Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
You wish....
Kubenea kachemsha - FACT!
Tanzania ina matatizo, watu hawaelewi kuwa kichwa cha habari tu cha kwenye magazeti kiaweza kupotosha kundi kubwa sana la wananchi?
Inabidi tufike mahali tuwe serious kidogo, asilimia kubwa ya magazeti ya leo yameandika kuwa mahakama imemsafisha Rostam kwenye ishu ya Richmond.....hivi kweli tutafika huko tuendako???
Kwenye gazeti lako kichwa cha habari umeandikaje?..
Unani-rank so high na kunipa ujiko nisio stahili sina uwezo (kipesa na kiakili ) wa kumiliki hata usambazaji wa flyers mitaani seuze gazeti!
Sikufika huko kaka, samahani kama nimekukwaza.
"Naona ni kweli kilichoandikwa maana hata RAIA MWEMA nanukuu"kwa mujibu wa nakala ya hukumu ambayo raia mwema imeipata. ROSTAM ANATAKIWA SASA KULIPWA FEDHA HIZO KAMA FIDIA YA KUKASHIFIWA KATIKA HABARI ZILIZOANDIKWA NA MWANAHALISI"mwisho wa kunukuu. Sasa waungwana kama hivyo ndivyo ilivyo si itakuwa kweli mahakama imeona luwa alionewa kuhusishwa na RICHMOND mie naona kama vyombo vya habari vya umma viko upande wake itashindikana nini kwa mahakama ni lini mahakama zetu zilikuwa huru?"
Hoops:
Tatizo lenu ni kwamba CCM imewdumaza sana fikra zenu -- zimegangamala. Jamaini mwenye hiyo "Order" ya jaji Makaramba aiweke humu ili watu wenye fikra finyu waisome. Mimi ninayo nakala lakini I'm sorry to say that I dont know how to post it.
Hakuna mahala ambapo "Order" hiyo inasema Rostam kasafishwa -- yaani Richmond siyo yake. Hawezi Jaji kusema hivyo kwa sababu shauri halikusikilizwa -- upande mmoja haukuwepo kujibu.
Kweli hela za mafisadi zinapunguza uwezo wa kufikiri.
Unauliza pingu Polisi?Habari leo,TBC1 kulikoni?
Mkulu RwabugirI: ninayo hard copy tu. Lakini kwa kuwa hukumu yenyewe ina mistari 13 tu naona niitoe tu hapa kwa manufaa ya wana-JF ambao hawajui Jaji aliandika nini. Hukumu, au Order ilitolewa tarehe 30.4.09 mbele ya wakili wa RA aitwaye Fungamtama:
Court: I have listened carefully to the submissions of Mr Fungamtama, learned Counsel for the plaintiff that this court pronounce on the strength of Order 8 Rule 14 of the CPC, judgement against all defendants for failure to file WSD. The learned Counsel has also cited the case of Kilindu Vs CRDB. The provisions of Rule 14 of Order VIII of the CPC are mandatory and there is no room for exercise of discretion. The defendants Counsel was present when this court has made orders for judgement to be delivered today but for reasons not entirely clear to this Court they have not appeared. In the circumstances and for reason that the defendants have failed to defend the suit, on strength of Rule 14(1) of Order VIII Judgement is hereby entered against all the defendants. Order accordingly.
Order: (1) Judgement entered against all defendants.
Signed: R.V. Makaramba
JUDGE
30.04.2009^^^^^^^^^^^^^
JE KUNA MAHALA POPOTE MAKARAMBA KASEMA KUWA ROSTAM SIYO MMILIKI AU HAHUSIKI NA RICHMOND?
RA ndiye "mwenye" nchi hii. Ndio maana mawaziri walishindana kumtetea. Inaonekana kuwa vyombo vya habari vya Serikali na vya CCM vyote "vinawajibika" kumtetea kwa nguvu zote. Wote wanajipendekeza tu kwa RA. Mkuchika kamsakizia Mzee Bendera kusema pumba; anamsema jasiri Mengi wanamuogopa fisadi Rostam, Wanaisema ITV wanaiacha TBC.
Viongozi serikalini wanamuogopa vibaya RA, ati ana ubavu na vibarua vyao.
Masikini Tanzania!