KUKUZA UCHUMI AMA KUZIGEUZA KONSTRAKTI ZA UCHUMI
Tekinolojia ya Umeme kutoka NUkta Sifuri,
Uvumbuzi wa kama akina Chikumbutsu, unaweka watu wote wa Intelijensia na mikakati dawatini na kuchora kila kitu upya--kama walikuwa hawajajiandaa katika nchi-dola zao...
Anayekuwa na kule ku-JUA vema kuhusu mapelekeo ya haya ya kinishati, nishati nukta sifuri na uvunaji wa nishati mbadala nyingine,
basi yeye ndiye anaweza kuwa na mitigati za kutikiswa kwa statusi kwou.
Kiukweli khasa wa mambo, mavumbuzi haya siyo mapya...
Nchi zote kubwa wanasehemu ya miradi yao ya uwani, mambo ya Tafiti&Maendelesho, ambavyo kila namna ya suluhu tayari zipo hapa Duniani...
Tekinolojia na UJAZI ndiyo sasa zinapata kibali kuvujishwa kwa mapana ya jamii na stawi; lakini hili linafungamana na hitaji la
kuchochea mageuzi ya kimifumo ya maisha na uwajibikaji sahihi wa kiraia.
Kwa sehemu kubwa, hili linakwenda kuhitaji
umma wenyewe ujitetee kwa kubadilisha 'fikra na mawazo yao' kuhusu mifumo mushkeli ambayo imekuwa inawatawala na bado ingali kuwatawala hata sasa.
Kitu vingi katika maisha haviko sawa, japo wanajamii wamepumbuzika na basi kuviona ni sawa--kuishia kuishi kwa shida na raha kana vile ni 'Mapenzi ya Mungu'... Mojawapo ni
mifumo ya fedha, uzalishaji mali na umiliki wa mali...
Hili linakwenda kubadilika sana ndani ya miaka 25 ijayo...
Kiufundi hili linatukumbusha, muda umewadia
wakufikiria maisha 'kitekinokrasia na meritokrasia' badala ya politiki/siasa; mambo ya siasa za hadaa kati ya mambo ya watawala na watawaliwa...
Hii ina maana, yeyote anayependa na kutaka
kusafiria 'Nyota za Wengine' kwa ujasiria-mifumo, mifumo ya watu waliojaa kwenye mifumo ya kujiziuka/kujitoa ufahamu/kujizima data, ana kibarua kigumu cha changamoto ya mabadiliko ya tabia, akili, fahamu na utambuzi katika wanajamii--changamoto inayokwenda kuwa 'dhahiri na dhahiri zaidi' ndani ya miaka hii 25 ijayo kote duniani...
Unapofikiria kuhusu
NIshati na Uchumi kwenye mwelekeo wa jami iliyo na ule UJAZI wa mbinu za kazi na utendaji basi ndiyo likukumbushe 'fedha' na 'mali' vinakwenda kuchukua 'uthamani tofauti'... Tunakokwenda, mambo ya fedha, majumba na mali yanakwenda kuwa 'vitu vya kawaida' sana... Si mambo ya 'fimbo/bakora ya kuchapia' wengine--mambo ya
malingishiano na 'kutengeneza sifa' mbele za wengine...
Kwa hivyo tunaelekea aina ya uchumi tutakaouita ni '
UCHUMI MAMA'...
UCHUMI MAMA, ni namna uchumi usifanania na 'Mifumo Dume'... Uchumi wa sasa ni utundu wa kimifumo dume kupitia '
Fedha na Mifumo Mushkeli ya Utaratibu wa Mikopo, Riba na Uhuni wake'...
Hili litukumbushe sote, Uchumi Mama unasubiri tu Umma wenyewe Ujielewe na Kujitambua; siyo mambo ya
kusubiri walio madarakani wazibadilishe sera na sheria eti ili kuyaleta 'mabadiliko'...
Popote pale ambapo wanajamii wanaweka
'imani kubwa kwa watawala', imani ya upofu wa kudhamiria/Unafiki ama kutodhamiria, na tena pasipo uwajibikaji sahihi wa kiraia basi hao watachelewa kujinasua na mifumo mibovu ya maisha na tawala hapa Duniani...
Wanajamii wanaouwezo kamili wa
kukataa mifumo isiyowafaa ya fedha, mali na uzalishaji mali; na katika hili wao si watu wakusubiri fadhila za waliopo madarakani ama vinara wa njia kuu za uchumi wa kileo, tuseme 2025.... Basi ndiyo yawa,
wao wenyewe inawapasa waoneshe njia ya kujikwamua na adha mbaya za uchumi wa kileo kwa kujipanga kitaasisi mpya za maendeleo ya Jamii zao...
Nishati nukta sifuri, nje ya kudhani ni jambo ya manufaa ya kiuchumi kichoyo, ni jambo linalotutaka kufikiria upya kuhusu utendaji na shughuli zenye kulenga moja kwa moja ujenzi wa jamii ya kijamaa na kujitegemea... Kiufundi,
maarifa ya kazi na kujitosheleza katika uhitaji wetu wa kila siku ndilo shauri tunaloliendea...
Haya mambo yanataka akili, utambuzi na mafahamu ya wanajamii wote yaanze kuchangamka...
Hakuna shule yoyote hata sasa ulimwenguni iliyowandaa kikamilifu wanajamii na
mageuzi haya makubwa Duniani yanayokuja kwa NIshati Nukta Sifuri na Matumizi ya Akili Bandia...
Kujiongeza ni lazima...
Hmmm