Magazeti ya Kenya yanahaha: Tanzania and Uganda under UN probe over N. Korea trade ties

Mbona hakuna fair ground kati ya NK na US linapokuja swala la kufanya majaribio ya silaha?
 
Magazeti ya Kenya yanahaha vipi wakati ni kweli kabisa UN inaichunguza Tanzania juu ya madai ya kununua silaha za vita kutoka North Korea??
kwani ni ajabu kununua silaha mbona tulikua tunanunua hapo mwanzo??kinachochunguzwa sio kununua silaha kinachochunguzwa na ukiukwaji wa Sheria katika ununuzi huo,na wala si mara ya kwanza Tanzania kununua silaha kwa hao watu.
 
Mbona hakuna fair ground kati ya NK na US linapokuja swala la kufanya majaribio ya silaha?
Nikumbushe ni lini Marekani au Urusi, au China, au nchi nyingine yoyote ile kati ya nchi zinazomiliki silaha za nyuklia ilifanya jaribio lolote la nyuklia tangu umoja wa mataifa ulipopiga marufuku utengenezaji na kufanya majaribio ya kinyuklia?

Kwa taarifa tu, baada ya vita kuu ya pili kumalizika na UNO kuundwa, kulipitishwa azimio la kutotengeneza wala kufanya majaribio ya silaha hizo kwa nchi yoyote ile, ndiyo maana nchi yoyote inayokiuka azimio hilo inawekwa chini ya vikwazo. Ila azimio hilo halikusema juu ya zile nchi ambazo tayari zilikuwa na slaa za nyuklia wazifanyeje, ndiyo maana hadi leo idadi ya silaa za nyuklia zilizopo kila nchi zinajulikana idadi yake, Urusi inaongoza na inafuatia Marekani, hairuhusiwi kuongeza hata silaa moja zaidi ya zile zilizokuwapo, azimio litakalofuata ni kuziteketeza silaha hizi zisiwepo duniani, bado teknolojia isiyokuwa na madhara ya kuziteketeza haijapatikana ndiyo sababu wameambiwa wayahifadhi kwanza chini ya uangalizi wa UN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unayafahamu. FOB na MOB?
 
Sasa wewe mleta mada mbona huoni bangi yako imekufanya ulete mada ya kitoto ,kiushenzi na mambo yasiohusiana?
 
Magazeti ya Kenya yanahaha vipi wakati ni kweli kabisa UN inaichunguza Tanzania juu ya madai ya kununua silaha za vita kutoka North Korea??
Inaichunguza ili iweje? [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakitugaia tunapokea tu. Tena inabidi watupe kwa lazima kwa kuwa wao wameendelea sana kwa sababu ya sisi hususan kipindi cha ukoloni
Tuache hii tabia ya kutafuta visingizio vya kijinga jinga.

Kama wao walituibia rasilimali zetu, sisi tulikubali vipi watuibie kama sio uzwazwa

Upendo ni tiba.
 
Tuache hii tabia ya kutafuta visingizio vya kijinga jinga.

Kama wao walituibia rasilimali zetu, sisi tulikubali vipi watuibie kama sio uzwazwa

Upendo ni tiba.
Tulijitahidi kupigana nao lakini tulishindwa, wakatutawala kimabavu. Mf majimaji war, mkwawa nk
 
Hao NK ni ndugu zetu mbele yao nyuma yetu[emoji120] [emoji120]
 
Hivi wewe huwa unaamini kwenye hizi sijui UN, WB, ama IMF? Hizo ni taasisi za USA na Ulaya.

Zipo kwa ajili ya maslai yao na zinakuwa toothless pindi zinapokinzana na maslai yao.

Ndio maana UN walikataa uvamizi wa Iraq lakini marekani akavamia tu.
Hivyo ni vyombo vya kifara sana[emoji51] [emoji51]
 
JF J-7 ni ya kichina na wakufunzi ni wachina. Vipi Leo waje wakorea kazkazni kutengeneza J-7... Au kwakuwa macho yao yafanana..
 
Naomba kueleweshwa kwa mnaojua zaidi, hivi Tz ni nchi huru na hatufungamani na upande wowote? Sasa kununua silaha sehemu yoyote tutakayotaka si ni sawa? Sasa kwa nini tuchunguzwe na UN?!! Au aina ya silaha tulizonunua hazitakiwi na UN?!!! Msaada wajuvi. Asante.
 
Mkuu kama nchi imewekewa vikwazo na UN basi dunia nzima inapaswa kutii vikwazo hivyo, kumbuka nchi zote zinawakilishwa pale UN, kwa hiyo ni kama maamuzi ya dunia nzima, japo kuna wakubwa yaani nchi zenye kura ya veto na sisi wadogo, North Korea iliwekewa vikwazo vya silaa, yaani isinunue, kuuza wala kushirikiana na nchi yoyote katika mambo yanayohusu silaa, sasa hivi imewekewa vikwazo vya uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…