Magari ya Wagonjwa bila kuchangia hupati huduma

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Tuanaweza vipi kuafford? Unaambia utoe lita 180 ili mgonjwa wako afike hospitali ya rufaa?

Hili la kwenye matenga ulichomoa kwa kug'aka huko Tunduru.

Lakini ukweli ni kuwa hili ni tatizo sugu. Magari ya Wagonjwa bila kuchangia hupati huduma. Sijui labda kwa unakaa mjini Dar.

Ila mimi najua huwa tunaambiwa kuchangia mafuta kulingana na umbali mgonjwa anapelekwa. Nyie mliosahau haya mambo endeleeni kula bata.
 
Lakini ukweli ni kuwa hili ni tatizo sugu. Magari ya Wagonjwa bila kuchangia hupati huduma. Sijui labda kwa kuwa wewe unakaa mjini Dar.

Ila mimi najua huwa tunaambiwa kuchangia mafuta kulingana na umbali mgonjwa anapelekwa. Nyie mliosahau haya mambo endeleeni kula bata.
Eeh, wanakanusha wakiwa Dar , ila ukweli ndio usemwao huku mikoani !
 
Hakuna vya Bure. Hospitali Haina bajeti ya kila mgonjwa kupelekwa rufaa sehemu nyingine. Isipokuwa na mafuta ni jukumu lako kuchangia mafuta
 
Waingize kwenye gharama ya bima tu kama hosp zinapewa magari ila hakuna bajeti.

Ila mkurugenzi na gar zake nyingine mafuta yapo tena hadi wanaiba. Hakuna anayetaka ugonjwa kwa hiyo nashauri halmashaur zihakikishe mafuta hayakosekani kwa gari za wagonjwa.
 
Tuanaweza vipi kuafford? Unaambia utoe lita 180 ili mgonjwa wako afike hospitali ya rufaa?

Hili la kwenye matenga ulichomoa kwa kug'aka huko Tunduru.

Lakini ukweli ni kuwa hili ni tatizo sugu. Magari ya Wagonjwa bila kuchangia hupati huduma. Sijui labda kwa unakaa mjini Dar.

Ila mimi najua huwa tunaambiwa kuchangia mafuta kulingana na umbali mgonjwa anapelekwa. Nyie mliosahau haya mambo endeleeni kula bata.
Hata ya polisi unachangia kama unaenda kumkamata mtuhumiwa.

Ndo bongo hii.
 
Afya ya watanzania ni biashara,wamenunua vifaa na kujenga mahoptali sio kuhudumia wananchi bali kufanyia Biashara au maonesho ya kufanikisha kukaa madarakani kwa baaadhi ya viongozi.
Unakutana na Jango zuri huku wakijinasibu kununua vifaa tiba, lakinini nanda pale ukaone huduma, ni vituko.
 
Mikoani ni kawaida kuchangia gari la wagonjwa la sivyo mgonjwa wako atakata moto unamuona.
 
Huduma za afya zimekuwa mbovu sana,haiwezekana mialka 63 ya. Uhuru Bado raia tunatibiwa kama watu wa mwaka 1700.
Kama huna pesa usiende hospital utapoteza muda na ikiwezekana utafariki Dunia.Yaliyomtokea Mariamu Zahoro kwa kukosa tsh 150,000 uhai wake iliondoka huku akiagana na mama yake Bi Fatima.

Gari la wagonjwa imekuwa bidhaa ya Anasa kwa watanzania maskini ,mtu yupo radhi asafirishe mgonjwa wake kwa baiskel.
Serikali iliyokaa miaka 63 inaona ni fahari kuwatoza hata wanafunzi wanaokwenda kuanza masomo yao kwa kuwachaji fedha ya vipimo.
 
Tuanaweza vipi kuafford? Unaambia utoe lita 180 ili mgonjwa wako afike hospitali ya rufaa?

Hili la kwenye matenga ulichomoa kwa kug'aka huko Tunduru.

