Magari yamegongana Iwambi Mbalizi Mbeya, moja imewaka moto

Magari yamegongana Iwambi Mbalizi Mbeya, moja imewaka moto

Afisa Mteule Drj 2

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Posts
3,865
Reaction score
4,506
Hiki kilima kikali au tuseme mteremko mkali wa Iwambi Mbalizi Mbeya umeshindikana kwa ajali,huwa muda mrefu haupiti bila ajali kutokea.

Leo imetokea ajali tena na Lori lililobeba shaba bila shaka kutoka zambia,limeteketea kwa moto baada ya kugongana na gari lingine.

Foleni iliyopo leo haijawahi kutokea tunduma Road yote imejaa malori nahisi km kama 10 na zaidi zimetwaliwa na foleni.

Huu mlima walokole wameenda sana kupiga maombi na hata machifu wanaendaga lakini hamna mabadiliko.
Screenshot_20210910-003647.png
 
Serikali ni kama haichukui hatua ninachokiona pale ile sehemu ni dangerous road sidhani kama eti ni lango la kuzimu kama wanavyoaminishana
 
Siamini Kama ni kweli,sirikali imeshindwa kupata suluhisho la kudumu la mteremko Iwambi au mlima MBALIZI,
Tumepoteza watu wengi Sana hapa Kwa ajali,Toka nipo primary nasikiaga vifo tuu yaani imefika mahala nikisikia mtu anaenda MBALIZI mwili unanisisimka.
 
Wale wachina waliopo mtaa wa MarryPrisca waliweka kambi kwa ajili ya ujenzi wa njia ya Mbalizi seminary mpaka Iyunga kwa kiwango cha lami lengo ikiwa ni gari ndogo na za abiria ziwe na njia yake hiyo kazi sijui ni kwa nini haijaanza mpaka sasa, wanasubiri yatokee yaliyotokea 2012 hapo mlimani? Pale mlimani hapahitaji ma chief wala waganga wala ile sehemu ya kusubiri iliyojengwa mwisho wa waya mpaka kwa esta, pale panahitaji upanuzi wa barabara kama siyo kuupunguza mlima au kujenga barabara ya seminary mpaka Iyunga. Anyway wataalamu wanajua zaidi ila sisi boda boda tumepiga faida leo maana gari zote za Mbalizi zimeshushia abiria Jb baada ya tukio.
 
Nilidhani Mbeya Ni bonge ya city kumbe kumejaa vibanda vya mama ntilie.
Hathi ya Mbeya Ni Kama Chato tu.
 
Nilidhani Mbeya Ni bonge ya city kumbe kumejaa vibanda vya mama ntilie.
Hathi ya Mbeya Ni Kama Chato tu.
Sasa hapo ni sehemu ya hamashauriya wilaya ya Mbeya (Mbeya vijijini) na sio Mbeya city council. Mbona Dar kuna maeneo nyumba hazitamaniki? milango ya vyoo ni magunia, choo hakina paa, mvua zikinyesha mnaokota kambale chini ya uvungu, huku mkipishana na misafara ya vinyesi vichochoroni.
 
Dah! Yaani barabara wenzetu wanapeleka wahandisi na maskaveta sisi tunapeleka walokole na machifu, really?

Labda useme ni jokes
 
Sasa hapo ni sehemu ya hamashauriya wilaya ya Mbeya (Mbeya vijijini) na sio Mbeya city council. Mbona Dar kuna maeneo nyumba hazitamaniki? milango ya vyoo ni magunia, choo hakina paa, mvua zikinyesha mnaokota kambale chini ya uvungu, huku mkipishana na misafara ya vinyesi vichochoroni.
Mwambie huyu jamaa.
Tena hayo unayosema wala hayapo mbali nenda mikocheni hata kinondoni.
 
Back
Top Bottom