Nataona kama itafika itafika kwetu mwisho wa reli ngoja itengenezwe pengine wabongo wasihusike mpaka mlinziHalafu huu msemo WATU HATUNA HELA alaaniwe alieuleta/anzisha!..
Toyota wakileta kiwanda hawataangalia watz million 40 kununua wanaangalia ukanda wa afrika mashariki na kati. Huna hela nunua baiskeli huna hela panda daladala!..
By the way gari zitakua bei cheap zikitengenezwa hapa hapa!..Usinambie bei ya azam cola Tz ni sawa na Congo/malawi.
INAKERA!..
Umewahi kufuatilia ni kwanini tunanunua used kwa bei juu sana na baadhi ya hayo malori na mabasi mapya baadhi wana mudu!Sijasoma m bango wote huo, kichwa cha habari chajitosheleza kwa kifupi hakuna kiwanda cha magari kitakachotufaa. Mostly watanzania hatuna uwezo wa kununua gari jipya, sisi tunaweza kununua used tu. Scania walikuwa wana assemble pale Tamco Kibaha, pamoja na tractor za Valmet, ila kutokana na bei wakafunga kiwanda, matajiri wengi wa maroli wananunua used rollies.
ni afadhali waje wahindi au wachina angalau tunaweza kununua magari yao ya Tata au Jiefang, angalau bei zake ni affordable.
Lakini Toyota Mh, itanunua serikali na wakina Bahresa...
Kwani umeambiwa yatatengenezwa special kwa Tz tu? Khaaaa wa Tz noma sana...umesahau kuwa kuna nchi jirani zitakuja kununua hizo gari hapa TZ?TBL inakufa kwa kukosa wateja, Toyota wataweza kweli kufanya biashara kwenye nchi ambayo purchasing power iko very low?
. Anapinga utafikiri kiwanda kinajengwa na serikali. Huyu mtu wa ajabu sana anapingaje mjapani binafsi anayejenga kiwanda kwa pesa zake asije?. Pesa ni yake. Huu uchambuzi wake ni uchambuzi koko. Unazuiaje mtu mwekezaji binafsi asije?Swali zuri. Maana jamaa kasema ni tetesi halafu akashusha povu utafikiri ana uhakika.