGY😂😂😂

KUFIKIA 2027 MITUMBA YA EV ITAKUWA IMEANZA KUNOGA KATIKA BARABARA ZA BONGO.HAPO TECHNICIAN KUTOKA CHINA WATAJICHUKULIA TENA HELA NA AJIRA ZA BURE KAMA WALE WACHINA KATIKA GAURAGE ZA TABATA WANAVYOJICHUKULIA HELA KIULAINI.

MAFUNDI MAIKO NA GAURAGE ZAO ZA CHINI YA MTI WATAKUFA NA NJAA HUKO MBELE YA SAFARI.
 
Huku bei ya mafuta ikiendelea kupanda kila kukicha ndani ya hii miaka mitano (kutoka Tsh 2100/= hadi sasa Tsh 3300/=) na hamna "dalili" kuona bei ikishuka, ni muda wa Watumiaji kubadirisha muelekeo (adaptation). Kwa wanaotafuta gari, ni bora kuangalia "Fuel Efficient cars" au "Hybrid cars" huku tunasubiria "Electrical Vehicles" miaka miwili ijayo.

Tukumbushane tu kua, Hybrid cars, kama wadau kwenye nyuzi zilizopita walivyowahi kusema, inakuja na battery mbili. Moja ni ile ya kawaida (12 Volts battery) inayofanya kazi ya "kupower" gari na kuwasha. Na ya pili ndio "high Voltage hybrid" battery inayotumika kumsaidia engine au kumreplace engine kusukuma gari.

Kwahiyo kuna scenario mbili hapa: (1) Kuna muda gari inaendeshwa na hii hybrid battery tu. Kwahiyo engine haifanyi kazi kabisa. Na mafuta hayatumiki kabisa. (2) Kuna muda engine na battery ya hybrid vinasaidiana. Kwahiyo gari inakua efficient sana. By sana namaanisha sana.

Kwahiyo, lengo kuu la kununua hybrid cars ni kusave mafuta. Na ndio maana tunashauri anunue mtu anaekaa mji wenye msongamano (trafic jam), we anaeendesha sana gari kwa siku au mwaka gari yake na mwisho angalau akae nayo iyo gari kwa miaka 3 kwenda mbele ndio ataona faida. Wale wazee wa kila miezi 6 kubadirisha gari hii kwake itakua haina "faida".

Ebu tujuzane magari ya Hybrid yanayofanya vizuri au tunayoshauri mtu wa kipato cha kati anunue.

1. Toyota Prius
Wenyewe wanasema huyu ndio king wa Hybrids. Prius ana generations tano (5) hadi sasa hivi. Tuipata 2nd generation sio mbaya ila 3rd generation ni nzuri pia.

Hii hapa ni 2nd generation 2003 hadi 2008. Unaweza kuipata jumla (CIF na ushuru) kwa chini ya mil 15.
View attachment 2967020

Hii hapa ni 3rd generation, mwaka 2009 hadi 2013 unaweza kuipata kwa angalau Mil 19 na kuendelea kutoka Japan.
Hii gari ishawahi pata tuzo nyingi sana. Highly recommended.
View attachment 2967021

Combined Fuel economy ya Prius inafika 25 km/L na ukiwa dereva mzuri inaweza kufika ata 30 km/L au zaidi.


2. Toyota Aqua (aka Prius C, C for City!)

Huyu ni mdogo wake Prius aliekua designed kwaajili ya kuendeshwa mjini. Kidogo ni mdogo, mwepesi na ana fuel economy kubwa zaidi.

View attachment 2967030

Ana generations mbili, ila tunatumia zaidi ya kwanza 2011 hadi 2020 maana hii ya pili inaanza 2022 tuassume ipo nje ya budget yetu.
Huyu ndio kipenzi cha Uber na Bolt drivers kwa sasa kwakua anaweza kwenda hadi 38 km/L hapa mjini.

3. Honda Insight
Honda nae havumi lakini yupo. Anachuma zake Hybrid kadhaa ila Honda Insight ni moja ya hybrid insyofanya vizuri.

Huyu ana generations tatu (3) hadi sasa. Ya kwanza ya mwaka 1999 ilikua ya kiwaki sana shape yake. Sijui madogo wa field ndio walikuja na Ile idea?

View attachment 2967031
Ila kuna wabishi walinunua. Aisee.

Ila second generation ya 2009 hadi 2016 ipo poa na Bongo zipo za kutosha. Inafanana sana na Prius hadi wengine wanasema kuna mtu aliuza ramani. Sasa hatujui nani kwasababu almost zote zimetoka mwaka mmoja (Honda Insight 2nd gen 2009 na Prius 3rd gen 2009).

View attachment 2967032

Hii Insight ukitulia Beforward unaweza ipata kwa Mil 15 na mafuta haipishani sana na Prius. Ukichagua yoyote utaenjoy.

