Magerezani hali ni mbaya kunahitajika mageuzi

Magerezani hali ni mbaya kunahitajika mageuzi

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Hali inatisha! Hata kama wako pale kutumikia adhabu lakini ni familia yako pia, kuna msemo kwamba wanakula bure mimi napinga, wanalima, wanatengeneza fanicha! Wanaingiza pesa! Kwanini wasinunuliwe vijigodoro vile vidogo kila mfungwa akalala peke yake?

Kwanini godoro moja walale wanne mpaka nane na wakiwa bila nguo? Kwani wakipewa vigogoro hawatakuwa gerezani? Kama serikali haiwezi, iruhusu watu binafsi wenye uwezo wasaidie magereza!
 
Kama hujui, mfumo wa magereza huko US hutumika kama mbadala wa ‘SLAVERY’ ambayo ilishapigwa stop mwaka 1898. Prisons ni mfumo mbadala wa kufaidi jasho la mtu bila kumlipa.

Marekani walikuwa wanahakikisha magereza yanajaa black prisoners ili wakatumikishwe kwenye ujenzi wa reli bila malipo, unasingiziwa hata bangi tu, ili mradi wapate free forced labour.
 
Magereza yamekua kama kuzimu kazi ngumu hamna vitendea kazi Magereza ya Kilimo kazi na adhabu zinatisha chakula ni mara moja kwa siku Magereza kama Kitai-Mbinga na Songwe wanalima sana ila chakula hamna pia upande wa kulala ni taabu watu wanalala kama njiti kwenye kiberiti nguo nazo ni kuukuu vipigo kutoka kwa Askari jela na manyapara ni balaa kula ni ubabe wafugwa wenye majeraha hawatibiwi hadi wanatoka usaha na kuoza.

Wafugwa wagonjwa hawatibiwi kufia gerezani ni kawaida hakika magereza sio kumbadili mtu bali ni kumuonea na kumfanya mtu sugu. Nasema haya kwa uzoefu nilioupata baada ya kukaa magereza mawili hapa nchini.
 
Tatizo la wafungwa kuishi Maisha Magumu Ni kutokana na idadi kubwa ya Mahabusu waliopo Gerezani Unakuta mahubusu niwengi kuzidi wafungwa ,while wafungwa ndo wanaojishughulisha na uzalishaji

Naongea nikimaanisha kuwa ili "nalo mkalitazame"
 
Magereza yote makubwa yapo na Idadi 60% mahubusu na kesi ya mauaji ndo nyingi

Endapo Serikali ingeweka mipango madhubuti ya kuhakikisha inapunguza idadi ya mahubusu ili Chakula wanacholima kiwatoshe wafungwa wore na mahubusu wachache
 
Magereza yamekua kama kuzimu kazi ngumu hamna vitendea kazi Magereza ya Kilimo kazi na adhabu zinatisha chakula ni mara moja kwa siku Magereza kama Kitai...
Na hakuna anayejali. Kuna moments bila ya kuzipitia unakuwa hujui pains zake once unapokuwa victim you start to realize that hell is empty all devil's are here.
 
Kama hujui, mfumo wa magereza huko US hutumika kama mbadala wa ‘SLAVERY’ ambayo ilishapigwa stop mwaka 1898. Prisons ni mfumo mbadala wa kufaidi jasho la mtu bila kumlipa...
Huko US na other western nations, magereza sio sehem ya hovyo. Kufungwa itoshe kuwa ni adhabu. Hizi kazi za sulubu na uchafu, sio busara
 
Na kuna kiongozi wa Bulgaria alitaka waongezewe dhahma magerezani hadi wajute kuzaliwa.Mungu na wanadamu.
 
Magereza yamekua kama kuzimu kazi ngumu hamna vitendea kazi Magereza ya Kilimo kazi na adhabu zinatisha chakula ni mara moja kwa siku Magereza kama Kitai...
It's time waruhusu jamaa wa wafungwa wawapelekee magodoro maana wao wameshindwa kuwahudumia. Ustaarabu wa jamii hupimwa kwa kuangalia ni namna gani wanahudumia wale ambao ni most vulnerable
 
madhara mengine ya kuwapa watu wenye akili uongozi kwenye jamii.

