Magari ya Nissan

Gari yangu ya kwanza ilikuwa Nissan Sunny (1984) ambapo ndiyo zilitoka kwa jina hilo la Nissan, kabla ya hapo zilikuwa zinautwa Datsun. Mpaka leo kila nikibadilisha gari nanunua Nissan. Sasa nhivi ninayo Nissan Pathfinder. Nissan zote nilizowahi kutumia hazijanipa matatizo yoyote. Magari mengi kikubwa ni service. Kwa upande wa spare parts, inaweza kuwa sida kuzipata kwa sababu Nissan siyo mengi TZ kama Toyota. Kuhusu "original or genuine spares" yhii ni kazi kubwa. Sasa hivi magari mengi yawe ya USA, Japan au Ulaya karibu 50% au zaidi yana parts zilizotengenezwa China. Katika nchi zingine kuna kitu wanaita "after market parts" hizo ni spare zilizotengenezwa na kamuni yoyote kwa niaba au ruhusa ya Nissan. Spare kama hizo haziandikwi Nissan au genuine Nissan parts lakini zinatumika pasipo tatizo. Ila inawezekana zipo parts sensitive ambazo unaweza hazitegenezwi na third party. Lakini nijuavyo wanawapa third party kutengeza parts.
 

Unanikumbusha Nissan sunny (station wagon), manual ndo nilijifunzia kuendesha miaka ya 90. Kaliuzwa kale kagari kakiwa kazima. Spare zilikuwa ghali kidogo ukikinganisha na Toyota. Nikaendeaha sana Nissan terrano ya diesel miaka ya 2000 mwanzoni (comfortable na imara), spare hazikuwa rahisi kama toyota ila zinamithilika na hununui kila siku. Now, nina experience na Nissan patrol TD42 (non turbo), inatulia barabarani, ngumu.
Nissan xtrail 1st generation sidhani kama zilikuwa nzuri sana, nadhani zilijuwa na issue ya head yake au kitu kama hicho, ila zilizofuata sidhani kama zina issue. Patrol ZD30 pia zina issue kidogo ya overboosting ya turbo ila kuna tiba zake na namna ya kuihudumia vizuri. Vinginevyo sidhani kama kwa ujumla wake Nissan zina shida. Tena naona kama ni imara sana hasa miguu, stability na handling.
Spare kweli ni ghali kidogo na nashauri ununue duka ambalo unajua kweli unauziwa genuine. Ukifunga unasahau
 
Naomba unisaidie naitamani sana pathfinder ,naomba maelekezo hasa ya kuzingatia
 
tatizo la magari ya Nissan pekee ni pale utakapotaka kuliuza ili ununue jingine, unaweza uza gari nzima kabiss kwa milioni 1
 
Jamani naombeni kujua pia kuhusu NISSAN DUALIS jamani maana hii gari naipenda mpaka naumwa
 
Na hapo ndipo tatizo kubwa la kumiliki Nissan lilipo...wauzaji wanakuuzia spea feki kwa bei ya original
 
mkuu kuna gari ambalo halina roof kweli?? labda wataalam watusaidie
unaposema roof si unamaanisha kile kioo cha juu kinacho funguka, kama ni iko kuna magari ya dualis baadhi hayana
 
unaposema roof si unamaanisha kile kioo cha juu kinacho funguka, kama ni iko kuna magari ya dualis baadhi hayana
Hapana tunamaanisha vile vitambaa kwenye roof hata milangoni huwa vinabanduka....

Sijui nitumie lugha gani kiutaalamu
 
kwaiyo mwanangu unanishauri nini mkuu, ebu niambie
Go on... Ukipata gari nzuri hivyo vitambaa sio shida mafundi kibao. Na by the way huwa vinaanza kuchoka baada ya miaka kuanzia 12-15 toka lianze kutumika...

Sio ishu kama umependa gari nunua. Jali ishu nyingine za muhimu.
 
Vp kuhusu Nissan Patrol Y61 Td42 , ukilinganisha na Land Cruiser let’s say 100 or 105 series diesel
 
Vp kuhusu Nissan Patrol Y61 Td42 , ukilinganisha na Land Cruiser let’s say 100 or 105 series diesel
Sina uzoefu sana na LC ila naamini unamaanisha engine za diesel, 1HZ, au nyingine zinakuwa na 1HDT. Zote ni gari nzuri, Kwenye LC, TOYOTA alitulia sana kutengeneza gari imara na amefanya maboresho kwenye kila toleo including 100 series. Hapa itategemea sana na preference yako. Ila binafsi napenda Nissan inavyotulia barabarani na handling kwa ujumla.
TD42 ipo ya turbo na isiyo na turbo, zote ni nzuri sana, ofcoz isiyo na turbo kawaida itakuwa na maisha kidogo kuliko ya turbo esp kama service za engine hizo zikiwa za kusuasua.
1HZ, 1HD, 1HDT nazo ni engine nzuri sana, story ya turbo vs non-turbo engines ni ile ile tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…