4. Honda Fit Hybrid na Honda Fit Shuttle Hybrid
Honda alifanya unyama kutuletea kagari kadogo kama IST flani akakaita Honda Fit. Best selling compact car kutoka kwa Honda. Kwa kuona haitoshi akaamua kukapa Hybrid. Aisee kama unatafuta gari dogo ambalo linanusa wese mara mbili ya IST basi ishi na Honda Fit Hybrid.
Hapa kuna generations nne (4) hadi tunavoandika huu uzi. Ila tuachane na 1st generation ni ya zamani sana na tuachane na 4th generation, bei sana. Tuishi na 2nd generation na 3rd generation.
Hii ni 2nd generation 2007 hadi 2012. Ukitaka Hybrid yake ipo, ukitaka isio Hybrid ipo, ukitaka Sports Edition (RS) ipo. Shindwa wewe.
View attachment 2967036
Hii unaweza ukapata kutoka Japan kwa chini ata ya Mil 14 ukifanya uchunguzi vizuri.

Hapa tuna Fit Hybrid 3rd generation kuanzia 2014 hadi 2020 aisee. Imeboreshwa muonekano, engine na ndani ina unyama sana.
View attachment 2967037
Honda Fit ina consumption ndogo pia inaweza kwenda hadi 30km/L hapo mjini town.

Pia, Honda alikuja na Honda Fit Shuttle ambayo ni "kubwa" ya Fit ya kawaida. Kilichobadirika ni shape tu. Hii kwa lugha ya wataalamu wanasema ni station wagon shape ya Honda Fit.

View attachment 2967040
Kwahiyo kama unapenda Fit ila haujapenda size yake, twende na Hii. Ingawa utasacrifice fuel economy kidogo kwasababu hii ni kubwa (heavy).

5. Harrier Hybrid
Harrier ina generations nne (4) hadi leo. Ila Hybrid engine walianza kutengeza kwenye 2nd generation (2003 hadi 2013). Hii almaarufu tako la nyani (usishangae logo ya Lexus, picha tu ila same car)
View attachment 2967041
Kama uchumi sio tatizo unaweza kwenda na 3rd generation kuanzia 2014. Mchawi pesa ila hii chuma kali kifala.

View attachment 2967042
Kidogo bei za Harrier sio rafiki kwasababu 2nd gen chini ya Mil 35 haupati na 3rd gen bila Mil 70 hauchomoi. Ila tuneona tuiweke kwa maboss.

Tufanye hesabu kidogo:
1. Tufanye Mshana amenunua IST inatumia mafuta 15 km/L na Bwana PureView Zeiss kanunua Toyota Aqua inayoenda 35 km/L na wote wanedesha 40 km kila siku kwenda na kurudi kazini.

2. Mshana kwa siku anatumia Lita 2.5 kwa bei ya leo ya Tsh 3300/= anatumia Tsh average ya Tsh 9,000/= kwa siku.
Kama anaendesha kila siku 365 za mwaka atatumia Tsh 3,285,000/= kwenye mafuta.
Tuassume amekaa na gari miaka mitano, kwahiyo tuzidishe na tano tunapata Mil 16.5 za mafuta.

3. PureView Zeiss yeye kwa siku anatumia Lita 1.2 za mafuta ambazo ni kama Tsh 4,000/= tu.
Kwa mwaka (siku 365) ni kama Tsh 1,460,000/= tu.
Nae amekaa na kiberiti chake kwa miaka mitano, tukizidisha tunapata Mil 7.3 tu.

4. Najua hesabu za ivo ni za motivation speakers ila my point kuonesha kwamba Hybrid inaweza save nusu ya gharama kwenye mafuta.

NB:
1. Bei nilizoandika ni estimation. Zitabadirika kutegemea na hali ya gari na kikokotoo cha TRA.
2. Fuel consumption nilizoandika nj estimation za mitandaoni. Zinaweza kupanda zaidi au kushuka kutegemea na mtumiaji.
3. Hybrids zina perfom vizuri kwenye low speed na mjini kuliko highway.
4. Hybrids nyingi zina options tatu. Eco, EV na Sport. Kama unaweka Eco muda wote tegemea ulaji mzuri wa wese kuliko anaeweka Sport.
5. Kama ilivyo battery ya simu yako, pia battery ya Hybrid inakufa (degradation) kutokana na muda na matumizi.
6. Unavyotafuta hybrid car online. Kilometa za kwenye odometer zisikudanganye. Usiangalie namba ndogo. Hii topic ya siku nyingine.

Nimeona tuziweke izo gari tano (5) ingawa hybrids siku hizi zipo nyingi sana kwahiyo kila mtu anaweza kuja na list yake. Natumai wachangiaji wataongeza hybrids pendwa zingine na wengine wataongezea nyama kwenye izo tulizodiscuss.

Karibuni
Wenzetu wa Hybrid service mnafanyia wapi? Ili na sie tununue. Lasivyo mafundi nyundo wetu hawa....
 
Back
Top Bottom