Lakini ukweli ni kuwa hili ni tatizo sugu. Magari ya Wagonjwa bila kuchangia hupati huduma. Sijui labda kwa unakaa mjini Dar.

Ila mimi najua huwa tunaambiwa kuchangia mafuta kulingana na umbali mgonjwa anapelekwa. Nyie mliosahau haya mambo endeleeni kula bata.
Halafu unakuta gari binafsi za watumishi wa umma zinatumia mafuta ya serikali. Jambo jingine ni matumizi ya ovyo sana ya mafuta. Unakuta gari ya Waziri, judge, na wengine imepaki ikimsubiri boss amalize kikao kutwa nzima inaunguruma. Unakuja kushangaa wanapongezana kwa ubadhirifu huu.
 
Mambo mengi yako ovyo sema mapambio ni mengi ndo maana watu wamekaa kimya wanajipambania wenyewe kimya kimya.Hizo gari ziwekwe wazi kua nizakukodi ili watu wajue chakufanya.
 
Eeh, wanakanusha wakiwa Dar , ila ukweli ndio usemwao huku mikoani !
Kutoka hospitali ya rufaa Morogoro kwenda Muhimbili wagonjwa walikuwa watatu, kila mmoja aliambiwa 450K, waliobargain waliishia 400K, huna kapandishe mgonjwa kwenye bus.
 
Unataka ulipiwe na nani hayo mafuta?? Cc Kiranga
Wenzetu kodi zao zinalipia yote hayo, hapa kodi pamoja na tozo kibao ila ukipata janga utajipambania mwenyewe. Polisi anakwambia toa 30K kumfuata mtuhumiwa kilometa 5 tu tena kwa gari yake binafsi. Kujaziwa maelezo polisi unaenda kutoa kopi mwenyewe. Mtuhumiwa anahitaji kuwataarifu ndugu zake kuwa kakamatwa anaambiwa toa 5K ya vocha. Nchi ngumu kweli kweli kwa wenye nchi
 
SAMIA aliwaambia jana kuwa walipa kodi hapa Tanzania ni watu mil 2 tu kati ya watu mil 60..Maana yake wale ambao hawalipi kodi wanawanyonya hao wanao lipa kodi..na mbaya zaidi tunazidi kuzaliana
 
Tuanaweza vipi kuafford? Unaambia utoe lita 180 ili mgonjwa wako afike hospitali ya rufaa?

Hili la kwenye matenga ulichomoa kwa kug'aka huko Tunduru.

Lakini ukweli ni kuwa hili ni tatizo sugu. Magari ya Wagonjwa bila kuchangia hupati huduma. Sijui labda kwa unakaa mjini Dar.

Ila mimi najua huwa tunaambiwa kuchangia mafuta kulingana na umbali mgonjwa anapelekwa. Nyie mliosahau haya mambo endeleeni kula bata.
ndugu,
hospitali ni biashara ya serikali sio huduma ya jamii
kwenda kuchuma mwarobaini kwa jirani au chroloqin ndio ilikua huduma ya jamii
zamani huko kijijini mgonjwa alibebwa juu ya kitanda cha mianzi hadi hospitali michango ilitolewa na wanajamii.

wanasiasa pepo wataisikia tu, wataingia jehanam kinguchiro nguchiro.
 
SAMIA aliwaambia jana kuwa walipa kodi hapa Tanzania ni watu mil 2 tu kati ya watu mil 60..Maana yake wale ambao hawalipi kodi wanawanyonya hao wanao lipa kodi..na mbaya zaidi tunazidi kuzaliana
Hizo ni porojo tu, inawezekana wanaolipa kodi direct wakawa wachache. Ila tozo na indirect tax ni kubwa na mzigo mkubwa sana kwa wananchi. Alafu yeye mwenyewe na wanasiasa wenzake hawalipi kodi, anamlalamikia nani sasa. Matumizi yenyewe ya hizo kodi yanakatisha tamaa.
 
Back
Top Bottom