Hivi ni kweli kuwa ung'oaji wa magego (Meno ya kutafunia) ya juu usiozingatia utaalam huweza kupelekea upofu au kifo kwa asilimia kubwa?
- Tunachokijua
- Kinywa cha binadamu aliyekomaa huwa na meno 32 ambayo mpangilio wa anatomia huyaweka kwenye makundi manne yenye majina ya Incisors, Canines, Premolars na kundi la mwisho la Molars ambalo ndilo hubeba magego.
Kazi kubwa ya meno haya (Magego) ni kusaga chakula ili kiweze kimeng’enywa kirahisi kinapoingia tumboni.
Vifo na upofu utokanao na kung’oa meno haya
Ung’oaji wa meno hupaswa kufanywa na mtaalam wa afya aliye na ujuzi wa kutosha ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kumkuta mgonjwa.
Madhara yanayoonekana mara nyingi ni;
- Homa kali
- Uvimbe
- Maumivu makali
- Kuvuja kwa damu
- Maambukizi
Ushauri
Baada ya kufanyiwa huduma hii, mgonjwa anashauriwa kuzingatia ushauri aliopewa ikiwemo kumeza dawa za kupunguza maumivu, homa na kuzuia maambukizi kwa wakati ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa afya yake, madhara ambayo yasiposhughulikiwa mapema yanaweza kugharimu uhai.