Askari polisi huku uraiani na baadhi ya watu waliopewa mamlaka hupeleka watu hovyohovyo mahabusu hata wasio na makosa au makosa mepesi mepesi ambayo wanaweza kuyamaliza kwa hekima na busara.

Mahakama nazo zinahukumu hata wezi wa kuku kwenda jela huku wangeweza kuwapa adhabu nyingine kali kuliko kwenda jela.
 
Hali inatisha! Hata kama wako pale kutumikia adhabu lakini ni familia yako pia, kuna msemo kwamba wanakula bure mimi napinga, wanalima, wanatengeneza fanicha! Wanaingiza pesa! Kwanini wasinunuliwe vijigodoro vile vidogo kila mfungwa akalala peke yake?

Kwanini godoro moja walale wanne mpaka nane na wakiwa bila nguo? Kwani wakipewa vigogoro hawatakuwa gerezani? Kama serikali haiwezi, iruhusu watu binafsi wenye uwezo wasaidie magereza!

Walale ili waote wasahau kilichowapeleka huko?ile maisha wanayoishi yapo kwenye notes board kabisa kwamba leo kulala kifua wazi kesho hakuna kulala ni kukaa tuu kesho kutwa kulala chini hivyo hivyo!
Sory mkuu wewe ulipewa kesi gani
 
Hali inatisha! Hata kama wako pale kutumikia adhabu lakini ni familia yako pia, kuna msemo kwamba wanakula bure mimi napinga, wanalima, wanatengeneza fanicha! Wanaingiza pesa! Kwanini wasinunuliwe vijigodoro vile vidogo kila mfungwa akalala peke yake?

Kwanini godoro moja walale wanne mpaka nane na wakiwa bila nguo? Kwani wakipewa vigogoro hawatakuwa gerezani? Kama serikali haiwezi, iruhusu watu binafsi wenye uwezo wasaidie magereza!
Hii kulala Pamoja Bila Nguo si Watapigana Sana Pipe Jama
 
Magereza yote makubwa yapo na Idadi 60% mahubusu na kesi ya mauaji ndo nyingi

Endapo Serikali ingeweka mipango madhubuti ya kuhakikisha inapunguza idadi ya mahubusu ili Chakula wanacholima kiwatoshe wafungwa wore na mahubusu wachache
Kwanini mahabusu hawafanyi kazi? Kufanya kazi siyo adhabu ni wajibu, mbona huku uraiani tunafanya kazi kulima, kufuga, ujenzi, kuponda kokoto na tunapata pesa kusaidia familia zetu nk, siyo adhabu.
 
Unajua maana ya Mahabusu?
Kwanini mahabusu hawafanyi kazi? Kufanya kazi siyo adhabu ni wajibu, mbona huku uraiani tunafanya kazi kulima, kufuga, ujenzi, kuponda kokoto na tunapata pesa kusaidia familia zetu nk, siyo adhabu.
 
Daa,mi naumia kweli jinsi dunia inavyokwenda😭😭
 
Na hakuna anayejali. Kuna moments bila ya kuzipitia unakuwa hujui pains zake once unapokuwa victim you start to realize that hell is empty all devil's are here.
Mama aliposhauriwa aachie baadhi ya wafungwa alisema nguvu kazi itapungua sababu dhaifu kabisa pia inashauriwa wajenge zaidi makambi na sio ngome ushauri ambao haujafanyiwa kazi kabisa Magereza ya Tanzania ni bora ufe ndio maana baadhi ya wafungwa wanatoroka ili wapigwe risasi wafe waondokane na mateso
 
Hilo la kulala uchi Tena wakiwa 8 godoro moja ni la kulipigia kelele kabisa..

Hapo lazima amwagiwe mtu,,,

Africa magereza ni nusu jehanam.
 
Back
Top Bottom