ksny
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 1,704
- 1,694
Gari yangu ya kwanza ilikuwa Nissan Sunny (1984) ambapo ndiyo zilitoka kwa jina hilo la Nissan, kabla ya hapo zilikuwa zinautwa Datsun. Mpaka leo kila nikibadilisha gari nanunua Nissan. Sasa nhivi ninayo Nissan Pathfinder. Nissan zote nilizowahi kutumia hazijanipa matatizo yoyote. Magari mengi kikubwa ni service. Kwa upande wa spare parts, inaweza kuwa sida kuzipata kwa sababu Nissan siyo mengi TZ kama Toyota. Kuhusu "original or genuine spares" yhii ni kazi kubwa. Sasa hivi magari mengi yawe ya USA, Japan au Ulaya karibu 50% au zaidi yana parts zilizotengenezwa China. Katika nchi zingine kuna kitu wanaita "after market parts" hizo ni spare zilizotengenezwa na kamuni yoyote kwa niaba au ruhusa ya Nissan. Spare kama hizo haziandikwi Nissan au genuine Nissan parts lakini zinatumika pasipo tatizo. Ila inawezekana zipo parts sensitive ambazo unaweza hazitegenezwi na third party. Lakini nijuavyo wanawapa third party kutengeza parts.Wapendwa wenye uzoefu wa magari naomba mnijuze magari ya Nissan yana tatizo gani...nimekuwa nikiambiwa nisijaribu kununua gari ya Nissan lolote kwani litanisumbua ninunue tu kampuni ya Toyota.sijajua tatizo ni nini..
Mimi kuna gari la Nissan Primera nalipenda na ninatamani kulinunua ila nimeambiwa magari yote ya Nissani kipengele,nimewauliza hao wanaosema hivyo kama wamewahi kumiliki Nissan wanasema na wao waliambiwa hivyo..so nimeona nisije nikaacha kitu cha maana kwa ajili ya maneno ya kuambiwa..
Maana akili za kuambiwa,changanya na zako[emoji16]
Sent from my SM-C5000 using JamiiForums mobile app